simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for the ‘Conflict’ Category

Tazara: Treni Daladala

leave a comment »


Tazara Daladala peak hour 1

Watu wakiwa katika Kituo Kikuu cha Garimoshi cha Tazara. Hawa wanasubiri kuruhusiwa kuingia katika garimoshi linalofanya safari kati ya Stesheni hiyo na viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam.

Tazara Daladala peak hour

Abiria baada ya kuruhusiwa kuingia katika mabehewa. Garimoshi moja katika safari hizi huwa na mabehewa yasiyopungua tisa (9). Katika nyakati ambako kuna abiria wengi, yaani asubuhi (kuelekea mjini) na jioni (kuelekea Mwakanga na vituo vya mbele). Nilichokiona katika safari niliyofanya ni udhaifu wa udhibiti wa mapato. Ukusanyaji nauli unafanyika kiholela. Ni rahisi mtu kulipa kiwango tofauti na kilichopangwa ili mradi hapewi risiti. Hii ina maana kuwa fedha hiyo itaingia kwenye mfuko wa aliyepewa dhamana ya kukusanya nauli. Kwa maana hiyo, shirika lisitegemee kuona mwujiza katika mapato yake katika kutoa huduma hii.

Nasi Watanzania tubadilike. Ili huduma kama hii udumu ni muhimu tutimize wajibu wetu. Mosi, tulipe nauli sahihi. Pili, tudai risiti halali katika kutumia huduma hiyo. Vinginevyo, huduma itakuwa mzigo kwa mamlaka na hatimaye kusitishwa. Jambo hilo likitokea, watakaoumia ni sisi.

Pamoja sana.

Advertisements

Ajira: Wanawake na Maendeleo

leave a comment »


Wanawake na Maendeleo

Ajira rasmi bado ni changamoto kubwa kwa nchi yetu. Kwa mujibu wa matokeo ya ‘Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kazi wa Mwaka 2014’ wa National Bureau of Statistics, kuna jumla ya watu 25,750,116 wenye uwezo wa kufanya kazi nchini. Miongoni mwao, Nguvu Kazi ya Taifa ni 22,321,924. Na kati ya hao kwenye kundi hilo la pili, walio kwenye ajira ni 20,030,139. Idadi hiyo ni jumla ya walio kwenye ajira rasmi na isiyo rasmi.

Kwa mujibu wa utafiti huo, sekta isiyo rasmi haijumuishi shughuli za kilimo. NBS inafafanua kuwa ni zile shughuli za kiuchumi zinazofanywa na mtu mmoja mmoja au na kaya lakini ambazo ni vigumu kisheria kuzitofautisha na wamiliki wake, kwani mara nyingi hazina akaunti zake zenyewe za benki, baadhi ya bidhaa wanazozalisha ni kwa ajili ya kuuza huku zikiajiri chini ya wafanyakazi watano.

Utafiti huo unaonyesha kuwa kuna kaya 4,338,070 zenye shughuli za kiuchumi zilizo katika sekta isiyo rasmi. Lakini utafiti unaonyesha kuwa wanaofanya kazi mmojammoja katika sekta isiyo rasmi ni watu 6,257,124.

Kwa hiyo, nchi yetu ina changamoto kubwa ya kuwaingiza hawa katika sekta rasmi. Ni kwa sababu ya ukosefu wa ajira rasmi siku hizi tunaanza kuona akina mama wakifanya shughuli za uchuuzi mijini. Shughuli hizi zilikuwa zikifanywa zaidi na akina baba. Hii ni kwa maana ya kubeba bidhaa na kuzitembeza kutafuta wateja.

Tulipe kodi ili kwa pamoja tulete mabadiliko katika uchumi wa nchi yetu.

Pamoja sana.

Room To Read … Writers’ Workshop

with 2 comments


20160211_150316

Deo Simba, Herieth Emmanuel, Upendo Naftari, Phabian Isaya, Elizabeth Shusha, Prisca Mdee (Trainer), Alison Ziki (Trainer), Mama Rehema Egbert, Mama Justa Mlyauki and Richard Mabala. Dar es Salaam. Tanzania. Feb 8 to 11, 2016. A great moment.

MV Logos Hope … Book Fair in Dar 2016

with one comment


20160213_133950

When it comes to books … children are highly interested. We are the mean ones for not spending as much as we should on books for children and for adults.

20160213_134527

And … Desmond Tutu … The Authorised Portrait …

20160213_133834

And … The Crowd … searching and searching …

Lushoto: On open market day

leave a comment »


Lushoto on open market day 2

Lushoto on open market day

It’s a beautiful day, beautiful people, beautiful weather. Open markets are always very interesting places to visit. They are full of life as money exchanges hands supported with a smile. Well, frowns are also there, especially when the day wears off and the sun leans to the west and one had not sold all that he or she had planned to sell. But, life must go on. Enjoy every moment as it comes. Cheers!

Magufuli: Tazama eneo hili pia

leave a comment »


Biashara ndogondogo Chalinze 1

Chalinze. Wachuuzi wengi ni wanaume.

Soni Akina mama wafanyabiashara

Soni, Lushoto. Wachuuzi wengi (kama sio wote) ni akina mama.

Mazao Biashara Ndogondogo 2

Mazao ya shamba. Masoko bora zaidi yanahitajika.

 

Ajira. Uchumi wa nchi hauwezi kukua endapo nguvukazi haitatumika vema kwa namna yenye kuleta tija kwao na kwa nchi. Wachuuzi walio hapo juu wanajitafutia riziki. Kile wanachopata hakiendani na nguvu wanayotumia. Tukiwa na utaratibu mzuri wa masoko — yaani kutafuta masoko ya uhakika — hawa watapata kipato kizuri zaidi. Hapo walipo ni vigumu kwao kulipa kodi (kama wanalipa basi ni ushuru kidogo unaokwenda halmashauri). Lakini wakiwa katika masoko maalumu, watapata kipato kizuri na kulipa kodi.

Mazingira wanayofanyia biashara pia si rafiki. Ni muhimu kubadili hali hii. Hivi sasa tunachokiona hapo juu kipo karibu kila kona, kila mji, kila njia kuu nchini Tanzania. Ni muhimu tubadili hii. Tunaweza tu kwa kufanya uchumi wetu ujiendeshe kwa nia zilizo rasmi. Kilimo kifanywe kwa tija na kwa njia zilizo rasmi, biashara ifanywe kwa njia rasmi. Serikali ifanye kazi kutafuta masoko ya uhakika kwa bidhaa zote zinazozalishwa nchini — za kilimo, mifugo, bahari, maziwa, mito na madini.

Ajira rasmi. Masoko ya uhakika. Kipato bora. Kulipa kodi. Kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara (ikiwemo miundombinu). Haya ndiyo baadhi ya mambo yatakayoleta mabadiliko chanya katika maisha ya Watanzania.

Pamoja sana.

Mshangao. Pale Chalinze wachuuzi ni wanaume (zaidi), kule Soni ni wanawake (zaidi). Sina majibu kwa hali hii. Je, Chalinze wanaotoka ni wanaume, wanawake wanabaki nyumbani? Je, kule Soni wanaotoka ni wanawake, wanaume wanabaki nyumbani? Kwa anayejua atujuze. Nafikiri kuna kitu cha kujifunza hapa.

… baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 … maisha yaendelee

with 2 comments


Bwama, Kisarawe, Tanzania

Bwama, Kisarawe, Tanzania

Uchaguzi Mkuu umepita. Suluhu kwa mgogoro wa Zanzibar inaendelea kutafutwa. Ni wakati wa kujenga Taifa. Kila mmoja pale alipo ajenge Taifa. Changamoto nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi zifanyiwe kazi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iundwe upya kwa kushirikisha wadau wote. Uwazi na uwajibikaji vipewe kipaumbele. Vyombo vya ulinzi na usalama vibaki kuwa mali ya umma — na si vya chama au mhimili fulani katika dola. Ubaguzi wa aina yoyote — ukabila, dini, rangi, asili, kipato, hadhi, ukanda — ni muhimu ufutwe, tena haraka. Vinginevyo, tutakuwa tunakata tawi la mti tulilolikalia. Huenda tusione madhara ya ubaguzi mapema, lakini wakati utafika ambapo hakuna atakayekuwa salama. Tanzania mpya inawezekana. Tanzania ya haki na amani ya kweli inawezekana. Sote tuna wajibu. Pamoja sana.