simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Daraja la Kinyerezi: Hatimaye matumaini yarejea …

with 2 comments

Darajani 7 April xx

Baada ya mahangaiko haya …

Darajani 7 April xxxx

… na haya yaliyodumu kwa zaidi ya mwezi mmoja, hatimaye matumaini yanaanza kurejea.

Darajani 7 April x

Daraja lilifika nusu …

Darajani 7 April xxx

… na kisha jana lilifika mwisho mwingine. Kazi iliyokuwa imebaki ni kutandaza sakafu.

Kasi ilikuwa ndogo … ya kusuasua sana. Pamoja na hayo pongezi kwa mamlaka yoyote iliyovalia njua dharura hii hadi sasa matumaini yanarejea. Pengine tusiishie hapo. Daraja ni mali adimu ya umma. Gharama yake ni zaidi sana ya zile tu za ujenzi na ununuzi wa vifaa … gharama yake ni pamoja na huduma inayotolewa na daraja hilo, ni vigumu kuikadiria. Kwa sababu hiyo, miundombinu kama madaraja ni muhimu yalindwe usiku na mchana. Ulinzi wenyewe uwe mkali kwelikweli. Nchi haiwezi kumudu kupoteza au kucheleweshewa maendeleo kwa sababu ya mtu fulani mzembe au mwenye tamaa zake. Hilo ni ni muhimu lieleweke na kuwekwa vichwani.

Pamoja sana.

Advertisements

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Nidhahiri zaidi kukubali na kujua kuwa dhamana ya kila mali iliyopo nchini na rasilimali pia isiyo lindwa na wananchi hupotea na kuharibika vibaya hivyo nijukumu la kila mwananchi ,

  Like

  A.Kangile

  April 12, 2015 at 9:52 pm

  • A. Kangile. Ni kweli, mwananchi ndiye anayepaswa kuwa mlinzi wa kwanza wa mali za umma. Hata hivyo, ni muhimu pia kuweka walinzi maalumu kwa mali nyeti za umma. Miundombinu kama madaraja inapoharibiwa, hasara ni kubwa kwa wananchi mmojammoja na kwa Taifa zima. Wananchi watimize wajibu wao wa kulipa kodi kama inavyostahili na kodi hiyo itumike kujenga miundombinu hiyo na kuweka walinzi wa kudumu ili asitokee yule anayejiona mjanja kuliko wote na kuihujumu. Asante sana kwa maoni yako. Pamoja sana.

   Like

   simbadeo

   April 13, 2015 at 12:18 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: