simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Posts Tagged ‘Dar Ferry

Weekend … Pumzisha Akili kwa Taswira Hizi

with 2 comments


Enero la Feri jijini Dar. Ni mahali unapoweza kutembea na kuburudika. Hata hivyo, kuna changamoto nyingi. Soko la samaki limechakaa ndani ya muda mfupi sana ... kama muongo mmoja tu. Swali la kujiuliza ... kutujengea watujengee ... hata kutunza nako waje kututunzia? Sisi kazi yenu ni nini? Kukusanya ushuru tu??? Tubadilike!

Enero la Feri jijini Dar. Ni mahali unapoweza kutembea na kuburudika. Hata hivyo, kuna changamoto nyingi. Soko la samaki limechakaa ndani ya muda mfupi sana … kama muongo mmoja tu. Swali la kujiuliza … kutujengea watujengee … hata kutunza nako waje kututunzia? Sisi kazi yenu ni nini? Kukusanya ushuru tu??? Tubadilike!

Mvua inapoamua kunyesha ... Hapana budi kusubiri ... Ndivyo ilivyokuwa ... Dakika 45!

Mvua inapoamua kunyesha … Hapana budi kusubiri … Ndivyo ilivyokuwa … Dakika 45!

Haya ... ulimi unaniponyoka ... Mara nyingi huwa tunalazimishwa kutenda vitu vingi pasipo kuhiyari. Mathalani, upo kituo cha basi, unasubiri usafiri ambao nao unakuwa umeota mbawa ... huna hili wala lile ... mara anakuja jamaa na spika yenye sauti kali ... anakatisha fikra ulizo nazo kwa kuanza kukumiminia neno. Papo hapo hakukutaka radhi, hakuomba ruhusa yako kama unaridhia kusikiliza au la. Kuondoka hapo huwezi, maana ndipo mahali pa wewe kupata usafiri. Unajikuta unameza dozi bila kupenda ... sorry ... Vitendo kama hivi ... haviwezi kuwekwa kundi moja na 'ubakaji'? Vipo vingine vingi. Huu ni mfano mmoja tu! Kuuliza si ujinga ... wahenga walisema!

Haya … ulimi unaniponyoka … Mara nyingi huwa tunalazimishwa kutenda vitu vingi pasipo kuhiyari. Mathalani, upo kituo cha basi, unasubiri usafiri ambao nao unakuwa umeota mbawa … huna hili wala lile … mara anakuja jamaa na spika yenye sauti kali … anakatisha fikra ulizo nazo kwa kuanza kukumiminia neno. Papo hapo hakukutaka radhi, hakuomba ruhusa yako kama unaridhia kusikiliza au la. Kuondoka hapo huwezi, maana ndipo mahali pa wewe kupata usafiri. Unajikuta unameza dozi bila kupenda … sorry … Vitendo kama hivi … haviwezi kuwekwa kundi moja na ‘ubakaji’? Vipo vingine vingi. Huu ni mfano mmoja tu! Kuuliza si ujinga … wahenga walisema!

Weekend njema wadau wa blogu hii. Mbarikiwe sana. Natumaini nimepata ridhaa yako hapo kabla ili kukuletea makala hii. Maoni ni ruksa, tusivunje tu sheria za nchi! Pamoja sana!

Written by simbadeo

January 18, 2013 at 11:23 pm

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , , ,