simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Hali tete Daraja la Kinyerezi na Majumba Sita

leave a comment »


Darajani 22 march 1

Darajani 22 march 4

Darajani 22 march 2

Darajani 22 march 7

Darajani 22 march 6

Kwa ufupi, hii ni kuhatarisha maisha ya wapiga kura katika nchi hii. Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu daraja la muda livunjike wakati lori la kuchanganya zege likipita juu yake. Hadi wakati huu, sijasikia tamko lolote kuhusu mpango uliopo wa kurekebisha hali ya mambo. Sijamsikia Mbunge wa Ukonga wala Madiwani wa Kata za Ukonga, Kipawa, Segerea wala Kinyerezi akizungumzia suala hili. Sijamsikia Waziri wa Ujenzi akisema lolote kuhusiana na tatizo lililopo.

Pengine wakuu hao wanasubiri mtu au watu wapoteze maisha na mali zao kisha ndio wajitokeze. Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo. Watu wanaojaribu kuvuka kwa kutumia vyuma vya daraja lililovunjika wanafanya hivyo kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao. Eneo si salama. Mawasiliano kati ya pande mbili hakuna. Hakuna gari wala pikipiki inayoweza kuvuka hapo wakati huu. Na huu ni mwanzo tu wa mvua za masika.

Chondechonde, serikali ilitazame eneo hili kwa namna ya pekee. Naamini tuna wahandisi wengi wazalendo wenye uwezo wa kubuni suluhisho la muda wakati daraja la kudumu likiendelea kujengwa. Hakika katika hili hatutawaelewa ikiwa hamtakuja na majibu ya haraka.

Ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe. Kuna wazee, watoto, akina mama na wananchi wengine wengi wanaotumia barabara na daraja hili. Hivi sasa watoto wa upande mmoja wanaosoma shule upande mwingine, hawana tena fursa ya kwenda shule. Pale hapavukiki. Vivyo hivyo kwa watoto wa upande mwingine. Kwa watu wazima, watalazimika kupata adhabu ya kuzunguka njia ndefu ili kwenda kutafuta riziki za watoto wao na kodi mbalimbali wanazolipa serikalini. Maana yake, maisha yatakuwa ghali zaidi.

Kinachotakiwa hapa ni uamuzi mgumu. Mtuthibitishie kuwa mnaweza kufanya uamuzi mgumu na kuwarejeshea mawasiliano wapiga kura wenu.

Kwa pamoja, tunaweza.

Inakuhusu. Inanihusu. Inatuhusu

with 2 comments


pic albino

Ndugu zangu,

Bila shaka kila mmoja wetu amesikia kuhusu mauaji yanayofanywa dhidi ya ndugu zetu wenye albinism. Kwa watu waliojitambua na kuvuka imani potofu, watu wanaofikiri kisayansi wanaumizwa sana na matukio haya. Watu wote wenye mapenzi mema wanachukizwa kuona ndugu, jamaa, rafiki, jirani na Watanzania wenzao wakiuwawa eti kwa sababu ya vile walivyoumbwa.

Wakati ambapo ninaungana na watu wote wenye mapenzi mema katika kukemea uovu huu mkuu, nimkumbushe kila mmoja wetu kuwa: Kuuwawa kwa wenzetu wenye albinism hakutuweki sisi salama. Watu wenye imani potovu na wale wanaowachochea kuendelea kuishikilia imani hiyo isiyo na maana hawana mipaka. Kesho, watazua mengine: watasema tafuta viungo vya mtu mwenye kipara, ni dili! Keshokutwa watasema, tafuta watu wanene wanene kidogo! Siku nyingine watasema, watu wembamba. Safari nyingine watazua watu warefu; wafupi; maji ya kunde; weusi sana; wang’avu n.k. Hawana mwisho hawa.

Kwa hiyo, dawa yake ni moja: kukomesha mauaji ya wenzetu wenye albinism sasa na kufutilia mbali kabisa imani potofu.

Kwa pamoja tunaweza. Kumbuka: INAKUHUSU. INANIHUSU. INATUHUSU. Sambaza ujumbe.

Indigenous Trees/Miti ya Asili … Naomba Majina

with one comment


Hi friends,

I’m looking for names of these indigenous trees. If you happen to know any, please share it with me here.

Salamu marafiki,

Ninatafuta majina ya miti hii ya asili. Kama unajua jina lolote tafadhali nishirikishe.

Thank you very much/Asante sana.

Simba

Mti Asili 1

Mti Asili 2

Mti Asili 3

Mti Asili 4

Mti Asili 5

Mti Asili 6

Mti Asili 7

Mti Asili 8

It will also be great to learn the use of each tree and whether there is any to be avoided for whatever reason.

Itakuwa jambo la kufurahisha kufahamu matumizi ya kila mti na kama kuna mti ambao mtu hana budi kuuepuka kwa sababu zozote.

Cheers.

Dar es Salaam: Daraja Kinyerezi – Maendeleo

leave a comment »


Daraja Kinyerezi 14

Hili ndilo Daraja la Kinyerezi-Majumbasita linaloendelea kujengwa. Hatua ya ujenzi iliyofikiwa inatia moyo. Lakini ni muhimu mkandarasi aongeze kasi. Wananchi wamechoka kuvunjikiwa na daraja la muda kila baada ya miezi michache. Ili kasi ya maendeleo iwe ya kutosha, ni muhimu miundombinu kama hii ijengwe katika kasi ya uhakika na kwa viwango bora. Endapo haya yamezingatiwa katika ujenzi wa daraja hili, basi litakuwa na mchango mkubwa sana kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa hili.

Mungu ibariki Tanzania.

Written by simbadeo

March 9, 2015 at 10:01 pm

Daraja la Kinyerezi, picha za mchana

leave a comment »


Daraja Kinyerezi 7

Daraja na lori, chali.

 

Daraja Kinyerezi 8

Sasa hivi magari yanapita chini kwenye eneo la Mto Msimbazi. Kasheshe itakapoanza masika.

 

Daraja Kinyerezi 10

Naam. Ndiyo hali ilivyo.

 

Daraja Kinyerezi 11

Na zege nalo lilimwagika.

 

Daraja Kinyerezi 12

Barabara ya mtoni.

 

Daraja Kinyerezi 9

Mitambo iliyoletwa ili kunyanyua lori lilipata ajali. Hata hivyo, mitambo ilishindwa kazi hiyo, kwani nayo iliishia kunasa kwenye mchanga. Zoezi lilishindikana hadi wajipange upya.

Dar es Salaam: Lori lavunja Daraja la Kinyerezi tena

with 2 comments


Ikiwa ni miezi michache tu tangu daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita kuvunjwa na lori lililosheheni matofali, leo hii tena, majira ya saa moja usiku lori lingine la kuchanganya kokoto limevunja daraja hilo.

Alama za barabarani huonyesha kuwa daraja hilo — ambalo ni la muda na lililotengenezwa kwa vyuma tupu — lina uwezo wa kubeba uzito usiozidi tani saba (7).

Kama ilivyokuwa safari ya kwanza, kuvunjika kwa daraja hili kunasababisha kero kubwa ya usafiri kwa wanaotumia barabara hii muhimu ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza kutoka katika Gereza la Segerea. Tayari kulikuwa na msururu wa mamia ya magari kila upande wa daraja, huku yakipeana muda kuvuka katika Bonde la Mto Msimbazi kwa kutumia barabara ya dharura inayopita kwenye eneo la mto. Barabara hiyo ina uwezo wa kupitisha gari moja tu kwa wakati mmoja — yaani, magari mawili hayawezi kupishana.

 

Daraja Kinyerezi 1

Picha zaidi hizi hapa (ubora wa picha zi mzuri kwa sababu ya eneo hilo kutawaliwa na giza wakati wa usiku):

Daraja Kinyerezi 2

Lori lililoanguka usiku huu.

Daraja Kinyerezi 4

Utambulisho wa lori hilo.

 

Daraja Kinyerezi 5

Sehemu ya shehena ya zege ikiwa imemwagika kutoka kwenye lori hilo. Wakati picha hii inapigwa tayari zege hilo lilikuwa limeshaanza kukauka.

 

Daraja Kinyerezi 6

Utambulisho mwingine wa lori hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakuwa tayari kutajwa kwa sababu wao si wazungumzaji rasmi, dereva na utingo wake walinusurika na kutiwa mbaroni na walinzi wa daraja.

Kwa hakika, wakati ambapo haijulikani ni lini daraja hili la muda litatengenezwa tena, wananchi wa maeneo jirani na watumiaji wengine wa barabara hii wajiandae kwa kero kubwa ya usafiri. Miongoni mwa watakaotaabika ni pamoja na wanafunzi ambao hufuatwa majumbani na mabasi ya shule wanakosoma. Wakati huohuo, mwezi Machi huwa ni mwanzo wa msimu wa masika katika Jiji la Dar es Salaam. Mara mvua zitakapoanza kunyesha, hata barabara ya muda itapitika kwa taabu sana, na hivyo kufanya eneo hili kutokuwa na mawasiliano na upande wa pili.

 

 

Kazi: Pengine ya kwako ni ngumu, tazama ya hawa…

leave a comment »


SAM_8637

Naam. Hii ni hatua ya katikati. Maana kazi yenyewe huanzia na kuangusha miti, kukata magogo na kisha kutengeneza matanuri. Ndugu huyu hapa anahakikisha kuwa tanuri la mkaa linaendelea vema.

 

SAM_9144

SAM_9146

Hatua nyingine ni usafirishaji. Kuna wanaobeba kwa vichwa, baiskeli, pikipiki na hata malori. Tafakari ugumu wa kazi ya wachoma mkaa. Linganisha na kazi yako. Huenda unalalamika kuwa kazi yako ni ngumu. Je, ni ugumu wa aina hii? Vipi kuhusu kipato kinachotokana na kazi yao, unakilinganisha vipi na cha kwako kwa kazi yako?

Angalizo

Wakati huohuo, ni muhimu tufanye jitihada kwa jamii yetu ya Watanzania ili tutoke katika matumizi ya mkaa. Yanaua mazingira. Yanaua maendeleo. Yanaua afya. Sasa tuna gesi. Tuhakikishe kwamba kila mmoja wetu anamudu gharama za gesi pamoja na zana zinazotakiwa ili tuhifadhi miti na misitu yetu.

Pamoja sana.

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,553 other followers