simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

… baada ya Uchaguzi Mkuu 2015 … maisha yaendelee

with 2 comments

Bwama, Kisarawe, Tanzania

Bwama, Kisarawe, Tanzania

Uchaguzi Mkuu umepita. Suluhu kwa mgogoro wa Zanzibar inaendelea kutafutwa. Ni wakati wa kujenga Taifa. Kila mmoja pale alipo ajenge Taifa. Changamoto nyingi zilizojitokeza wakati wa uchaguzi zifanyiwe kazi. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iundwe upya kwa kushirikisha wadau wote. Uwazi na uwajibikaji vipewe kipaumbele. Vyombo vya ulinzi na usalama vibaki kuwa mali ya umma — na si vya chama au mhimili fulani katika dola. Ubaguzi wa aina yoyote — ukabila, dini, rangi, asili, kipato, hadhi, ukanda — ni muhimu ufutwe, tena haraka. Vinginevyo, tutakuwa tunakata tawi la mti tulilolikalia. Huenda tusione madhara ya ubaguzi mapema, lakini wakati utafika ambapo hakuna atakayekuwa salama. Tanzania mpya inawezekana. Tanzania ya haki na amani ya kweli inawezekana. Sote tuna wajibu. Pamoja sana.

Advertisements

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. naaam, na jinsi tulivyomkimbilia Mungu kipindi hiki tuendelee ili haki na hukumu za Mungu zisimamie nchi.
  Mungu ibariki Tanzania

  Like

  Jennifer

  November 4, 2015 at 6:45 am

  • Hahaha! Jennifer. Mwenyezi Mungu tunamtaja sana. Lakini maombi yetu hayana budi kuoana na matendo yetu. Ikiwa mdomoni tunasifu na kuomba huku kwa vitendo vyetu tunalaani na kuendeleza dhuluma, basi sala zetu ni bure. Kila mmoja pale alipo atende haki na Inshallah … tutaona Mwenyezi Mungu naye akitunyooshea mambo yetu. Pamoja sana.

   Like

   simbadeo

   November 4, 2015 at 5:37 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: