simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Hali tete Daraja la Kinyerezi na Majumba Sita

leave a comment »

Darajani 22 march 1

Darajani 22 march 4

Darajani 22 march 2

Darajani 22 march 7

Darajani 22 march 6

Kwa ufupi, hii ni kuhatarisha maisha ya wapiga kura katika nchi hii. Ni zaidi ya wiki mbili sasa tangu daraja la muda livunjike wakati lori la kuchanganya zege likipita juu yake. Hadi wakati huu, sijasikia tamko lolote kuhusu mpango uliopo wa kurekebisha hali ya mambo. Sijamsikia Mbunge wa Ukonga wala Madiwani wa Kata za Ukonga, Kipawa, Segerea wala Kinyerezi akizungumzia suala hili. Sijamsikia Waziri wa Ujenzi akisema lolote kuhusiana na tatizo lililopo.

Pengine wakuu hao wanasubiri mtu au watu wapoteze maisha na mali zao kisha ndio wajitokeze. Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo. Watu wanaojaribu kuvuka kwa kutumia vyuma vya daraja lililovunjika wanafanya hivyo kwa kuhatarisha maisha yao na mali zao. Eneo si salama. Mawasiliano kati ya pande mbili hakuna. Hakuna gari wala pikipiki inayoweza kuvuka hapo wakati huu. Na huu ni mwanzo tu wa mvua za masika.

Chondechonde, serikali ilitazame eneo hili kwa namna ya pekee. Naamini tuna wahandisi wengi wazalendo wenye uwezo wa kubuni suluhisho la muda wakati daraja la kudumu likiendelea kujengwa. Hakika katika hili hatutawaelewa ikiwa hamtakuja na majibu ya haraka.

Ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe. Kuna wazee, watoto, akina mama na wananchi wengine wengi wanaotumia barabara na daraja hili. Hivi sasa watoto wa upande mmoja wanaosoma shule upande mwingine, hawana tena fursa ya kwenda shule. Pale hapavukiki. Vivyo hivyo kwa watoto wa upande mwingine. Kwa watu wazima, watalazimika kupata adhabu ya kuzunguka njia ndefu ili kwenda kutafuta riziki za watoto wao na kodi mbalimbali wanazolipa serikalini. Maana yake, maisha yatakuwa ghali zaidi.

Kinachotakiwa hapa ni uamuzi mgumu. Mtuthibitishie kuwa mnaweza kufanya uamuzi mgumu na kuwarejeshea mawasiliano wapiga kura wenu.

Kwa pamoja, tunaweza.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: