Posts Tagged ‘risiti’
Tazara: Treni Daladala
Watu wakiwa katika Kituo Kikuu cha Garimoshi cha Tazara. Hawa wanasubiri kuruhusiwa kuingia katika garimoshi linalofanya safari kati ya Stesheni hiyo na viunga mbalimbali vya jiji la Dar es Salaam.
Abiria baada ya kuruhusiwa kuingia katika mabehewa. Garimoshi moja katika safari hizi huwa na mabehewa yasiyopungua tisa (9). Katika nyakati ambako kuna abiria wengi, yaani asubuhi (kuelekea mjini) na jioni (kuelekea Mwakanga na vituo vya mbele). Nilichokiona katika safari niliyofanya ni udhaifu wa udhibiti wa mapato. Ukusanyaji nauli unafanyika kiholela. Ni rahisi mtu kulipa kiwango tofauti na kilichopangwa ili mradi hapewi risiti. Hii ina maana kuwa fedha hiyo itaingia kwenye mfuko wa aliyepewa dhamana ya kukusanya nauli. Kwa maana hiyo, shirika lisitegemee kuona mwujiza katika mapato yake katika kutoa huduma hii.
Nasi Watanzania tubadilike. Ili huduma kama hii udumu ni muhimu tutimize wajibu wetu. Mosi, tulipe nauli sahihi. Pili, tudai risiti halali katika kutumia huduma hiyo. Vinginevyo, huduma itakuwa mzigo kwa mamlaka na hatimaye kusitishwa. Jambo hilo likitokea, watakaoumia ni sisi.
Pamoja sana.
Written by simbadeo
April 24, 2016 at 10:59 pm
Posted in Business, Conflict, Culture, Economy, Education, Entertainment, Family and social life, Investment, Media, Nature and the Environment, People, Places
Tagged with daladala, huduma, Mwakanga, nauli, risiti, TAZARA