simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Dar es Salaam: Lori lavunja Daraja la Kinyerezi tena

with 2 comments

Ikiwa ni miezi michache tu tangu daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita kuvunjwa na lori lililosheheni matofali, leo hii tena, majira ya saa moja usiku lori lingine la kuchanganya kokoto limevunja daraja hilo.

Alama za barabarani huonyesha kuwa daraja hilo — ambalo ni la muda na lililotengenezwa kwa vyuma tupu — lina uwezo wa kubeba uzito usiozidi tani saba (7).

Kama ilivyokuwa safari ya kwanza, kuvunjika kwa daraja hili kunasababisha kero kubwa ya usafiri kwa wanaotumia barabara hii muhimu ikiwa ni pamoja na Jeshi la Magereza kutoka katika Gereza la Segerea. Tayari kulikuwa na msururu wa mamia ya magari kila upande wa daraja, huku yakipeana muda kuvuka katika Bonde la Mto Msimbazi kwa kutumia barabara ya dharura inayopita kwenye eneo la mto. Barabara hiyo ina uwezo wa kupitisha gari moja tu kwa wakati mmoja — yaani, magari mawili hayawezi kupishana.

 

Daraja Kinyerezi 1

Picha zaidi hizi hapa (ubora wa picha zi mzuri kwa sababu ya eneo hilo kutawaliwa na giza wakati wa usiku):

Daraja Kinyerezi 2

Lori lililoanguka usiku huu.

Daraja Kinyerezi 4

Utambulisho wa lori hilo.

 

Daraja Kinyerezi 5

Sehemu ya shehena ya zege ikiwa imemwagika kutoka kwenye lori hilo. Wakati picha hii inapigwa tayari zege hilo lilikuwa limeshaanza kukauka.

 

Daraja Kinyerezi 6

Utambulisho mwingine wa lori hilo.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao hawakuwa tayari kutajwa kwa sababu wao si wazungumzaji rasmi, dereva na utingo wake walinusurika na kutiwa mbaroni na walinzi wa daraja.

Kwa hakika, wakati ambapo haijulikani ni lini daraja hili la muda litatengenezwa tena, wananchi wa maeneo jirani na watumiaji wengine wa barabara hii wajiandae kwa kero kubwa ya usafiri. Miongoni mwa watakaotaabika ni pamoja na wanafunzi ambao hufuatwa majumbani na mabasi ya shule wanakosoma. Wakati huohuo, mwezi Machi huwa ni mwanzo wa msimu wa masika katika Jiji la Dar es Salaam. Mara mvua zitakapoanza kunyesha, hata barabara ya muda itapitika kwa taabu sana, na hivyo kufanya eneo hili kutokuwa na mawasiliano na upande wa pili.

 

 

Advertisements

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. poleni sana wakazi wa kinyerezi unajua kila mtu ana akili zake kiukweli inakela sana sisi madereva tunaonekana wote hatuna hata chembe ya hakili wakati tunazo hebu tujaribu kutulia maana hata foren tunasababisha wenyewe inakera sana

  Like

  adolf t byera

  March 9, 2015 at 8:03 am

  • Naam Ndugu Adolf. Umenena kweli. Kuna watu wanafanya fani ya udereva ionekani haina maana. Kwa makampuni makubwa, inafaa wafanye mchujo mkali pale wanapoajiri madereva wao. Mathalani dereva wa kampuni inayomiliki lori hili, ni kama vile alipata kazi kwa njia ya upendeleo. Malori yote hupita barabara ya chini, kilichomfanya apite juu ya daraja sijui ni nini.

   Like

   simbadeo

   March 9, 2015 at 10:44 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: