simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Posts Tagged ‘daladala

Tazara: Treni Daladala

leave a comment »


Tazara Daladala peak hour 1

Watu wakiwa katika Kituo Kikuu cha Garimoshi cha Tazara. Hawa wanasubiri kuruhusiwa kuingia katika garimoshi linalofanya safari kati ya Stesheni hiyo na viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam.

Tazara Daladala peak hour

Abiria baada ya kuruhusiwa kuingia katika mabehewa. Garimoshi moja katika safari hizi huwa na mabehewa yasiyopungua tisa (9). Katika nyakati ambako kuna abiria wengi, yaani asubuhi (kuelekea mjini) na jioni (kuelekea Mwakanga na vituo vya mbele). Nilichokiona katika safari niliyofanya ni udhaifu wa udhibiti wa mapato. Ukusanyaji nauli unafanyika kiholela. Ni rahisi mtu kulipa kiwango tofauti na kilichopangwa ili mradi hapewi risiti. Hii ina maana kuwa fedha hiyo itaingia kwenye mfuko wa aliyepewa dhamana ya kukusanya nauli. Kwa maana hiyo, shirika lisitegemee kuona mwujiza katika mapato yake katika kutoa huduma hii.

Nasi Watanzania tubadilike. Ili huduma kama hii udumu ni muhimu tutimize wajibu wetu. Mosi, tulipe nauli sahihi. Pili, tudai risiti halali katika kutumia huduma hiyo. Vinginevyo, huduma itakuwa mzigo kwa mamlaka na hatimaye kusitishwa. Jambo hilo likitokea, watakaoumia ni sisi.

Pamoja sana.

Advertisements

Treni Daladala … Umelipanda?

leave a comment »


Ndani ... Jioni unapotoka upande wa Ubungo, halina msongamano ... ni kujimwaga tu!

Ndani … Jioni unapotoka upande wa Ubungo, halina msongamano … ni kujimwaga tu!

Linapokatisha mitaa ... Sasa hivi nadhani wanafunzi wakifundishwa kuhusu treni/gari moshi, walau wanaelewa, maana wanaliona. Ni tofauti na hapo kati ambapo kuonekana kwake kulikuwa kumeanza kuwa nadra ...

Linapokatisha mitaa … Sasa hivi nadhani wanafunzi wakifundishwa kuhusu treni/gari moshi, walau wanaelewa, maana wanaliona. Ni tofauti na hapo kati ambapo kuonekana kwake kulikuwa kumeanza kuwa nadra …

Kwa ujumla, lina burudani ya aina yake kusafiri nalo. Kama unataka kutalii kidogo kwa treni, chagua wakati ule linapokuwa halina watu wengi. Kama ni peak hour kutoka mjini, basi wewe panda kinyume chake. Utalifurahia sana.

Na hili ni moja ya mabasi maarufu kama 'daladala' yanayofanya kazi ya kubeba abiria katika vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam na viunga vyake. Usafiri huu nao ni historia ya aina yake. Una mguso katika maisha ya watu na kuna mengi ya kujifunza humo pia.

Na hili ni moja ya mabasi maarufu kama ‘daladala’ yanayofanya kazi ya kubeba abiria katika vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam na viunga vyake. Usafiri huu nao ni historia ya aina yake. Una mguso katika maisha ya watu na kuna mengi ya kujifunza humo pia.

Written by simbadeo

January 30, 2013 at 11:52 pm

Kwa hakika … Treni Daladala Halina Budi Kufika Huku Nako

leave a comment »


Maana kwa mtindo huu … watu wanajiweka kwenye hatari nyingi: vibaka kuchomoa fedha, simu, mikufu ya dhahabu na vinginevyo vya thamani. Wakati huo huo magonjwa yanayoambukiza kwa njia ya hewa na yale yanayotokana na kugusana ngozi nayo yanakuwa kwenye uwezekano mkubwa wa kuenezwa. Ukiachilia mbali hayo … fikiria mtu akianguka hapo … si jozi kadhaa za miguu zitamkanyaga kabla watu hawajakumbuka kwamba kuna mwenzao kadondoka hapo!

Ndiyo sababu nafikiri fedha inayopatikana kwenye Treni Daladala la Mwakyembe, litumike kusogeza njia ya reli katika pande mbalimbali za jiji la Dar na vitongoji vyake ili kupunguza adha hizi, au siyo wajemeni? Ninaamini kwamba tutakuwa pia tukipewa taarifa za mapato na matumizi ya chombo hiki cha umma … maana sote tu wadau na tuna kila haki ya kuhabarishwa!

Pamoja sana.

Written by simbadeo

November 21, 2012 at 12:27 am