simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Rais Barack Obama … Karibu Tanzania

with 2 comments

Rais Obama na mkewe Michelle walipokuwa Afrika ya Kusini majuzi.

Rais Obama na mkewe Michelle walipokuwa Afrika ya Kusini majuzi.

Rais Obama na familia yake pamoja na walinzi wao.

Rais Obama na familia yake pamoja na walinzi wao.

Dar es Salaam ... evening before Obama visit.

Dar es Salaam … evening before Obama visit.

Obama in Tanzania June 2013 four

Dar es Salaam ... evening before Obama visit.

Dar es Salaam … evening before Obama visit.

Rais Barack Obama, karibu sana Tanzania, nchi ya amani na utulivu. Kama ilivyo ada yetu Watanzania, tunafurahi kukupokea na kukukirimu kwa ukunjufu wa mioyo yetu. Tunaelewa pia kwamba umeacha mambo mengi muhimu nchini kwako na kutenga muda ili kututembelea. Tunalithamani sana jambo hilo.

Tunaelewa pia kwamba unalenga kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya Taifa lako la Marekani na letu Tanzania. Kwa hakika, jambo hili ni jema na muhimu kwa ustawi wa watu wa pande zote mbili na ulimwengu kwa ujumla.

Hata hivyo, Taifa lako liko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kunufaika na kuimarishwa huku kwa uhusiano wa kibiashara kwani tayari watu wako wana nguvu kubwa ya kiuchumi na uzoefu mpana katika kuhimili biashara kubwa za kimataifa. Zaidi ya hayo, watu wako wana teknolojia ya kisasa kabisa kuweza kutumia rasilimali na kuibadili kuwa utajiri.

Pengine hapo ndipo palipo na mtihani kwetu. Watu wetu wanakosa mtaji, uzoefu na teknolojia sahihi. Tulicho nacho ni rasilimali na watu.

Unapohimiza kukuzwa kwa uhusiano baina ya pande mbili hizi, ni vema ukumbuke kuwahimiza watu wako (wafanyabiashara) kuchukua aina ya ubepari ule unaojali pia haki na maendeleo ya wenyeji. (Tunaelewa kwamba, kama ilivyo kwa siasa mbalimbali, ubepari nao umegawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna aina ile inayotazama kukuza tu faida ya wenye mtaji na haujali kama unaumiza wengine na hata kiasi cha kuwageuza kuwa watumwa nchini mwao. Mifano ya aina hii ya ubepari ipo mingi. Hata hapa kwetu tumeanza kuona makali yake.)

Kumbe basi, uhusiano huu uwe kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili, sisi tupate kukua (kwa haki na usawa) kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiroho nanyi mtengeneze faida kwa mitaji mtakayoweka.

Historia haifutiki na haifichiki. Tungependa tunapoingia katika ngazi hii ya uhusiano, tuingie tukiwa watu wenye utambuzi kamili na hiari ya kushiriki kikamilifu kwa manufaa yetu, ya vizazi vyetu vijavyo na vivyo hivyo kwa upande wa watu wako. Tafadhali, tuweke kando aina ile ya uhusiano ambao mababu zetu waliwahi kuwa na wageni. Katika uhusiano huo wa kale, wazazi wetu waliporwa mali, ardhi na hata watu wao kwa kupewa shanga, vioo na pombe kali. Hatutaki historia ituhukumu kwa kugawa rasilimali pasipo nasi kama Taifa kupata manufaa yanayostahili kwa haki na usawa.

Kuna hili la uchimbaji madini ya urani (Uranium). Pamoja na teknolojia ambayo Taifa lako linayo, bado madini haya kuyachokoza huko kwenye makazi yake (ardhini) pasipokuwa na umakini wa hali ya juu inaweza kugeuka janga kwetu na mazingira yetu. Tafadhali lipime sana hili. Kama hakuna ULAZIMA wa kuyachokoza huko yaliko hivi sasa, hebu tusubiri hata miaka mingine 100. Madini ya urani yanaweza kugeuka angamizo kuu la Sayari ya Dunia katika muda mfupi. Wakati huu ambapo baadhi ya mataifa yenye nguvu za kinyuklia yameamua kusitisha kuiendeleza (hata kama ni kwa matumizi salama), ni vema tukaacha kufikiri kuchimba urani hivi sasa (hata kama ina matumizi mengine). Yawezekana kabisa kwamba bado dunia nzima (Taifa lako likiwemo) halijapata teknolojia sahihi ya kutumia madini hayo kwa njia zilizo sahihi pasipo kuleta madhara kwa viumbe hai, mazingira na sayari yetu kwa ujumla wake.

Kuna uwekezaji katika mashamba makubwa. Hili linaweza kuwa jambo jema kwani kwa njia hiyo chakula kingi zaidi kitazalishwa na hivyo kuleta usalama zaidi wa chakula kwa ulimwengu. Lakini biashara hii isisababishe watu kuporwa ardhi zao na kuhamishwa (kwa nguvu au bila nguvu) kutoka maeneo yao ya asili wanakojipatia maisha, labda kama kwa kufanya hivyo, watu hawa watanufaika zaidi kupewa mbadala ambao utawafanya wapande ngazi kuelekea maisha bora zaidi kuliko yale wanayoishi sasa.

Hilo la kilimo huendana, mara nyingine, na uanzishwaji wa mazao ya kibaiolojia, wataalamu wanaita GMOs. Chonde chonde, dunia bado haijawa na teknolojia ya kuaminika kwa asilimia kubwa kuhusu mazao ya aina hii. Hebu tuendeleze mbegu bora lakini zile za asili.

Tanzania imekuwa nchi ya amani kwa miaka mingi. Tungependa hali hii idumu daima. Tusaidie katika kuimarisha demokrasia yetu ili tuelewe kwamba kutofautiana katika itikadi za kisiasa SIYO lazima kutugeuze kuwa maadui au mahasimu. Tufanye siasa zetu kwa njia ya ukomavu zaidi, njia yenye kuzingatia haki na usawa. Vyombo vya dola vitambue nafasi yake katika nchi, kwamba vyenyewe na watu wao havipaswi kuegemea huku wala kule. CCM, Chadema, TLP, CUF, NCCR-Mageuzi na vyama vingine vinaweza kutoweka hata leo, lakini Tanzania itabaki daima.

Kutokana na ujio wako, kuna ambao wameumia. Biashara zao ndogondogo za kujikimu zimebomolewa na wao kuhamishwa kutoka kwenye maeneo ya biashara. Si ajabu kwamba huenda kuna kaya kadhaa ambazo zimekosa mlo wao kwa sababu hawana mahali pa kujipatia riziki. Pengine uhimize kwamba baada ya safari yako, watu hawa wafidiwe kwa haki na kupatiwa maeneo mapya ya kufanya kazi zao, ili mradi wazingatie sheria na kanuni za kuendesha biashara za nchi hii.

Mwisho, jiji limesafishwa (kwa kiasi fulani), lakini hili si la kwako, hili ni la Mababa wa Jiji letu. Chonde chonde, zingatieni uwazi na uwajibikaji, tungependa kusikia fedha zinazotokana na kodi zetu kujua zilitumikaje na kama kuna uwiano kati ya matumizi na kile tunachokiona.

Vinginevyo, karibu sana Rais Barack Obama pamoja na familia yako. Karibu katika nchi ya amani, utulivu na ukarimu. Kwa pamoja tumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere kwa kutuwekea misingi mizuri ya maelewano na umoja wa kitaifa. Karibu sana.

Advertisements

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Worst AMERICAN President ever. An absolute embarrassment to America. He is laughable. His complexion led him to this position. He is inexperienced, a leftist and all talk. Do not believe the hype. An American in Tanzania

  Like

  Dabby

  July 2, 2013 at 6:00 am

 2. ….- As the world’s #1, have you now exposed yourself and shown everybody your wenk2ess&#8a30;..a cleavage and you’re all shaky and have lost your concentration??? Don’t you think you’ve made it very difficult for yourself?- Yes, but luckily – for me – it will take a while until all the players are ladies with cleavages:D- Aah, very good. I wish you good luck and hope you’ll stay on top as long as you live – Magnus Carlsen!

  Like

  Kalyn

  May 9, 2017 at 5:54 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: