simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Posts Tagged ‘huduma

Tazara: Treni Daladala

leave a comment »


Tazara Daladala peak hour 1

Watu wakiwa katika Kituo Kikuu cha Garimoshi cha Tazara. Hawa wanasubiri kuruhusiwa kuingia katika garimoshi linalofanya safari kati ya Stesheni hiyo na viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam.

Tazara Daladala peak hour

Abiria baada ya kuruhusiwa kuingia katika mabehewa. Garimoshi moja katika safari hizi huwa na mabehewa yasiyopungua tisa (9). Katika nyakati ambako kuna abiria wengi, yaani asubuhi (kuelekea mjini) na jioni (kuelekea Mwakanga na vituo vya mbele). Nilichokiona katika safari niliyofanya ni udhaifu wa udhibiti wa mapato. Ukusanyaji nauli unafanyika kiholela. Ni rahisi mtu kulipa kiwango tofauti na kilichopangwa ili mradi hapewi risiti. Hii ina maana kuwa fedha hiyo itaingia kwenye mfuko wa aliyepewa dhamana ya kukusanya nauli. Kwa maana hiyo, shirika lisitegemee kuona mwujiza katika mapato yake katika kutoa huduma hii.

Nasi Watanzania tubadilike. Ili huduma kama hii udumu ni muhimu tutimize wajibu wetu. Mosi, tulipe nauli sahihi. Pili, tudai risiti halali katika kutumia huduma hiyo. Vinginevyo, huduma itakuwa mzigo kwa mamlaka na hatimaye kusitishwa. Jambo hilo likitokea, watakaoumia ni sisi.

Pamoja sana.

Advertisements

Mwisho wa Dunia … Ondoa Shaka!

leave a comment »


Sehemu ya kalenda ya Ki-Mayan inayobashiri kwamba tarehe 21 Desemba ndiyo mwisho wa dunia. Je, utabiri huo utatimia? Fuatilia kuanzia Mashariki ya Mbali ambako tayari wamekwishaanza siku mpya ... Kuna habari za pekee kule? Fuatilia ...

Sehemu ya kalenda ya Ki-Mayan inayobashiri kwamba tarehe 21 Desemba ndiyo mwisho wa dunia. Je, utabiri huo utatimia? Fuatilia kuanzia Mashariki ya Mbali ambako tayari wamekwishaanza siku mpya … Kuna habari za pekee kule? Fuatilia …

Mayan apocalypse: End of the world, or a new beginning?

By Jane Little

BBC News, Washington

One in 10 of us is said to be anxious that 21 December marks the end of the world. The Ancient Mayans predicted this doomsday, and the press is eating it up. But where are all the believers?

That the world will end in 2012 is the most widely-disseminated doomsday tale in human history, thanks to the internet, Hollywood and an ever-eager press corps.

Recent hurricanes, unrest in the Middle East, solar flares, mystery planets about to collide with us – all “proof” of what the ancient Mayans knew would come to pass on 21 December 2012.

According to a Reuters global poll, one in 10 of us is feeling some anxiety about this date.

Russians have been so worried that the Minister of Emergency Situations issued a denial that the world would end.

Authorities in the village of Bugarach in the South of France have barred access to a mountain where some believe a UFO will rescue them.

And survivalists in America – many of whom use the term “prepper” – have been busy preparing for all manner of cataclysm.

SOURCE: http://www.bbc.co.uk/news/magazine-20764906

KWA UFUPI: SIKU HII ITAPITA KAMA ZINAVYOPITA SIKU NYINGINE. HAKUTAKUWA NA MWISHO WA DUNIA WALA NINI. WATU WAENDELEE NA SHUGHULI ZAO KAMA KAWAIDA. TUONDOE HOFU NA TUPUUZE HABARI KAMA HIZI. TUSIACHE KUCHAPA KAZI NA KUTOA HUDUMA KWA WENZETU.

Written by simbadeo

December 20, 2012 at 10:58 pm

South Dar Mbagala … Kazi ya Mikono ya Watu

leave a comment »


Workshop … Kazi zinaendelea. Gurudumu la maendeleo linasukumwa kwenda mbele.

Matunda. Yanasubiri kuvunwa.

Ndiyo. Mbagala inabadilika. Unaweza kuishi huko miezi sita bila kuwa na sababu ya kwenda mjini. Huduma zote unapata huko huko.

Na miundombinu inaimarishwa … hata kama ni kwa kusahihisha upungufu uliokuwepo mwanzo.

Benki zinashindana kutafuta wateja na kuwasogezea wateja huduma.

Vituo vya mafuta navyo vinashindana …

Ukiona namna hii … ujue shughuli huko mbele ni pevu.

Huduma za hospitali nazo hazikubaki nyuma. Usiniulize kama kuna madaktari na dawa na vifaa vingine … hilo sikulitafiti safari hii. Lakini wenyeji watatueleza na wenye dhamana na mamlaka nao wataibuka kutueleza.

Kwa ujumla, Mbagala inabadilika. Miongo miwili iliyopita, watu wengi wasingetamani kuishi Mbagala. Huduma zilikuwa duni sana na changamoto zilikuwa nyingi. Bado changamoto ni nyingi hata sasa, lakini kuna huduma nyingi, hasa za kibiashara zilizojisegeza karibu. Je, maisha ya watu yanakuwa bora zaidi … pengine hilo ni swali linalohitaji utafiti wa kina ikiwa ni pamoja na kufanyia kazi takwimu nyingi sana. Kwa sasa uwanja huu hauna uwezo huo, ila pengine siku za usoni. Pamoja sana.

Written by simbadeo

October 1, 2012 at 11:58 pm