simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Obama … Apingwa na Sall kuhusu Haki za Mashoga

with 3 comments

Rais Barack Obama akitazama kupitia mlango wa mahali pa kihistoria unaojulikana kama "mlango wa kutorejea" ("door of no return") alipotembelea Kisiwa cha Goree, Alhamis, 27 Juni, 2013, nchini Senegali. Kisiwa hicho kilikuwa eneo la nyumba ya watumwa na mahali pa kuwapakilia kwenye meli. Kituo hicho kilijengwa na Wadachi mwaka 1776. Ilikuwa kutokea hapo ambapo watumwa walisafirishwa kwenda Amerika. "Mlango wa kutorejea" ulikuwa mahali pa kupandia meli za watumwa. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais Barack Obama akitazama kupitia mlango wa mahali pa kihistoria unaojulikana kama “mlango wa kutorejea” (“door of no return”) alipotembelea Kisiwa cha Goree, Alhamis, 27 Juni, 2013, nchini Senegali. Kisiwa hicho kilikuwa eneo la nyumba ya watumwa na mahali pa kuwapakilia kwenye meli. Kituo hicho kilijengwa na Wadachi mwaka 1776. Ilikuwa kutokea hapo ambapo watumwa walisafirishwa kwenda Amerika. “Mlango wa kutorejea” ulikuwa mahali pa kupandia meli za watumwa. (AP Photo/Evan Vucci)

Obama, mwenyeji wake wa Kiafrika watofautiana kuhusu haki za mashoga

Na JULIE PACE | The Associated Press
Dakar, Senegali

Likiwa ni tukio la mgangano wa kiutamaduni, Rais Barack Obama, siku ya Alhamis aliwahimiza viongozi wa Kiafrika kufikiria kutoa haki sawa kwa watu wanaoshiriki ngono za jinsi moja, lakini pendekezo hilo lilikatishwa na kauli kali ya Rais wa Senegali, aliyesema kwamba nchi yake “haikuwa tayari” kufanya ngono ya jinsia moja isiwe kosa la jinai.

Obama alianza safari yake ya juma zima barani Afrika siku moja tu baada ya Mahakama ya Juu kabisa ya Marekani kupanua wigo wa kifedelali kuhusu ‘wanandoa’ wa jinsi moja. Katika maoni yake ya kwanza kabisa binafsi kuhusiana na uamuzi huo wa mahakama, Obama alisema uamuzi huo ulikuwa wa “kujivunia sana kwa Marekani”. Alisisitiza kutambuliwa kwa haki kama hiyo barani Afrika, ambapo aligusa eneo nyeti katika ukanda ambamo nchi dazeni kadhaa zina sheria zinazopiga marufuku ngono ya jinsi moja, na nyingine hata kutoa hukumu ya kifo kwa ukiukwaji wowote wa sheria hiyo.

“Linapokuja suala la namna gani dola linawatendea watu, jinsi sheria inavyoshughulika na watu, ninaamini kwamba kila mmoja anastahili kutendewa kwa usawa,” Obama alisema wakati wa mkutano na vyombo vya habari akiwa pamoja na Rais wa Senegali Macky Sall katika Ikulu ya nchi hiyo, jijini Dakar.

Lakini Rais Sall hakuwa na subira. Alimhakikishia Rais Obama kwamba Senegali ni “nchi yenye ustahimilivu mkubwa,” lakini “haiko tayari bado kufanya ngono ya jinsi moja isiwe kosa la jinai.” Sall alisema kwamba nchi hufanya uamuzi kuhusu masuala mazito katika wakati wao yenyewe, akisema kwamba Senegali imefuta hukumu ya kifo wakati ambapo nchi nyingine hazijafanya hivyo — jibu hilo likiwa ni kisu kikali dhidi ya Marekani, ambapo hukumu ya kifo bado ni halali katika majimbo yaliyo mengi.

Safari ya Obama, ambayo itamchukua hati Afrika ya Kusini na Tanzania, ndio safari ya kwanza ndefu zaidi kufanywa na Rais huyo wa kwanza mweusi wa Marekani tangu alipoingia madarakani. Waafrika wengi wameonyesha kutoridhishwa na kiwango cha kujihusisha kwa Obama na masuala yanayoendelea barani humu — hasa kwa kuzingatia kwamba baba yake alikuwa raia wa Kenya na ana ndugu wengi wanaoishi barani Afrika — ingawa pamoja na hayo, bado alipokewa kwa mashamushamu makubwa.

Maelfu ya watu walikusanyika kandokando ya barabara karibu na Ikulu wakati msafara wa Obama ulipopita kandokando ya jiji hilo la pwani. Watu wengi walivaa mavazi meupe kuashiria amani. Wapo wengi waliopeperusha ujumbe mbalimbali wa kumkaribisha Obama, wakati ambapo wengine walikusanyika karibu na lango kuu la Ikulu na kuimba nyimbo na kucheza ngoma, sauti ya yote hayo ilikuwa ya juu kabisa.

Chanzo: http://www.sltrib.com/sltrib/world/56524571-68/obama-president-africa-senegal.html.csp

Maoni

Naam. Ninamwunga mkono Rais Macky Sall kuhusu msimamo na mtazamo wa suala la ngono za jinsi moja. Kama tukilegeza msimamo huo, kuna siku ‘wezi’ nao watataka watambuliwe kuwa wana haki ya kuiba eti kwa sababu kuna wale ambao ‘wasipoiba’ hawajisikii amani. Kweli?

Na, Rais Sall ameniongezea ufahamu mwingine, siku zote ninapinga adhabu ya kifo. Nimefurahi sana kufahamu kwamba nchi ya Senegali ni moja katika zile zilizokwishafuta adhabu hiyo. Tanzania tunasubiri nini? Hivi kuna nini hasa katika adhabu hii ya kifo? Unamwua mtu (unayemhukumu kwamba ni mkosaji), kisha nini kinafuatia baada ya kifo chake? Kama aliua mtu, basi unapomwua mtu huyu, tayari watu wawili wamekufa. Kama mtu aliyeuwawa kwanza alikuwa anategemewa na familia ya watu watano, na huyu wa pili naye (mwuaji) anategemewa na watu watano, tayari kunakuwa na watu kumi waliopoteza walishi wao. Kwa hakika, kwa sababu hii na nyingine nyingi, ikiwa ni pamoja na kutojua nini hasa kinafuata baada ya kifo (ukiachilia mbali imani za kidini), adhabu ya kifo haina msaada wowote.

Pamoja sana.

Advertisements

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Maoni

  Nielewavyo mimi, adhabu ya kifo haimlengimkosaji aliyekutwa na kosa na kuhukumiwa kuuawa. Adhabu hiyo inawalenga wale ambao wangeshawishiwa kuua waogope kuwa wakiua watauawa, hivyo ni kinga. Kwenye mazishi yoyote, hotuba na mahubiri hayamlengi marehemu kwani ameshakufa, hasikii! Hotuba huwalenga wahudhuriaji. Kama alikuwa mwadilifu mtenda mema aigwe, kama alikuwa mwovu watu hushauriwa wasiige mfano wake. Ninaunga mkono adhabu ya kifo!

  *******************************************************

  Canute Temu, Tel +255754282101 Tanzania

  Residence, Vanilla/Cardamom Organic Gardens; Moshi, Kilimanjaro, Tanzania

  Educationist, Development Consultant, Translator, Interpreter, Logistics.

  *************************

  Do good and do it well : Fanya mema na yafanye vizuri.

  ****************

  Like

  canute temu

  June 28, 2013 at 6:47 pm

  • Ndugu Canute. Asante sana kwa maoni yako. Tunatofautiana kimtazamo kuhusu ‘adhabu ya kifo’. Nikitazama maoni yako, ni kwamba ‘adhabu’ hii inalengwa kwa wale ambao kwa sababu moja au nyingine hawajatenda kosa la kuua (au hata kama wamewahi kuua, basi pengine hawajafahamika au kuthibitika kuwahi kufanya hivyo). Kama hiyo ndiyo pekee sababu ya kuwepo kwa ‘adhabu’ hii ya kifo, ninajiuliza kwa nini mauaji yanaendelea kutokea — mara nyingine katika namna na sababu ambazo ni senseless kabisa. Kule Marekani, ambako majimbo mengi bado wanahusudu sana ‘adhabu hiyo’, utakuta kwamba mtu anaweza kujichukulia bunduki yake, anaingia katika shule au ukumbi wa starehe, anamimina risasi, watu kibao wanapoteza maisha … Sasa adhabu hiyo imesaidia vipi kukomesha vitendo na mauaji kama hayo? Lakini, kama ‘adhabu’ ingelengwa kwa huyu anayetoa uhai wa mwenzake, labda ingesaidia zaidi.

   Naelewa suala hili linahitaji mjadala mrefu na wa kina zaidi ya sentensi mbili tatu tunazoandika hapa. Hata hivyo, niseme tu kwamba ‘adhabu ya kifo’ haijasaidia kumfanya binadamu kuwa kiumbe bora zaidi.

   Vilevile, ninaona kwamba utetezi wako unawataka watu wawe na nidhamu ya woga, kwamba waogope ‘kuua’ kwa sababu nao watauwawa. Lakini, swali bado lipo palepale, je, kwa mtu asiyehofu kifo? Na tuelewe kwamba kuna watu wengi katika kundi hili, ndiyo maana unasikia mara nyingi tu watu wanajitoa mhanga wanajilipua wao pamoja na wengine!

   Hapa Tanzania hukumu hii imetusaidia vipi? Miaka ya hivi karibuni tumekuwa na matumizi ya nguvu kupita kiwango ya Jeshi la Polisi kiasi cha kusababisha mauaji ya watu/raia wasio na hatia … sina hakika tuseme nini kuhusu hili!

   Tuendelee na mjadala!

   Like

   simbadeo

   June 30, 2013 at 12:28 pm

 2. It was difficult to find your site in google. You should create some
  high Pagerank contextual backlinks in order to rank your blog.
  I know – writing articles is very time consuming,
  but contextual backlinks are the best type of backlinks. I know very useful tool that will help you to create
  unique, readable content in minute, just type in google – laranita free content

  Like

  Lorrine

  October 14, 2014 at 12:47 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: