simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

‘Daraja Hili … Thamani Yake ni Mvua ya Saa Tatu’

leave a comment »

Siku chache zilizopita, wengine wetu tulipolalamikia uzio huo!

Siku chache zilizopita, wengine wetu tulipolalamikia uzio huo!

Daraja na uzio na vifaa vingine vya ujenzi wa daraja jipya ... vimesombwa na maji ...

Daraja na uzio na vifaa vingine vya ujenzi wa daraja jipya … vimesombwa na maji …

Mitambo ya ujenzi ... karibu ufukiwe na udongo ...

Mitambo ya ujenzi … karibu ufukiwe na udongo …

Hivi ndivyo uvukaji ulivyokuwa ... Ni eneo lenye udongo unaoteleza. Usipokuwa makini, unavunja mguu au mkono kama si kupasua kichwa!

Hivi ndivyo uvukaji ulivyokuwa … Ni eneo lenye udongo unaoteleza. Usipokuwa makini, unavunja mguu au mkono kama si kupasua kichwa!

Hali ya usafiri ilikuwa hivi. Daladala za kutoka Kinyerezi na Majumbasita ziliishia hapa. Zile za kutoka Tabata na Segerea, nazo ziliishia upande wa pili. Hiyo haikutoa unafuu wa nauli ... au utembee hadi Segerea Mwisho, au upande gari na ulipe nauli nyingine. Kufa kufaana.

Hali ya usafiri ilikuwa hivi. Daladala za kutoka Kinyerezi na Majumbasita ziliishia hapa. Zile za kutoka Tabata na Segerea, nazo ziliishia upande wa pili. Hiyo haikutoa unafuu wa nauli … au utembee hadi Segerea Mwisho, au upande gari na ulipe nauli nyingine. Kufa kufaana.

Ndivyo hali ilivyo katika daraja linalounganisha Kinyerezi na Segerea. Ni daraja muhimu kwani linategemewa na maelfu ya wakazi wa upande huo wa Dar es Salaam. Daraja la muda lilijengwa kwa muda wa miezi kadhaa. Malori ya mawe yalimwagwa hapo. Wajenzi wakatumia maarifa yao. Mamilioni ya fedha yaliingia hapo … sijui ni milioni ngapi. Kudumu kwa daraja hilo miezi michache tangu lijengwe kumekomeshwa na mvua iliyodumu kwa saa 3 tu! Hapa ndipo ninakumbuka kauli ya dereva wa daladala aliyetubeba ‘Thamani ya Daraja hili ni saa tatu ya mvua’!

Abiria wengine walijiuliza … ‘hasara hii ni ya nani’? Nani atabeba gharama za ujenzi mwingine wa daraja la muda? Miongoni mwa abiria hakuna aliyekuwa na majibu.

Hapa tunaona umuhimu wa kutumia maarifa yetu vema. Mwezi Desemba 2011 wakati wa mafuriko ya Dar, daraja lililokuwa hapo kwa miaka mingi lilisombwa. Hiyo ilitosha kabisa kutoa angalizo kwa wakandarasi walioshinda zabuni hiyo. Daraja la muda lilipaswa liwe madhubuti na kubwa kuliko lililokuwepo awali, na daraja la kudumu linalopaswa kuwa hapo linatakuwa kuwa kubwa sana, lililopanda juu sana na pana vizuri ili lisije kusombwa na mafuriko.

Tanzania ni yetu sote. Kila mmoja ajisikie uchungu na kuchukua hatua kukabili magumu yanayotusibu!

Advertisements

Written by simbadeo

March 25, 2013 at 11:29 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: