simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for the ‘afya’ Category

Dar Streets Series: BRT on the Scene

leave a comment »


BRT Dar 2

And another

BRT Dar 1

The rapid bus service is a new addition to the city. Commuters using the services cut the time they spend on the road by about 70 per cent. What an improvement! Imagine, spending only half an hour from the Kimara suburb to the Central Business District. Using ordinary commuter buses would normally take not less than an hour and a half!

Advertisements

Dar Street Series: Jet point along Nyerere; Kipawa Fish Market

leave a comment »


 

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Jet area along Julius Nyerere Road in Dar es Salaam.

 

OLYMPUS DIGITAL CAMERA

Customers at the Kipawa Fish Market along Nyerere Road, Dar es Salaam. Life goes on.

Lushoto: Beautiful Weather…

leave a comment »


SAM_1506

Section of Lushoto town. PHOTO | TINA SIMBA (8yrs old)

Written by simbadeo

April 22, 2016 at 12:16 pm

Family Time: Happy birthday Tina Bahati Deo Simba

with 4 comments


20151228_133859

Tina Bahati Simba as she clocks 8 years. Congrats to you. May you be blessed abundantly.

20151228_135650

With big brother Martin Jubilee Deo Simba. Life is all about accompaniment.

20151225_224803

With big sister Cecilia Deo Simba. Big time. Guidance. Inspiration. Trust. Confidence. Being together.

Merry Christmas. Noeli Njema. 2015

with 7 comments


20151225_094711

This is to wish a Merry Christmas to all fans and readers of this blog and other social networks associated with it. May the day bring joy and plant the seeds of peace in our societies. Let there be peace always and the rest will follow.

Stay blessed.

Hii ni maalumu kuwatakia Furaha ya Noeli kwa wapenzi na wasomaji wote wa blogu hii pamoja na mitandao mingine ya kijamii inayohusiana nayo. Siku hii ilete furaha na kupanda mbegu za amani katika jamii zetu. Sote tujibidishe kuleta amani na mengine yote yatafuatia.

Ubarikiwe sana.

Reli ya Dar-Tanga-Moshi-Arusha ifufuliwe

leave a comment »


Reli Korogwe to Moshi Arusha

Moja ya mambo yanayoumiza mioyo ya Watanzania walio wengi ni kuona namna Reli ya Kati pamoja na matawi yake ilivyouwawa. Mfano ni reli inayotoka Dar es Salaam kwenda Tanga; na ile ya Tanga kwenda Moshi hadi Arusha. Licha ya kwamba usafirishaji kwa njia ya reli ni wa gharama nafuu, usafiri huo pia ni jia nzuri sana ya kukuza biashara ya utalii. Kwa hiyo, kuna tija kubwa kwa nchi yetu ikiwa tutadhamiria kikweli kufufua na kuendeleza miundombinu hii ya reli. Naamini serikali mpya italitupia jicho makini suala hili.

Ikumbukwe kuwa njia hizi zilijengwa na mababu zetu kwa jasho, damu na hata maisha yao. Haijalishi kwamba walishiriki katika ujenzi wake wakiwa chini ya utawala wa kikoloni, kikubwa ni kuwa tutawaenzi sana kwa kuifufua na kuiendeleza. Hiyo ni licha ya kutuletea manufaa ya kiuchumi na kijamii. Nasita kusema ya kisiasa maana siasa zetu zimetufikisha hapa tulipo sasa.

Pamoja sana.

Written by simbadeo

December 3, 2015 at 12:03 am

Magufuli: Tazama eneo hili pia

leave a comment »


Biashara ndogondogo Chalinze 1

Chalinze. Wachuuzi wengi ni wanaume.

Soni Akina mama wafanyabiashara

Soni, Lushoto. Wachuuzi wengi (kama sio wote) ni akina mama.

Mazao Biashara Ndogondogo 2

Mazao ya shamba. Masoko bora zaidi yanahitajika.

 

Ajira. Uchumi wa nchi hauwezi kukua endapo nguvukazi haitatumika vema kwa namna yenye kuleta tija kwao na kwa nchi. Wachuuzi walio hapo juu wanajitafutia riziki. Kile wanachopata hakiendani na nguvu wanayotumia. Tukiwa na utaratibu mzuri wa masoko — yaani kutafuta masoko ya uhakika — hawa watapata kipato kizuri zaidi. Hapo walipo ni vigumu kwao kulipa kodi (kama wanalipa basi ni ushuru kidogo unaokwenda halmashauri). Lakini wakiwa katika masoko maalumu, watapata kipato kizuri na kulipa kodi.

Mazingira wanayofanyia biashara pia si rafiki. Ni muhimu kubadili hali hii. Hivi sasa tunachokiona hapo juu kipo karibu kila kona, kila mji, kila njia kuu nchini Tanzania. Ni muhimu tubadili hii. Tunaweza tu kwa kufanya uchumi wetu ujiendeshe kwa nia zilizo rasmi. Kilimo kifanywe kwa tija na kwa njia zilizo rasmi, biashara ifanywe kwa njia rasmi. Serikali ifanye kazi kutafuta masoko ya uhakika kwa bidhaa zote zinazozalishwa nchini — za kilimo, mifugo, bahari, maziwa, mito na madini.

Ajira rasmi. Masoko ya uhakika. Kipato bora. Kulipa kodi. Kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara (ikiwemo miundombinu). Haya ndiyo baadhi ya mambo yatakayoleta mabadiliko chanya katika maisha ya Watanzania.

Pamoja sana.

Mshangao. Pale Chalinze wachuuzi ni wanaume (zaidi), kule Soni ni wanawake (zaidi). Sina majibu kwa hali hii. Je, Chalinze wanaotoka ni wanaume, wanawake wanabaki nyumbani? Je, kule Soni wanaotoka ni wanawake, wanaume wanabaki nyumbani? Kwa anayejua atujuze. Nafikiri kuna kitu cha kujifunza hapa.