simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for June 2013

Rais Barack Obama … Karibu Tanzania

with 2 comments


Rais Obama na mkewe Michelle walipokuwa Afrika ya Kusini majuzi.

Rais Obama na mkewe Michelle walipokuwa Afrika ya Kusini majuzi.

Rais Obama na familia yake pamoja na walinzi wao.

Rais Obama na familia yake pamoja na walinzi wao.

Dar es Salaam ... evening before Obama visit.

Dar es Salaam … evening before Obama visit.

Obama in Tanzania June 2013 four

Dar es Salaam ... evening before Obama visit.

Dar es Salaam … evening before Obama visit.

Rais Barack Obama, karibu sana Tanzania, nchi ya amani na utulivu. Kama ilivyo ada yetu Watanzania, tunafurahi kukupokea na kukukirimu kwa ukunjufu wa mioyo yetu. Tunaelewa pia kwamba umeacha mambo mengi muhimu nchini kwako na kutenga muda ili kututembelea. Tunalithamani sana jambo hilo.

Tunaelewa pia kwamba unalenga kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya Taifa lako la Marekani na letu Tanzania. Kwa hakika, jambo hili ni jema na muhimu kwa ustawi wa watu wa pande zote mbili na ulimwengu kwa ujumla.

Hata hivyo, Taifa lako liko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kunufaika na kuimarishwa huku kwa uhusiano wa kibiashara kwani tayari watu wako wana nguvu kubwa ya kiuchumi na uzoefu mpana katika kuhimili biashara kubwa za kimataifa. Zaidi ya hayo, watu wako wana teknolojia ya kisasa kabisa kuweza kutumia rasilimali na kuibadili kuwa utajiri.

Pengine hapo ndipo palipo na mtihani kwetu. Watu wetu wanakosa mtaji, uzoefu na teknolojia sahihi. Tulicho nacho ni rasilimali na watu.

Unapohimiza kukuzwa kwa uhusiano baina ya pande mbili hizi, ni vema ukumbuke kuwahimiza watu wako (wafanyabiashara) kuchukua aina ya ubepari ule unaojali pia haki na maendeleo ya wenyeji. (Tunaelewa kwamba, kama ilivyo kwa siasa mbalimbali, ubepari nao umegawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna aina ile inayotazama kukuza tu faida ya wenye mtaji na haujali kama unaumiza wengine na hata kiasi cha kuwageuza kuwa watumwa nchini mwao. Mifano ya aina hii ya ubepari ipo mingi. Hata hapa kwetu tumeanza kuona makali yake.)

Kumbe basi, uhusiano huu uwe kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili, sisi tupate kukua (kwa haki na usawa) kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiroho nanyi mtengeneze faida kwa mitaji mtakayoweka.

Historia haifutiki na haifichiki. Tungependa tunapoingia katika ngazi hii ya uhusiano, tuingie tukiwa watu wenye utambuzi kamili na hiari ya kushiriki kikamilifu kwa manufaa yetu, ya vizazi vyetu vijavyo na vivyo hivyo kwa upande wa watu wako. Tafadhali, tuweke kando aina ile ya uhusiano ambao mababu zetu waliwahi kuwa na wageni. Katika uhusiano huo wa kale, wazazi wetu waliporwa mali, ardhi na hata watu wao kwa kupewa shanga, vioo na pombe kali. Hatutaki historia ituhukumu kwa kugawa rasilimali pasipo nasi kama Taifa kupata manufaa yanayostahili kwa haki na usawa.

Kuna hili la uchimbaji madini ya urani (Uranium). Pamoja na teknolojia ambayo Taifa lako linayo, bado madini haya kuyachokoza huko kwenye makazi yake (ardhini) pasipokuwa na umakini wa hali ya juu inaweza kugeuka janga kwetu na mazingira yetu. Tafadhali lipime sana hili. Kama hakuna ULAZIMA wa kuyachokoza huko yaliko hivi sasa, hebu tusubiri hata miaka mingine 100. Madini ya urani yanaweza kugeuka angamizo kuu la Sayari ya Dunia katika muda mfupi. Wakati huu ambapo baadhi ya mataifa yenye nguvu za kinyuklia yameamua kusitisha kuiendeleza (hata kama ni kwa matumizi salama), ni vema tukaacha kufikiri kuchimba urani hivi sasa (hata kama ina matumizi mengine). Yawezekana kabisa kwamba bado dunia nzima (Taifa lako likiwemo) halijapata teknolojia sahihi ya kutumia madini hayo kwa njia zilizo sahihi pasipo kuleta madhara kwa viumbe hai, mazingira na sayari yetu kwa ujumla wake.

Kuna uwekezaji katika mashamba makubwa. Hili linaweza kuwa jambo jema kwani kwa njia hiyo chakula kingi zaidi kitazalishwa na hivyo kuleta usalama zaidi wa chakula kwa ulimwengu. Lakini biashara hii isisababishe watu kuporwa ardhi zao na kuhamishwa (kwa nguvu au bila nguvu) kutoka maeneo yao ya asili wanakojipatia maisha, labda kama kwa kufanya hivyo, watu hawa watanufaika zaidi kupewa mbadala ambao utawafanya wapande ngazi kuelekea maisha bora zaidi kuliko yale wanayoishi sasa.

Hilo la kilimo huendana, mara nyingine, na uanzishwaji wa mazao ya kibaiolojia, wataalamu wanaita GMOs. Chonde chonde, dunia bado haijawa na teknolojia ya kuaminika kwa asilimia kubwa kuhusu mazao ya aina hii. Hebu tuendeleze mbegu bora lakini zile za asili.

Tanzania imekuwa nchi ya amani kwa miaka mingi. Tungependa hali hii idumu daima. Tusaidie katika kuimarisha demokrasia yetu ili tuelewe kwamba kutofautiana katika itikadi za kisiasa SIYO lazima kutugeuze kuwa maadui au mahasimu. Tufanye siasa zetu kwa njia ya ukomavu zaidi, njia yenye kuzingatia haki na usawa. Vyombo vya dola vitambue nafasi yake katika nchi, kwamba vyenyewe na watu wao havipaswi kuegemea huku wala kule. CCM, Chadema, TLP, CUF, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vinaweza kutoweka hata leo, lakini Tanzania itabaki daima.

Kutokana na ujio wako, kuna ambao wameumia. Biashara zao ndogondogo za kujikimu zimebomolewa na wao kuhamishwa kutoka kwenye maeneo ya biashara. Si ajabu kwamba huenda kuna kaya kadhaa ambazo zimekosa mlo wao kwa sababu hawana mahali pa kujipatia riziki. Pengine uhimize kwamba baada ya safari yako, watu hawa wafidiwe kwa haki na kupatiwa maeneo mapya ya kufanya kazi zao, ili mradi wazingatie sheria na kanuni za kuendesha biashara za nchi hii.

Mwisho, jiji limesafishwa (kwa kiasi fulani), lakini hili si la kwako, hili ni la Mababa wa Jiji letu. Chonde chonde, zingatieni uwazi na uwajibikaji, tungependa kusikia fedha zinazotokana na kodi zetu kujua zilitumikaje na kama kuna uwiano kati ya matumizi na kile tunachokiona.

Vinginevyo, karibu sana Rais Barack Obama pamoja na familia yako. Karibu katika nchi ya amani, utulivu na ukarimu. Kwa pamoja tumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kutuwekea misingi mizuri ya maelewano na umoja wa kitaifa. Karibu sana.

Obama … Wakomunisti Wamshambulia Afrika ya Kusini

with one comment


Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mmoja wa binti zake.

Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mmoja wa binti zake.

Safari ya Obama Afrika ni ya Upande Mmoja: Wakomunisti

Pretoria – Wale waliotaraji kwamba kipindi cha utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama kingekuwa tofauti, wanajihisi kuangushwa, katibu mkuu wa chama cha Young Communist League (YCL) Buti Manamela alisema siku ya Ijumaa.

Safari ya Obama katika mataifa matatu, iliyoanzia Senegali, Afrika ya Kusini na inayotarajiwa kumalizika Tanzania, ni ya upande mmoja, nao ni kwa maslahi ya Marekani, alisema Manamela.

“Kusema ukweli, Obama yupo hapa kwa ajali ya kujenga uhusiano wa kibishara, si kwa manufaa ya bara hili, lakini kwa manufaa ya ubepari mkongwe wa Marekani. Manufaa kwa makampuni ya Amerika kuendelea kuvuna ralimali zetu za madini.”

Manamela na maofisa wengine waliwaongoza wanaharakati elfu moja katika maandamano kuelekea katika Ubalozi wa Marekani huko Arcadia, Pretoria.

“Tupo hapa ili kuonyesha hasira yetu na kukasirishwa kwetu na uhusiano unaoendeleza mabavu ya Marekani, sio tu katika uchumi, bali hata katika nyanja za siasa vilevile,” alisema.

“Tulitaraji kwamba kwa kuchaguliwa kwake, mambo hayo yangepungua.”

Dunia litaraji kwamba angeondoa majeshi kutoka Afghanistan, angewaruhusu Waafrika kutafuta suluhu zao kwa matatizo yao wenyewe, angefungilia mbali mahabusu yenye ulinzi mkali ya Guantanamo Bay.

Manamela alisema matarajio hayo yabebaki kuwa ndoto tu.

Obama aliamua kutembelea Afrika kwa sababu Marekani ilihisi kutishwa na kuzidi kujipenyeza kwa China katika soko kubwa la Afrika, alisema Manamela.

“Wao [Wamarekani] wanaona kwamba China tayari iko hapa. Ni kwa sababu ya kitisho hicho cha Uchina kwamba Marekani nayo imekuja hapa. Jambo hili zima [safari] limepata msukumo kutokana na ukweli kwamba uchumi wa Afrika unakua,” alisema.

“Ni udanganyifu kwa Wamarekani kuifanya safari hii ionekane kana kwamba ni kwa manufaa ya bara hili wakati ambapo kwa kweli ni sehemu ya vita yao dhidi ya China.”

Baada ya waandamanaji hao kufika hadi kwenye ubalozi huo, kikundi cha wanaharakati Waislamu kilifanya ibada. Kikundi hicho (kilichokuwa na watu wachache) kilisogea hadi mbele ya ofisi za ubalozi, ambapo mablanketi na vipande vya kapeti vilitandikwa karibu na eneo lenye mfumo wa kutolea hotuba. Mtu mmoja alizungumza na waumini hao waliokuwa wakisujudu.

“Tukimzungumzia Obama, yeye si alama ya demokrasia. Tumeona kuongezeka kwa mauaji ya watu. Hebu tazama Afghanistan, Irak na nchi nyingine,” alisema.

Waandamanaji

Waandamanaji wengine, wakivalia mavazi ya YCL, walishuhudia kikundi hicho wa Waislamu wakisujudu na kushiriki ibada.

Kulikuwa na maofisa kadhaa waliosimama karibu na lango la kuingilia ofisi za ubalozi. Kulikuwa na zaidi ya magari ya polisi 20, likiwemo Nyala, nje ya ubalozi.

Waandamanaji walichoma moto bendera ya Marekani karibu na lango hilo.

Baadhi ya mabango waliyokuwa wamebeba waandamanaji yalisomeka: “Obama, acha kuunga mkono madikteta barani Afrika. Hakuna mafuta hapa, nenda zako”; “Miaka 100 ya mauaji ya kimbari huko Irak. Vita katika mataifa 100. Dola la Kihuni.”

Bango la mwandamanaji mmoja mvulana lilisomeka: “Hapan, huwezi kunipeleleza”. Bango lingine lilisomeka: “USA = Under Satanic Administration, yaani ‘Marekani = Chini ya Utawala wa Kishetani”.

Bango kubwa lilibeba picha ya uso wa Obama na maneno: “Huyu ndiye mwuwaji nambari moja duniani”.

Bango hilo lilimwonyesha Obama akiwa katika chumba cha gereza.

Waandishi wengi wa habari wa nchini Afrika ya Kusini na wa Kimataifa, ambao walikuwa wamepiga kambi nje ya Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic, ambamo Rais wa zamani Nelson Mandela anatibiwa, walikimbia kwenda kuchukua habari za maandamano.

Wakati watu walipopita karibu na hospitali hiyo, walipaaza sauti ili kufikisha salamu zao za upendo na kumtakia faraja mwanaharakati huyo aliye ishara madhubuti ya kupinga siasa za ubaguzi wa rangi.

Chanzo: http://www.news24.com/SouthAfrica/News/Obamas-African-trip-one-sided-YCL-20130628

Ndio.

Katika kipindi hiki ambapo Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla tumeshikwa na ‘homa ya Obama’, ni muhimu kugeuza shingo, kufungua masikio na kusikiliza nini wengine wanasema kuhusu kiongozi huyu wa dola kuu la Marekani. Na, kwa ujumla mawazo yao hatuwezi kuyachukua kiurahisi, ni lazima tuyabebe kwa uzito unaostahili. Tuyapime, tuyachekeche na tujitathmini sisi kama Taifa na wapi tulipo, tunakokwenda na namna gani tunataka kufika huko.

Pamoja sana.

Obama … Apingwa na Sall kuhusu Haki za Mashoga

with 3 comments


Rais Barack Obama akitazama kupitia mlango wa mahali pa kihistoria unaojulikana kama "mlango wa kutorejea" ("door of no return") alipotembelea Kisiwa cha Goree, Alhamis, 27 Juni, 2013, nchini Senegali. Kisiwa hicho kilikuwa eneo la nyumba ya watumwa na mahali pa kuwapakilia kwenye meli. Kituo hicho kilijengwa na Wadachi mwaka 1776. Ilikuwa kutokea hapo ambapo watumwa walisafirishwa kwenda Amerika. "Mlango wa kutorejea" ulikuwa mahali pa kupandia meli za watumwa. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais Barack Obama akitazama kupitia mlango wa mahali pa kihistoria unaojulikana kama “mlango wa kutorejea” (“door of no return”) alipotembelea Kisiwa cha Goree, Alhamis, 27 Juni, 2013, nchini Senegali. Kisiwa hicho kilikuwa eneo la nyumba ya watumwa na mahali pa kuwapakilia kwenye meli. Kituo hicho kilijengwa na Wadachi mwaka 1776. Ilikuwa kutokea hapo ambapo watumwa walisafirishwa kwenda Amerika. “Mlango wa kutorejea” ulikuwa mahali pa kupandia meli za watumwa. (AP Photo/Evan Vucci)

Obama, mwenyeji wake wa Kiafrika watofautiana kuhusu haki za mashoga

Na JULIE PACE | The Associated Press
Dakar, Senegali

Likiwa ni tukio la mgangano wa kiutamaduni, Rais Barack Obama, siku ya Alhamis aliwahimiza viongozi wa Kiafrika kufikiria kutoa haki sawa kwa watu wanaoshiriki ngono za jinsi moja, lakini pendekezo hilo lilikatishwa na kauli kali ya Rais wa Senegali, aliyesema kwamba nchi yake “haikuwa tayari” kufanya ngono ya jinsia moja isiwe kosa la jinai.

Obama alianza safari yake ya juma zima barani Afrika siku moja tu baada ya Mahakama ya Juu kabisa ya Marekani kupanua wigo wa kifedelali kuhusu ‘wanandoa’ wa jinsi moja. Katika maoni yake ya kwanza kabisa binafsi kuhusiana na uamuzi huo wa mahakama, Obama alisema uamuzi huo ulikuwa wa “kujivunia sana kwa Marekani”. Alisisitiza kutambuliwa kwa haki kama hiyo barani Afrika, ambapo aligusa eneo nyeti katika ukanda ambamo nchi dazeni kadhaa zina sheria zinazopiga marufuku ngono ya jinsi moja, na nyingine hata kutoa hukumu ya kifo kwa ukiukwaji wowote wa sheria hiyo.

“Linapokuja suala la namna gani dola linawatendea watu, jinsi sheria inavyoshughulika na watu, ninaamini kwamba kila mmoja anastahili kutendewa kwa usawa,” Obama alisema wakati wa mkutano na vyombo vya habari akiwa pamoja na Rais wa Senegali Macky Sall katika Ikulu ya nchi hiyo, jijini Dakar.

Lakini Rais Sall hakuwa na subira. Alimhakikishia Rais Obama kwamba Senegali ni “nchi yenye ustahimilivu mkubwa,” lakini “haiko tayari bado kufanya ngono ya jinsi moja isiwe kosa la jinai.” Sall alisema kwamba nchi hufanya uamuzi kuhusu masuala mazito katika wakati wao yenyewe, akisema kwamba Senegali imefuta hukumu ya kifo wakati ambapo nchi nyingine hazijafanya hivyo — jibu hilo likiwa ni kisu kikali dhidi ya Marekani, ambapo hukumu ya kifo bado ni halali katika majimbo yaliyo mengi.

Safari ya Obama, ambayo itamchukua hati Afrika ya Kusini na Tanzania, ndio safari ya kwanza ndefu zaidi kufanywa na Rais huyo wa kwanza mweusi wa Marekani tangu alipoingia madarakani. Waafrika wengi wameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha kujihusisha kwa Obama na masuala yanayoendelea barani humu — hasa kwa kuzingatia kwamba baba yake alikuwa raia wa Kenya na ana ndugu wengi wanaoishi barani Afrika — ingawa pamoja na hayo, bado alipokewa kwa mashamushamu makubwa.

Maelfu ya watu walikusanyika kandokando ya barabara karibu na Ikulu wakati msafara wa Obama ulipopita kandokando ya jiji hilo la pwani. Watu wengi walivaa mavazi meupe kuashiria amani. Wapo wengi waliopeperusha ujumbe mbalimbali wa kumkaribisha Obama, wakati ambapo wengine walikusanyika karibu na lango kuu la Ikulu na kuimba nyimbo na kucheza ngoma, sauti ya yote hayo ilikuwa ya juu kabisa.

Chanzo: http://www.sltrib.com/sltrib/world/56524571-68/obama-president-africa-senegal.html.csp

Maoni

Naam. Ninamwunga mkono Rais Macky Sall kuhusu msimamo na mtazamo wa suala la ngono za jinsi moja. Kama tukilegeza msimamo huo, kuna siku ‘wezi’ nao watataka watambuliwe kuwa wana haki ya kuiba eti kwa sababu kuna wale ambao ‘wasipoiba’ hawajisikii amani. Kweli?

Na, Rais Sall ameniongezea ufahamu mwingine, siku zote ninapinga adhabu ya kifo. Nimefurahi sana kufahamu kwamba nchi ya Senegali ni moja katika zile zilizokwishafuta adhabu hiyo. Tanzania tunasubiri nini? Hivi kuna nini hasa katika adhabu hii ya kifo? Unamwua mtu (unayemhukumu kwamba ni mkosaji), kisha nini kinafuatia baada ya kifo chake? Kama aliua mtu, basi unapomwua mtu huyu, tayari watu wawili wamekufa. Kama mtu aliyeuwawa kwanza alikuwa anategemewa na familia ya watu watano, na huyu wa pili naye (mwuaji) anategemewa na watu watano, tayari kunakuwa na watu kumi waliopoteza walishi wao. Kwa hakika, kwa sababu hii na nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na kutojua nini hasa kinafuata baada ya kifo (ukiachilia mbali imani za kidini), adhabu ya kifo haina msaada wowote.

Pamoja sana.

Obama … Tanzania, Afrika Zitarajie Nini?

leave a comment »


Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakipunga mkono kabla ya kuingia kwenye ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One.

Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakipunga mkono kabla ya kuingia kwenye ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One.

Rais wa Marekani Barack Obama anatembelea Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Kwa ujumla, Waafrika wamepoteza mashamsham waliyokuwa nayo kwa rais wa kwanza Mweusi wa Marekani, hata hivyo, bado kuna wale walio tayari kumpa tena fursa.

Baadhi ya wenyeji wa Bara la Afrika walikuwa na matarajio makubwa sana baada ya Obama, ambaye ana asili ya Kenya, alipochaguliwa kwanza mwaka 1008. Wengi walifikiri kwamba, je, ni nani mwingine kama si rais huyu, ambaye angeweza kuirejeshea Afrika hadhi yake inayostahili? Zaidi ya miaka minne baadae, homa hiyo inaelekea kuyeyuka. Kiasi cha utayari wa Obama kushirikiana na Afrika, kimeonekana kuwa chini kuliko hata kwa watangulizi wake (weupe).

Kupitia hotuba yake aliyoitoa katika Bunge la Ghana mwaka 2009, alikuwa amewapa Waafrika matarajio makubwa zaidi.

“Kwanza kabisa, nina damu ya kutoka Afrika ndani mwangu. Historia ya familia yangu inabeba matukio yote ya huzuni na ushindi ya historia pana zaidi ya Afrika,” alisema rais huyo wa Marekani.

Kulikuwa na shangwe nyingi pale Obama alipokiri hadharani kuhusu asili yake ya Afrika. Alikemea vikali ufisadi barani Afrika na kudai kwamba Waafrika lazima wabebe jukumu la kusimamia maisha yao wanyewe, lakini yote hayo yaelekea yalimezwa na shamrashamra hizo za furaha.

Je, ni nani kama si rais wa kwanza Mweusi wa Marekani angaliweza kubadili upepo wa sera ya Marekani kuhusu Afrika hasa kwa kuchochea uwekezaji na utalii wa moja kwa moja?

Hata hivyo, jambo hilo halikutokea. Bw David Shinn alikuwa balozi wa Marekani nchini Ethiopia na Burkina Faso, na sasa ni Profesa wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha George Washington.

Alisema Marekani ilikuwa ikikabiliwana mambo makubwa mno, hasa mgogoro wa fedha, jambo lililotatiza ushiriki wa jitihada za Obama kuelekea Afrika katika muhula wake wa kwanza kama rais. “Nadhani hivi sasa anajaribu kurekebisha upungufu huo katika muhula huu wa pili,” aliliambia Shirika la Habari la DW.

Hata hivyo, itakuwa si haki kumtuhumu Obama na Wizara ya Mambo ya Nje kuipa kisogo Afrika. Obama aliingilia kati mwenyewe katika mgogoro wa Sudan na hata alimtuma mjumbe wake maalumu ili kuokoa upigwaji wa kura ya maoni katika Sudani Kusini na hatimaye nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 2011.

Mwaka uliofuata, Obama aliwaalika viongozi wa Afrika katika Mkutano wa G8 kule Camp David ili kushiriki katika jitihada za serikali ya Marekani ya ‘Lisha Kizazi Kijacho’, mkakati uliolenga kukuza usalama wa chakula, na ambao hivi sasa unatekelezwa katika nchi 20, zikiwamo Senegali na Tanzania, nchi ambazo katika safari yake hii atazitembelea.

Utawala wa Obama pia umejituma katika masuala yenye utatanishi kama vile kutuma vikosi maalumu ili kwenda kumsaka Joseph Kony huko Afrika ya Kati au kujenga vikosi vyake nchini Ethiopia, Niger na Djibouti.


Chanzo cha habari kuu
: http://www.dw.de/obama-on-three-nation-african-tour/a-16909317

Je, safari ya Obama inaweza kuwa na athari gani kwa Tanzania?

— Ongezeko la uwekezaji kutoka Marekani, hususan katika Kilimo cha mashamba makubwa
— Uchimbaji wa madini ya urani
— Uchimbaji wa mafuta na gesi ya asili
— Kuja kwa kambi la Marekani kwa ajili ya AFRICOM?

Je, hayo yanaweza kuwa na athari zipi?
— Sera za ardhi inaweza kuguswa, kwani ili kupata mashamba makubwa kwa kilimo cha kibiashara, huenda baadhi ya watu/wanakijiji watalazimika kuhama kutoka maeneo yao
— Biashara ya urani mara nyingi ina utata mkubwa na pale inapoanza kuchimbwa, inaweza kuleta athari kwa viumbe hai na mazingira
— Vita dhidi ya ugaidi kuimarishwa katika ukanda huu wa Afrika
— Biashara ya mafuta na gesi ya asili kunufaisha kundi dogo tu la wananchi wa Tanzania moja kwa moja.

Waziri Mkuu wa Zamani … Miaka Saba Jela

leave a comment »


Bi Karima na Bw Silvio Berlusconi

Bi Karima na Bw Silvio Berlusconi

Hukumu ya Bunga Bunga: Silvio Berlusconi Akutwa na Hatia

Na Nick Pisa, Jijini Milano

Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Bw Silvio Berlusconi, amejitetea kwamba yeye “hana hatia hata chembe” baada ya kukutwa na hatia ya kulipa kwa ajili ya ngono kwa kahaba mwenye rika la mtoto.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76 alihukumiwa miaka saba jela na kupigwa marufuku kushika wadhifa wowote wa uongozi na majaji watatu wa Jijini Milano.

Mwanzoni alikanusha kujihusisha na vitendo vya ngono na Karima El Mahroug, anayejulikana pia kama Ruby the Heart Stealer, baada ya waendesha mashtaka kudai kwamba kulikuwa na tafrija za ngono zilizoitwa “bunga bunga” katika kasri la thamani kubwa la Bw Berlusconi mwaka 2010.

“Nilikuwa na imani kubwa sana kwamba ningeachiliwa huru kwani hakukuwa na uwezekano wa kukutwa na hatia, hasa kwa kuzingatia ushahidi,” alisema.

“Ninakusudia kupinga mashtaka kwa sababu mimi sina hatia kabisa na sitaki kupoteza mapambano yangu ya kuifanya Italia iwe huru na ya haki
kweli.”

Wakati wa kesi, mahakama iliwasikia dazeni kwa dazeni ya wasichana, akiwemo Bi El Mahroug, ambaye wakati wa tukio alikuwa na umri wa miaka 17 tu, ambapo walilipwa kwa fedha taslimu, malipo mengine na hata magari ili kushiriki kwenye tafrija za ngono za Berlusconi na hata kucheza mbele yake wakiwa nusu uchi.

Vilevile, Berlusconi pia alikutwa na hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kumsaidia Bi El Mahrough, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, kuachiwa kutoka mahabusu alipokamatwa kwa kushukiwa kwa wizi.

Upande wake wa utetezi ulidai kwamba yeye aliamini kwamba mcheza muziki huyo alikuwa mpwa wa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak na kwamba alikuwa akijaribu kuepuka tatizo la kidiplomasia.

Wakili wake, Niccolo Ghedini, alithibitisha kwamba watakata rufaa, huku akiielezea hukumu hiyo kama “ilisiyoendana na hali halisi” na “isiyo na mantiki hata chembe”.

“Tazama, majaji wamekwenda mbali zaidi ya kile walichoomba waendesha mashtaka, hukumu ya miaka sita,” alisema.

Kila mara Berlusconi amesisitiza kwamba alikuwa akikandamizwa na majaji kwa sababu za kisiasa.

Hata hivyo, mchakato wa rufaa unaweza kuchukua miaka mingi kabla haujakamilika, kwa sheria za Italia.

Mwezi Oktoba uliopita, Berlusconi alihukumiwa miaka minne jela kwa kosa la kuepa kodi kuhusiana na vituo vyake vya televisheni.

Kesi hiyo kwa sasa inasikilizwa katika mahakama ya juu kabisa na ya mwisho kwa rufani, baada ya upande wake wa utetezi kushindwa kukwamisha
hukumu hiyo katika mahakama ya kikatiba.

Chanzo: http://uk.news.yahoo.com/silvio-berlusconi-found-guilty-sex-trial-152906400.html#4BnSKXg

Naam. Kama hukumu za namna hii zingetiliwa mkazo nchini Tanzania, sijui ni nani angepona, maana mmm! matumizi mabaya ya ofisi, ndoa zinazohusisha mabinti chini ya umri wa miaka 18, ma-shuga dadi na ma-shuga mami. Kazi kwelikweli.

Walter Rodney … 33 Years Later

leave a comment »


Walter Rodney

Walter Rodney

Walter Rodney's image on Tee-shirt.

Walter Rodney’s image on Tee-shirt.

The death anniversary of Dr. Walter Rodney is upon us and still no closure

By Oscar Ramjeet

It was on June 14, 1980, when for the first time, the BBC 7.15 Caribbean report was blocked from the Guyana Broadcasting Corporation because the powers that be did not want the public to learn of the assassination of Dr. Walter Rodney, the popular and powerful historian whose life was snuffed out the night before – Friday the 13th… ‘Black Friday’ – by a bomb which was in the form of a walkie-talkie.

Up to this day, 33 years later, the authorities still fail to bring to light who was behind the daring murder of the great leader who bridged the racial gap between Indo- and Afro-Guyanese.

The Forbes Burnham administration failed to hold an Inquiry, but the Desmond Hoyte-led government in 1988 – eight long years after the slaying – ordered an Inquest, only after Rodney’s widow, Patricia Rodney addressed a sorrowing letter, followed by protest from a group called “Women in Guyana” which sent a petition via Rodney’s mother to President Hoyte.

However that Inquest was “marred by grave defects” by the International Commission of Jurists (ICJ) when it visited Guyana. The finding of the Coroner “death by accident or misadventure” was said to be unsatisfactory and flawed for many reasons.

What is disturbing is that Dr. Cheddi Jagan when he took office in 1992, instead of ordering a high-powered Commission of Inquiry, threw cold water by stating that he “wondered what the conviction and imprisonment of the suspect would do for Walter Rodney”. He however conferred Guyana’s highest award – The Order of Excellence – on Walter Rodney posthumously. The Guyana Archives many years later was named after him.

Jagan’s action did not find too much favour with the historian’s son, Shaka, who held a fast and vigil which prompted Caribbean Rights and the ICJ to be involved. Steps were taken to repatriate the suspect, Gregory Smith, from Cayenne in French Guiana, after he was formerly charged with murder in 1996 and
a warrant of arrest was issued by the then Chief Magistrate, K Juman Yassin.

Smith, a former Guyana Defence Force sergeant left for French Guiana the day after the murder and was using another name, Cyril Johnson. His extradition was delayed because the French government prohibited extradition for offences involving capital punishment – the death penalty.

Smith is reported to have died in 2002 from stomach cancer. However the Rodney family and his supporters still want to know who was behind the assassination of this great man who was deemed persona non grata by Hugh Shearer, Jamaica Prime Minister, which led to student demonstration at Mona Campus of the UWI, lead by Ralph Gonsalves, who was at the time Head of the Students Union. Dr. Gonsalves is now the Prime Minister of St. Vincent and the Grenadines.

After his ban in Jamaica, the Burnham administration denied Dr. Rodney a job at the University of Guyana, which forced him to move into politics. His book “How Europe Underdeveloped Africa” was a best seller in the 1970s.

Source: http://pambazuka.org/en/category/features/87813

Naam. Wanamapinduzi ya kweli watazidi kuenziwa kwa miongo na karne nyingi baadaye. Pumzika kwa amani Walter Rodney. Miaka 33 sasa tangu ututoke, lakini mapambano uliyoanzisha bado yanaendelea.

Brazili … Hali Yazidi kuwa Tete

leave a comment »


Machafuko yanazidi kuwa tete na yenye kuonyesha hasira za watu, jambo linalozidi kuhatarisha amani na ustawi wa nchi hiyo.

Machafuko yanazidi kuwa tete na yenye kuonyesha hasira za watu, jambo linalozidi kuhatarisha amani na ustawi wa nchi hiyo.

Takwimu muhimu kuhusu yanayoendelea nchini Brazili.

Takwimu muhimu kuhusu yanayoendelea nchini Brazili.

Ghasia za Brazili: Watu ‘milioni’ moja waandamana

Zaidi ya watu milioni moja wameripotiwa kujiunga na maandamano katika zaidi ya miji 100 kote nchini Brazil, yote yakiwa katika mfululizo wa maandamano ya ghasia yaliyoikumba nchi hiyo.

Ghasi ziliyakumba maeneo mengi ambapo kijana mmoja mwenye umri wa miaka18 alifariki dunia baada ya gari kukiingia kizuizi kwa mwendo kasi huko katika jimbo la Sao Paulo.

Upotevu wa amani ulianza kujitokeza tangu wiki iliyopita kupinga ongezeko la nauli, lakini sasa yanahusishwa na kupinga ufisadi na gharama kubwa ya maandalizi kwa Mashindano ya Kombe la Dunia hapo mwakani.

Rais Dilma Rousseff alifuta safari yake ya kwenda nchini Japan ili apate fursa ya kushughulikia mgogoro huo.

Ameitisha mkutano wa dharura wa Baraza lake la Mawaziri leo Ijumaa ili kujadili machafuko hayo.

Gazeti la Folha de Sao Paulo, likinukuu takwimu rasmi, lilisema kwamba zaidi ya watu milioni moja walishiriki katika maandamano siku ya Alhamis.

Vyombo vya habari nchini Brazil vilisema maandamano hayo yaliyoandamana na ghasia yalifanyika katika zaidi ya majiji 100.

Huko Rio de Janeiro, askari wa kutuliza ghasia walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kutawanya makundi ya vijana walioficha nyuso zao na waliokuwa wakiijongelea Ofisi Kuu ya Jiji hilo siku ya Alhamis. Walau watu 29 wameripotiwa kujeruhiwa.

Mamlaka jijini Rio waliweka ulinzi mkali kuzunguka jengo la Bunge la jimbo hilo, ofisi ya Seneta, Makao Makuu ya utawala ya Guanabara na ofisi ya Meya.

Picha za televisheni zilionyesha makundi ya wahalifu wakivunja na kuiba kutoka katika maeneo ya biashara katikati ya jiji hilo — ingawa wafanyabiashara walio wengi wa jijini humo walikuwa wamejenga ngao nzito za mbao ili kuzuia vitendo vya wizi kwenye biashara zao.

“Si tena suala la nauli,” alisema mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18, Camila Sena wakati akishiriki kwenye maandamano hayo katika Jiji la Niteroi, karibu na Rio de Janeiro, siku ya Jumatano.

“Wati wamechoshwa kabisa na mfumo, wamechoshwa mno, na sasa tunachodai ni mabadiliko.”

Ghasia zinazoendelea sasa ni kubwa kuliko zote tangu mwaka 1992, wakati ambapo watu waliingia mitaani kudai kuondolewa kwenye madaraka kwa Rais wa wakati huo, Bw Fernando Collor de Mello.


Taarifa za nyongeza:

1. Brazili ni moja kati ya mataifa matano yanayoibukia kwa nguvu za kiuchumi (nchi hizi hujulikana kama BRICS, yaani, Brazil, Russia, India, China na South Africa).

2. Brazili imekuwa na uhusiano mzuri (kwa viwango vya wastani) na Tanzania. Katika miezi ya hivi karibuni, kampuni ya Brazili la uchimbaji mafuta na gesi, Petro Bras, imepata fursa za kuendesha biashara yake hiyo kwa viwango tofauti hapa nchini.

3. Brazili ina uchumi unaokuwa kwa kasi sana duniani, kiasi cha kuelekea kuipuku hata Uingereza.

4. Pamoja na taarifa hizo muhimu, machafuko haya yanatupa picha kwamba mambo si shwari sana nchini humo. Kasi ya ukuaji uchumi inawanufaisha wachache na walio wengi wanabaki wakiishi maisha ya kubangaiza.

5. Swali. Tujifunze nini kutoka nchini Brazili na hayo yanayoendelea? Unaweza kuwa na majibu kwa swali hili, lakini, baadhi ni haya: Tujenge taifa lenye uwiano kimapato, tutoe haki kwa kila mmoja, tukumbuke kujenga kundi kubwa zaidi la watu wa kipato cha kati kuliko kuwa na watu wachache tu ndiyo wanaoshikilia uchumi wote. Tafadhali lete majibu yako.

Chanzo cha habari kuu: BBC News

Written by simbadeo

June 21, 2013 at 3:19 pm

Viongozi wa G8 … Tazama Uvaaji

with 4 comments


Naam. Hawa ndiyo viongozi wa Mataifa 8 mazito zaidi duniani kiuchumi, kijeshi na kiushawishi. Nimeguswa sana na uvaaji wao ulio 'simple' and 'unsophisticated' tofauti sana na ulimwengu wetu huku. Bado hainiingii akilini unawezaje kuvaa suti jijini Dar es Salaam na likawa ndiyo vazi lako la kila siku. Well. Ni maoni binafsi hata hivyo.

Naam. Hawa ndiyo viongozi wa Mataifa 8 mazito zaidi duniani kiuchumi, kijeshi na kiushawishi. Nimeguswa sana na uvaaji wao ulio ‘simple’ and ‘unsophisticated’ tofauti sana na ulimwengu wetu huku. Bado hainiingii akilini unawezaje kuvaa suti jijini Dar es Salaam na likawa ndiyo vazi lako la kila siku. Well. Ni maoni binafsi hata hivyo.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Afadhali hali ya hewa ya Burundi inaruhusu uvaaji huu ... lakini Dar?

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi. Afadhali hali ya hewa ya Burundi inaruhusu uvaaji huu … lakini Dar?

Written by simbadeo

June 20, 2013 at 8:33 am

Tanzania, Uganda … Sare sare kodi ya simu

leave a comment »


Watu wengi -- katika nchi za Afrika ya Mashariki -- hutumia simu ili kupokea na kutuma fedha. Huduma hii pamoja na nyinginezo zinazohusiana na matumizi ya simu za mkononi zitaanza kutozwa kodi ya ushuru.

Watu wengi — katika nchi za Afrika ya Mashariki — hutumia simu ili kupokea na kutuma fedha. Huduma hii pamoja na nyinginezo zinazohusiana na matumizi ya simu za mkononi zitaanza kutozwa kodi ya ushuru.

Uganda itaanza kutoza kodi kwa kiasi cha asilimia 10 katika utumaji fedha kwa njia ya simu za mkononi na nyinginezo.

Fedha zinazotumwa na raia wa Uganda wanaoishi nje ya nchi pia zitaingia kwenye mkumbo huo.

Waziri wa Fedha Maria Kiwanuka alisema alikuwa anakusudia kukusanya kiasi cha Dola za Marekani 16.5 milioni (karibu sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 25) kwa kutoza kodi ya ushuru kwenye simu za miito ya kimataifa zinazopigwa kwenda nchini humo.

Bi Kiwanuka pia alilazimika kutafuta namna ya kupata fedha za kuziba pengo la kiasi cha Dola za Marekani 214 katika bajeti ya mwaka baada ya wafadhali kupunguza misaada kutokana na shutuma za ufisadi.

Mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga aliye kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, alisema kwamba kumekuwa na ukosoaji wa bajti iliyosombwa Bungeni siku ya Alhamis kwamba itawakandamiza sana watu wa kipato cha chini zaidi nchini humo.

Utumaji fedha kwa njia ya simu imekuwa namna maarufu na rahisi zaidi kwa watu wengi katika taifa hilo, sawa na mataifa mengine ya ukanda wa Afrika ya Mashariki. Njia hiyo inatumiwa sana hata kwa watu wasio na akaunti za benki, wote, wa mijini na vijijini.

Wakala mmoja wa huduma za kutuma na kupokea fedha kwa njia ya simu alimwambia mwandishi huyo kwamba kwa kawaida huingiza hadi Dola za Marekani 8,000 (sawa na Shilingi za Tanzania milioni 13) kwa mwaka kutokana na biashara hiyo.

Bi Kiwanuka aliwaambia Wabunge kwamba mwaka jana kiasi cha Dola za Marekani milioni 767 (karibu sawa na Shilingi za Tanzania bilioni 125) kilitumwa nchini humo na raia wanaoishi nje.

Kwa mujibu wa gazeti binafsi la nchini humo, Daily Monitor, kodi hiyo mpya kwenye utumaji fedha kwa njia ya simu za mkononi utawaathiri watu wasiopungua milioni 8.9.

Wakati huohuo, Waziri wa Fedha katika nchi jirani ya Tanzania, Bw William Mgimwa, naye akisoma bajeti ya Serikali Bungeni siku ya Alhamis alitangaza kuanzishwa kwa tozo ya kodi kwenye utumaji fedha kwa njia ya simu. Alifafanua kwamba kodi hiyo itagusa kamisheni wanayopokea mawakala wa kutoa huduma hiyo. Tozo itakuwa asilimia 10 ya kamisheni. Hii itakusanywa na makampuni ya utoaji huduma za simu za mkononi.

Chanzo cha habari kuu: BBC News

Kenya … Wabunge ‘wakubali kupunguza mishahara’

leave a comment »


Mmoja wa waandamanaji akionyesha fedha ya Kenya ikiwa na mchoro wa nguruwe kufuatia maandamano ya tarehe 11 Juni, 2013. Waandamanaji hao waliwatuhumu Wabunge wa Kenya kwa uroho uliokithiri.

Mmoja wa waandamanaji akionyesha fedha ya Kenya ikiwa na mchoro wa nguruwe kufuatia maandamano ya tarehe 11 Juni, 2013. Waandamanaji hao waliwatuhumu Wabunge wa Kenya kwa uroho uliokithiri.

Wabunge wa Kenya wamekubali kupunguza mishahara yao kwa kiasi cha Dola za Marekani 45,000 (sawa na Shilingi za Tanzania milioni 65) ambapo sasa watapokea jumla ya Dola za Marekani 75,000 (sawa na Shilingi za Tanzania milioni 130) kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa chombo cha serikali nchini humo.

Hata hivyo, Wabunge watapokea posho ya gari yenye thamani ya Dola za Marekani 58,000 (sawa na Shilingi za Tanzania milioni 90) kwa kukubali kwao kupunguza mshara, Tume ya Kusimamia Mishahara na Maslahi (SRC) ilisema.

Jumanne wiki hii, waandamanaji katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, waliwalaani Wabunge wakiwalinganisha na ‘nguruwe’.

Awali, Wabunge hao walikuwa wamepitisha mshahara wenye thamani ya Dola za Marekani 120,000 (karibu sawa na shilingi za Tanzania milioni 200) mwezi Mei, kinyume na mapendekezo ya SRC na Rais Uhuru Kenyatta.

Wabunge hao walitoa hoja kwamba kazi yao ni ngumu sana na mara nyingi walitoa misaada ya kifedha kwenye majimbo yao.

Hata hivyo, uamuzi wao huo ulipokewa kwa hasira karibu nchini kote kwa kuwa Wabunge hao ni miongoni mwa wale wanaolipwa vizuri zaidi duniani, huku wastani wa kipato cha raia wa kawaida nchini humo kikiwa karibu Dola za Marekani 1,800 (sawa na Shilingi za Tanzania Milioni 3) kwa mwaka.

Wabunge walikubali kupunguza kipato chao kwa karibu asilimia 40 kufuatia mazungumzo ‘yaliyozaa matunda’ kati yao na SRC.

Chanzo cha Habari: BBC News

Written by simbadeo

June 13, 2013 at 12:56 pm