simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Bendera ya Taifa Letu …

with one comment

dscf0047.jpg

Picha hii imepigwa jana saa 12.15 jioni pale ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Huenda mimi nimepitwa na wakati. Nilipokuwa kwenye mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria nilijifunza kuwa Bendera ya Taifa hushushwa kutoka kwenye mlingoti kila ifikapo saa 12 kamili jioni.

Inawezekana ni mimi ndiye niliyepitwa na wakati au inawezekana kabisa wale wenye jukumu la kushusha bendera hii pale ofisini kwa Mzee Kandoro walipitiwa wakati saa za mwishomwisho za 2007 zikiyoyoma.

Inawezekana pia ni ishara kuwa Watanzania huwa hatujali muda. Tunapanga wenyewe lakini ni sisi sisi ndiyo tunaovunja ahadi za muda tulizoweka. Wakati ni mali. Nidhamu katika kutunza muda ni muhimu kwa maendeleo ya aina yoyote ile.

 Nawatakia HERI na MAFANIKIO katika mwaka huu mpya wa 2008 ambao sasa hivi una umri wa nusu saa hivi.

Kila la kheri.

Advertisements

Written by simbadeo

January 1, 2008 at 12:35 am

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. Bwana Simba, nimepata nafasi ya kusoma baadhi ya makala zako. Kweli nakufagilia. Hasa nilipata kuona picha yetu tulipopanda mlima Kilimanjaro mwaka 1990. Kweli nimeliwazika kwani ile nakala yangu ilipotea nilipokumbwa na unyang’anyi Burundi.

  Yapo mengi ya kusifu kwani Watanzania wengi tumelala fofofo. Pengine ni kwa ajili ya shida za kiuchumi kwamba hatuna nafasi ya kujiandikia mambo yetu au ni kwa kutojali tu.

  Nimepata website yako kwa mara ya kwanza na hapa nakupongeza sana, tena nakuahidi kuwa bega kwa bega nawe endapo utakuwa na jambo la kuhitaji ushirikiano wangu.

  Wote tuliokuwa kwenye safari kupanda mlima bado tupo hai tena na kazi zetu. Wengi wao ni Wamisionari kamili na waliobaki ni Wazalendo hasa, tena majina yao yanavuma sana pale walipo. Karibu Bwana Deogratius Simba tuwasiliane zaidi.

  Like

  Reginald Mbuya

  March 19, 2010 at 10:52 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: