simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Obama … Tanzania, Afrika Zitarajie Nini?

leave a comment »

Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakipunga mkono kabla ya kuingia kwenye ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One.

Rais Barack Obama na mkewe Michelle Obama wakipunga mkono kabla ya kuingia kwenye ndege ya Rais wa Marekani, Air Force One.

Rais wa Marekani Barack Obama anatembelea Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Kwa ujumla, Waafrika wamepoteza mashamsham waliyokuwa nayo kwa rais wa kwanza Mweusi wa Marekani, hata hivyo, bado kuna wale walio tayari kumpa tena fursa.

Baadhi ya wenyeji wa Bara la Afrika walikuwa na matarajio makubwa sana baada ya Obama, ambaye ana asili ya Kenya, alipochaguliwa kwanza mwaka 1008. Wengi walifikiri kwamba, je, ni nani mwingine kama si rais huyu, ambaye angeweza kuirejeshea Afrika hadhi yake inayostahili? Zaidi ya miaka minne baadae, homa hiyo inaelekea kuyeyuka. Kiasi cha utayari wa Obama kushirikiana na Afrika, kimeonekana kuwa chini kuliko hata kwa watangulizi wake (weupe).

Kupitia hotuba yake aliyoitoa katika Bunge la Ghana mwaka 2009, alikuwa amewapa Waafrika matarajio makubwa zaidi.

“Kwanza kabisa, nina damu ya kutoka Afrika ndani mwangu. Historia ya familia yangu inabeba matukio yote ya huzuni na ushindi ya historia pana zaidi ya Afrika,” alisema rais huyo wa Marekani.

Kulikuwa na shangwe nyingi pale Obama alipokiri hadharani kuhusu asili yake ya Afrika. Alikemea vikali ufisadi barani Afrika na kudai kwamba Waafrika lazima wabebe jukumu la kusimamia maisha yao wanyewe, lakini yote hayo yaelekea yalimezwa na shamrashamra hizo za furaha.

Je, ni nani kama si rais wa kwanza Mweusi wa Marekani angaliweza kubadili upepo wa sera ya Marekani kuhusu Afrika hasa kwa kuchochea uwekezaji na utalii wa moja kwa moja?

Hata hivyo, jambo hilo halikutokea. Bw David Shinn alikuwa balozi wa Marekani nchini Ethiopia na Burkina Faso, na sasa ni Profesa wa Masuala ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha George Washington.

Alisema Marekani ilikuwa ikikabiliwana mambo makubwa mno, hasa mgogoro wa fedha, jambo lililotatiza ushiriki wa jitihada za Obama kuelekea Afrika katika muhula wake wa kwanza kama rais. “Nadhani hivi sasa anajaribu kurekebisha upungufu huo katika muhula huu wa pili,” aliliambia Shirika la Habari la DW.

Hata hivyo, itakuwa si haki kumtuhumu Obama na Wizara ya Mambo ya Nje kuipa kisogo Afrika. Obama aliingilia kati mwenyewe katika mgogoro wa Sudan na hata alimtuma mjumbe wake maalumu ili kuokoa upigwaji wa kura ya maoni katika Sudani Kusini na hatimaye nchi hiyo kujipatia uhuru mwaka 2011.

Mwaka uliofuata, Obama aliwaalika viongozi wa Afrika katika Mkutano wa G8 kule Camp David ili kushiriki katika jitihada za serikali ya Marekani ya ‘Lisha Kizazi Kijacho’, mkakati uliolenga kukuza usalama wa chakula, na ambao hivi sasa unatekelezwa katika nchi 20, zikiwamo Senegali na Tanzania, nchi ambazo katika safari yake hii atazitembelea.

Utawala wa Obama pia umejituma katika masuala yenye utatanishi kama vile kutuma vikosi maalumu ili kwenda kumsaka Joseph Kony huko Afrika ya Kati au kujenga vikosi vyake nchini Ethiopia, Niger na Djibouti.


Chanzo cha habari kuu
: http://www.dw.de/obama-on-three-nation-african-tour/a-16909317

Je, safari ya Obama inaweza kuwa na athari gani kwa Tanzania?

— Ongezeko la uwekezaji kutoka Marekani, hususan katika Kilimo cha mashamba makubwa
— Uchimbaji wa madini ya urani
— Uchimbaji wa mafuta na gesi ya asili
— Kuja kwa kambi la Marekani kwa ajili ya AFRICOM?

Je, hayo yanaweza kuwa na athari zipi?
— Sera za ardhi inaweza kuguswa, kwani ili kupata mashamba makubwa kwa kilimo cha kibiashara, huenda baadhi ya watu/wanakijiji watalazimika kuhama kutoka maeneo yao
— Biashara ya urani mara nyingi ina utata mkubwa na pale inapoanza kuchimbwa, inaweza kuleta athari kwa viumbe hai na mazingira
— Vita dhidi ya ugaidi kuimarishwa katika ukanda huu wa Afrika
— Biashara ya mafuta na gesi ya asili kunufaisha kundi dogo tu la wananchi wa Tanzania moja kwa moja.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: