Posts Tagged ‘segerea’
‘Daraja Hili … Thamani Yake ni Mvua ya Saa Tatu’
Ndivyo hali ilivyo katika daraja linalounganisha Kinyerezi na Segerea. Ni daraja muhimu kwani linategemewa na maelfu ya wakazi wa upande huo wa Dar es Salaam. Daraja la muda lilijengwa kwa muda wa miezi kadhaa. Malori ya mawe yalimwagwa hapo. Wajenzi wakatumia maarifa yao. Mamilioni ya fedha yaliingia hapo … sijui ni milioni ngapi. Kudumu kwa daraja hilo miezi michache tangu lijengwe kumekomeshwa na mvua iliyodumu kwa saa 3 tu! Hapa ndipo ninakumbuka kauli ya dereva wa daladala aliyetubeba ‘Thamani ya Daraja hili ni saa tatu ya mvua’!
Abiria wengine walijiuliza … ‘hasara hii ni ya nani’? Nani atabeba gharama za ujenzi mwingine wa daraja la muda? Miongoni mwa abiria hakuna aliyekuwa na majibu.
Hapa tunaona umuhimu wa kutumia maarifa yetu vema. Mwezi Desemba 2011 wakati wa mafuriko ya Dar, daraja lililokuwa hapo kwa miaka mingi lilisombwa. Hiyo ilitosha kabisa kutoa angalizo kwa wakandarasi walioshinda zabuni hiyo. Daraja la muda lilipaswa liwe madhubuti na kubwa kuliko lililokuwepo awali, na daraja la kudumu linalopaswa kuwa hapo linatakuwa kuwa kubwa sana, lililopanda juu sana na pana vizuri ili lisije kusombwa na mafuriko.
Tanzania ni yetu sote. Kila mmoja ajisikie uchungu na kuchukua hatua kukabili magumu yanayotusibu!
Weekend … Pumzisha Akili kwa Taswira Hizi
Weekend njema wadau wa blogu hii. Mbarikiwe sana. Natumaini nimepata ridhaa yako hapo kabla ili kukuletea makala hii. Maoni ni ruksa, tusivunje tu sheria za nchi! Pamoja sana!
Segerea Darajani … Uvukaji
Baada ya daraja lililokuwepo kusombwa na mafuriko miezi michache iliyopita … hivi ndivyo baadhi ya magari na watu wanavyovuka bonde hili. Ni katika Mto Msimbazi, sehemu inayounganisha Segerea (upande wa Seminari) na Sitakishari (Majumbasita).
Mahali lilipokuwa daraja kabla ya kusombwa. Chora mstari wa moja kwa moja na barabara iliyo ng’ambo ya mto (bonde la mto).
Bonde la mto baada ya kupanuliwa na mmomonyoko wa udongo …
Upande mwingine wa bode … nyumba zilizokuwa karibu kusombwa na maji.
Swali la kizushi
Mamlaka inayohusika na barabara hii … daraja hili litajengwa lini? Kimsingi, barabara hii inafupisha sana umbali kati ya Segerea na Sitakishari hadi Uwanja wa Ndege. Vilevile, endapo kuna tatizo lolote katika barabara ya Kinyerezi-Majumbasita, hii inaweza kutumika. Kumbe, ni barabara muhimu na yafaa kwamba daraja litengenezwe upya. Pamoja … sana.
Ajali … Segerea darajani … barabara nusu yafungwa
Kwanza nimekuta basi hili katika hali hii … na ni basi la shule … katika barabara inayounganisha Segerea na Kinyerezi Mbuyuni … mbele ni msululu wa magari uliokuwa ukienda kwa mwendo wa kinyonga …
Msululu wa magari yanayoelekea Kinyerezi …
Haya … hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kasheshe nzima usiku huu … ni katika daraja linalounganisha Segerea na Kinyerezi …
Hali ilikuwa hivi …
Kwa mujibu wa mashuhuda … au waliodai kuwa mashuhuda, lori hilo lenye shehena ya mchanga lilishindwa kupanda mlima. Baada ya hapo lilianza kurudi nyuma. Hiyo pick up ilikuwa ikija kwa nyuma. Basi kasheshe yake ndiyo kama unavyoona. Habari zaidi zilieleza kwamba waliokuwa kwenye pick up walijeruhiwa na mpaka mimi nafika eneo la tukio walikuwa wamekwenda police ili kupata PF3 kwa ajili ya kwenda hospitali kwa matibabu.
Haya … karibu na Daraja linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita, kwenye barabara ya kwenda Mongo la Ndege, nimekutana na hii tena.
Kwa maelezo niliyopata hapa. Mbele ya hiyo gari ndogo kulikuwa na gari lingine lililoshindwa kupanda mpando mdogo ulio mbele kidogo. Dereva wa pick up, pengine alikuwa na haraka sana, aliamua kuovertake gari hili dogo … matokeo yake ndiyo hiyo pasi …
Ndiyo niliyoshuhudia usiku wa leo wakati narejea kijijini kwetu … Ya barabarani ni mengi, mengine makubwa.