simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Posts Tagged ‘TAZARA

Tazara: Treni Daladala

leave a comment »


Tazara Daladala peak hour 1

Watu wakiwa katika Kituo Kikuu cha Garimoshi cha Tazara. Hawa wanasubiri kuruhusiwa kuingia katika garimoshi linalofanya safari kati ya Stesheni hiyo na viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam.

Tazara Daladala peak hour

Abiria baada ya kuruhusiwa kuingia katika mabehewa. Garimoshi moja katika safari hizi huwa na mabehewa yasiyopungua tisa (9). Katika nyakati ambako kuna abiria wengi, yaani asubuhi (kuelekea mjini) na jioni (kuelekea Mwakanga na vituo vya mbele). Nilichokiona katika safari niliyofanya ni udhaifu wa udhibiti wa mapato. Ukusanyaji nauli unafanyika kiholela. Ni rahisi mtu kulipa kiwango tofauti na kilichopangwa ili mradi hapewi risiti. Hii ina maana kuwa fedha hiyo itaingia kwenye mfuko wa aliyepewa dhamana ya kukusanya nauli. Kwa maana hiyo, shirika lisitegemee kuona mwujiza katika mapato yake katika kutoa huduma hii.

Nasi Watanzania tubadilike. Ili huduma kama hii udumu ni muhimu tutimize wajibu wetu. Mosi, tulipe nauli sahihi. Pili, tudai risiti halali katika kutumia huduma hiyo. Vinginevyo, huduma itakuwa mzigo kwa mamlaka na hatimaye kusitishwa. Jambo hilo likitokea, watakaoumia ni sisi.

Pamoja sana.

Msongamano wa Magari … Taffic Jams

leave a comment »


Mahali pa njia tatu … zimeibuka njia tano au sijui sita … duh! Hii ni changamoto kubwa kwa maendeleo. Kwa mtindo huu watu wataendelea kuweka maisha yao rehani kwa kutumia pikipiki ili wasishikwe na foleni. Miundombinu inapaswa kushughulikiwa kwa namna ya pekee kabisa na kwa kutazama miaka 40 hadi 50 ijayo.

Naamini kama tutaweka kiwango cha ‘kufurahi’, basi ‘furaha’ ya wakazi wengi hunyong’onyezwa na mgogoro huu wa msongamano wa magari. Stress hapa lazima ziwe nyingi maana kila mmoja ana haraka zake, lakini anakwazwa na hali kama hii. Ili kuwapa watu furaha na amani kwenye nafsi yao … miundombinu nayo ina nafasi yake. Pamoja sana!

Written by simbadeo

September 26, 2012 at 9:46 am