simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for the ‘Breaking News’ Category

Book: Economic Integration in Africa

leave a comment »


 

Economic Integration in Africa
The East African Community in Comparative Perspective

 

Overview

In this work, Richard E. Mshomba offers an in-depth analysis of economic integration in Africa with a focus on the East African Community (EAC), arguably the most ambitious of all the regional economic blocs currently in existence in Africa. Economic Integration in Africa provides more than just an overview of regional economic blocs in Africa; it also offers a rich historical discussion on the birth and death of the first EAC starting with the onset of colonialism in the 1890s, and a systematic analysis of the birth, growth, and aspirations of the current EAC. Those objectives include forming a monetary union and eventually an East African political federation. This book also examines the African Union’s aspirations for continent-wide integration as envisioned by the Abuja Treaty. Mshomba carefully argues that maturity of democracy and good governance in each country are prerequisites for the formation of a viable and sustainable East African federation and genuine continent-wide integration.

  • Examines economic integration in Africa from a historical, economic, and political perspective, showing the confluence of history, economics, and politics in shaping the pace of economic integration
  • Focuses on one regional economic bloc (the East African Community) while at the same time maintaining a broader perspective by considering continent-wide integration efforts
  • Presented in chronological order, making historical developments easy to follow

 

Reviews & endorsements

Advance praise: ‘To date, we have lacked authoritative studies of some of Africa’s most important regional organizations, which has undermined our understanding of how African states engage with one another. Richard E. Mshomba has filled this gap for the East African Community, providing a thorough, clearly written and persuasive account of its strengths and weaknesses. This volume represents a significant contribution to the debate, and will be an important touchstone for academics, policy makers and practitioners alike.’ Nic Cheeseman, University of Birmingham

Advance praise: ‘Professor Richard E. Mshomba has produced an outstanding study that should be of utmost value to a wide variety of scholars, students, and policy practitioners. In cogent and compelling language, he has clarified the economic challenges and opportunities of regional economic federations; he has brought us a compelling history of the efforts to achieve regional economic integration in Eastern Africa. His analysis and conclusions will be of interest to scholars of economic integration throughout the developing world.’ Michael F. Lofchie, University of California, Lost Angeles.

 

Read more at http://www.cambridge.org/us/academic/subjects/economics/economic-development-and-growth/economic-integration-africa-east-african-community-comparative-perspective#WKeKLgeys6DpwZ4F.99

Written by simbadeo

October 17, 2017 at 6:50 pm

Unatafuta Ajira? Tangazo hili linakuhusu …

leave a comment »


wanaotafuta ajira

Pengine ni namna nzuri ya kuuanza Mwaka Mpya 2016. Jifunze kitu kipya. Shiriki ili kuona fursa mpya. Jipatie maarifa. Jiongezee ujuzi. Ongeza idadi ya marafiki unaofahamiana nao (networking). Kwa hakika ni fursa ya pekee.

Happy Independence (Uhuru) Day

leave a comment »


Uhuru Day Tanzania

Thank you Google for making this day even more special to Tanzanians wherever they may be on planet earth. Uhuru na Kazi/Freedom and Work = Accountability. Pamoja sana.

Daraja la Kinyerezi: Sasa linapitika …

with 2 comments


Daraja Kinyerezi vvv

Naam. Hivi sasa linapitika — toka jana. Sasa masika inaruhusiwa kumiminika kama kawaida yake … maana ingalikuja kwa nguvu wiki tatu nne zilizopita … ingalikuwa majanga zaidi.

Pamoja sana.

Daraja la Kinyerezi: Hatimaye matumaini yarejea …

with 2 comments


Darajani 7 April xx

Baada ya mahangaiko haya …

Darajani 7 April xxxx

… na haya yaliyodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja, hatimaye matumaini yanaanza kurejea.

Darajani 7 April x

Daraja lilifika nusu …

Darajani 7 April xxx

… na kisha jana lilifika mwisho mwingine. Kazi iliyokuwa imebaki ni kutandaza sakafu.

Kasi ilikuwa ndogo … ya kusuasua sana. Pamoja na hayo pongezi kwa mamlaka yoyote iliyovalia njua dharura hii hadi sasa matumaini yanarejea. Pengine tusiishie hapo. Daraja ni mali adimu ya umma. Gharama yake ni zaidi sana ya zile tu za ujenzi na ununuzi wa vifaa … gharama yake ni pamoja na huduma inayotolewa na daraja hilo, ni vigumu kuikadiria. Kwa sababu hiyo, miundombinu kama madaraja ni muhimu yalindwe usiku na mchana. Ulinzi wenyewe uwe mkali kwelikweli. Nchi haiwezi kumudu kupoteza au kucheleweshewa maendeleo kwa sababu ya mtu fulani mzembe au mwenye tamaa zake. Hilo ni ni muhimu lieleweke na kuwekwa vichwani.

Pamoja sana.

Hali tete Daraja la Kinyerezi na Majumba Sita

leave a comment »


Darajani 22 march 1

Darajani 22 march 4

Darajani 22 march 2

Darajani 22 march 7

Darajani 22 march 6

Kwa ufupi, hii ni kuhatarisha maisha ya wapiga kura katika nchi hii. Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu daraja la muda livunjike wakati lori la kuchanganya zege likipita juu yake. Hadi wakati huu, sijasikia tamko lolote kuhusu mpango uliopo wa kurekebisha hali ya mambo. Sijamsikia Mbunge wa Ukonga wala Madiwani wa Kata za Ukonga, Kipawa, Segerea wala Kinyerezi akizungumzia suala hili. Sijamsikia Waziri wa Ujenzi akisema lolote kuhusiana na tatizo lililopo.

Pengine wakuu hao wanasubiri mtu au watu wapoteze maisha na mali zao kisha ndio wajitokeze. Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo. Watu wanaojaribu kuvuka kwa kutumia vyuma vya daraja lililovunjika wanafanya hivyo kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao. Eneo si salama. Mawasiliano kati ya pande mbili hakuna. Hakuna gari wala pikipiki inayoweza kuvuka hapo wakati huu. Na huu ni mwanzo tu wa mvua za masika.

Chondechonde, serikali ilitazame eneo hili kwa namna ya pekee. Naamini tuna wahandisi wengi wazalendo wenye uwezo wa kubuni suluhisho la muda wakati daraja la kudumu likiendelea kujengwa. Hakika katika hili hatutawaelewa ikiwa hamtakuja na majibu ya haraka.

Ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe. Kuna wazee, watoto, akina mama na wananchi wengine wengi wanaotumia barabara na daraja hili. Hivi sasa watoto wa upande mmoja wanaosoma shule upande mwingine, hawana tena fursa ya kwenda shule. Pale hapavukiki. Vivyo hivyo kwa watoto wa upande mwingine. Kwa watu wazima, watalazimika kupata adhabu ya kuzunguka njia ndefu ili kwenda kutafuta riziki za watoto wao na kodi mbalimbali wanazolipa serikalini. Maana yake, maisha yatakuwa ghali zaidi.

Kinachotakiwa hapa ni uamuzi mgumu. Mtuthibitishie kuwa mnaweza kufanya uamuzi mgumu na kuwarejeshea mawasiliano wapiga kura wenu.

Kwa pamoja, tunaweza.

Dar es Salaam: Lori lavunja Daraja la Kinyerezi tena

with 2 comments


Ikiwa ni miezi michache tu tangu daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita kuvunjwa na lori lililosheheni matofali, leo hii tena, majira ya saa moja usiku lori lingine la kuchanganya kokoto limevunja daraja hilo.

Alama za barabarani huonyesha kuwa daraja hilo — ambalo ni la muda na lililotengenezwa kwa vyuma tupu — lina uwezo wa kubeba uzito usiozidi tani saba (7).

Kama ilivyokuwa safari ya kwanza, kuvunjika kwa daraja hili kunasababisha kero kubwa ya usafiri kwa wanaotumia barabara hii muhimu ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza kutoka katika Gereza la Segerea. Tayari kulikuwa na msururu wa mamia ya magari kila upande wa daraja, huku yakipeana muda kuvuka katika Bonde la Mto Msimbazi kwa kutumia barabara ya dharura inayopita kwenye eneo la mto. Barabara hiyo ina uwezo wa kupitisha gari moja tu kwa wakati mmoja — yaani, magari mawili hayawezi kupishana.

 

Daraja Kinyerezi 1

Picha zaidi hizi hapa (ubora wa picha zi mzuri kwa sababu ya eneo hilo kutawaliwa na giza wakati wa usiku):

Daraja Kinyerezi 2

Lori lililoanguka usiku huu.

Daraja Kinyerezi 4

Utambulisho wa lori hilo.

 

Daraja Kinyerezi 5

Sehemu ya shehena ya zege ikiwa imemwagika kutoka kwenye lori hilo. Wakati picha hii inapigwa tayari zege hilo lilikuwa limeshaanza kukauka.

 

Daraja Kinyerezi 6

Utambulisho mwingine wa lori hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakuwa tayari kutajwa kwa sababu wao si wazungumzaji rasmi, dereva na utingo wake walinusurika na kutiwa mbaroni na walinzi wa daraja.

Kwa hakika, wakati ambapo haijulikani ni lini daraja hili la muda litatengenezwa tena, wananchi wa maeneo jirani na watumiaji wengine wa barabara hii wajiandae kwa kero kubwa ya usafiri. Miongoni mwa watakaotaabika ni pamoja na wanafunzi ambao hufuatwa majumbani na mabasi ya shule wanakosoma. Wakati huohuo, mwezi Machi huwa ni mwanzo wa msimu wa masika katika Jiji la Dar es Salaam. Mara mvua zitakapoanza kunyesha, hata barabara ya muda itapitika kwa taabu sana, na hivyo kufanya eneo hili kutokuwa na mawasiliano na upande wa pili.

 

 

Homa ya Kutisha … Dengue … Wakinge Uwapendao

with 2 comments


Sote tujitahidi kuzingatia maelekezo haya. Ni kwa kushirikiana tu ndio tutaishinda homa hii hatari. Jikinge na wakinge wengine dhidi ya Homa ya Dengue. Ni homa hatari ya virusi vinavyoenezwa na mbu. Pamoja Tutashinda.

Sote tujitahidi kuzingatia maelekezo haya. Ni kwa kushirikiana tu ndio tutaishinda homa hii hatari. Jikinge na wakinge wengine dhidi ya Homa ya Dengue. Ni homa hatari ya virusi vinavyoenezwa na mbu. Pamoja Tutashinda.

Written by simbadeo

May 6, 2014 at 11:27 pm

Papa John Paul II na Papa John XXIII … Watangazwa watakatifu

leave a comment »


Papa Francis akielekea madhabahuni kuongoza ibada maalumu ya Misa ya kuwatangaza watakatifu Papa John Paul II na Papa John XXIII huko Jijini Roma, Italia.

Papa Francis akielekea madhabahuni kuongoza ibada maalumu ya Misa ya kuwatangaza watakatifu Papa John Paul II na Papa John XXIII huko Jijini Roma, Italia.

Papa John Paul II na John XXIII watangazwa watakatifu

Vatikano imewatangaza leo hii mapapa wawili maarufu wa Karne ya 20 — John Paul II na John XXIII — kuwa Watakatifu katika sherehe zilizofana katika Jiji la Roma.

Chanzo: BBC World

Written by simbadeo

April 27, 2014 at 11:58 am

Waziri Mkuu ajiuzulu … Ni baada ya kivuko kuzama

leave a comment »


Ndugu wa watu wanaohofiwa kufa maji baada ya kuzama kwa kivuko kule Korea Kusini wakifuatilia taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw Chung, akitangaza kujiuzulu.

Ndugu wa watu wanaohofiwa kufa maji baada ya kuzama kwa kivuko kule Korea Kusini wakifuatilia taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw Chung, akitangaza kujiuzulu.

Huyu si mwingine bali ni Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Bw Chung Hong-won. Amejiuzulu kufuatia serikali yake kukosolewa vikali kwa namna ilivyoshughulikia tukio la kuzama kwa kivuko.

Katika taarifa yake, Bw Chung, aliyeonekana mnyonge, alisema: “vilio vya familia za watu ambao bado miili yao haijapatikana vinanifanya kukesha usiku kucha”.

Kivuko cha Sewol kikiwa na abiria 476 — wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu — kilizama katika bahari huko Korea Kusini mnamo tarehe 16 Aprili.

Maofisa wamethibitisha kuwa watu 187 walifariki dunia, lakini kuna makumi wengine ambao hawajapatikana na wanahofiwa kuwa wamekufa maji.

“Kwa niaba ya serikali, ninaomba msamaha kwa matatizo mengi kuanzia kushindwa kuzuia kutokea kwa ajali hadi namna ilivyoshughulikiwa.”

Ndugu wenye hasira wamekuwa wakitoa shutuma kali dhidi ya kile kilichoonekana kama uzembe katika kuendesha operesheni ya uokoaji.

“Jambo sahihi kwangu kufanya ni kuwajibika na kujiuzulu kama mtu niliyekuwa kiongozi wa baraza la mawaziri,” alisema Bw Chung katika taarifa fupi iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni.

Aliongeza: “Kumekuwa na matatizo mengi yaliyoendelea kutokea katika jamii yetu pamoja na utendaji ambao umekwenda kombo. Nina imani kuwa safari hii maovu haya yaliyojikita katika jamii yatasahihishwa na kuwa aina hii ya ajali hazitatokea tena.”

Hakukuwa na taarifa iliyopatikana mara moja kutoka kwa Rais Bi Park Geun-hye kama alikubali kujiuzulu kwa Bw Chung.

 

Chanzo: BBC World

Swali: Utamaduni huu wa kuwajibika kutokana na upungufu unaojitokeza katika uongozi utaota lini mizizi barani Afrika?

Written by simbadeo

April 27, 2014 at 11:37 am