simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Brazili … Hali Yazidi kuwa Tete

leave a comment »

Machafuko yanazidi kuwa tete na yenye kuonyesha hasira za watu, jambo linalozidi kuhatarisha amani na ustawi wa nchi hiyo.

Machafuko yanazidi kuwa tete na yenye kuonyesha hasira za watu, jambo linalozidi kuhatarisha amani na ustawi wa nchi hiyo.

Takwimu muhimu kuhusu yanayoendelea nchini Brazili.

Takwimu muhimu kuhusu yanayoendelea nchini Brazili.

Ghasia za Brazili: Watu ‘milioni’ moja waandamana

Zaidi ya watu milioni moja wameripotiwa kujiunga na maandamano katika zaidi ya miji 100 kote nchini Brazil, yote yakiwa katika mfululizo wa maandamano ya ghasia yaliyoikumba nchi hiyo.

Ghasi ziliyakumba maeneo mengi ambapo kijana mmoja mwenye umri wa miaka18 alifariki dunia baada ya gari kukiingia kizuizi kwa mwendo kasi huko katika jimbo la Sao Paulo.

Upotevu wa amani ulianza kujitokeza tangu wiki iliyopita kupinga ongezeko la nauli, lakini sasa yanahusishwa na kupinga ufisadi na gharama kubwa ya maandalizi kwa Mashindano ya Kombe la Dunia hapo mwakani.

Rais Dilma Rousseff alifuta safari yake ya kwenda nchini Japan ili apate fursa ya kushughulikia mgogoro huo.

Ameitisha mkutano wa dharura wa Baraza lake la Mawaziri leo Ijumaa ili kujadili machafuko hayo.

Gazeti la Folha de Sao Paulo, likinukuu takwimu rasmi, lilisema kwamba zaidi ya watu milioni moja walishiriki katika maandamano siku ya Alhamis.

Vyombo vya habari nchini Brazil vilisema maandamano hayo yaliyoandamana na ghasia yalifanyika katika zaidi ya majiji 100.

Huko Rio de Janeiro, askari wa kutuliza ghasia walitumia mabomu ya machozi na risasi za mpira kutawanya makundi ya vijana walioficha nyuso zao na waliokuwa wakiijongelea Ofisi Kuu ya Jiji hilo siku ya Alhamis. Walau watu 29 wameripotiwa kujeruhiwa.

Mamlaka jijini Rio waliweka ulinzi mkali kuzunguka jengo la Bunge la jimbo hilo, ofisi ya Seneta, Makao Makuu ya utawala ya Guanabara na ofisi ya Meya.

Picha za televisheni zilionyesha makundi ya wahalifu wakivunja na kuiba kutoka katika maeneo ya biashara katikati ya jiji hilo — ingawa wafanyabiashara walio wengi wa jijini humo walikuwa wamejenga ngao nzito za mbao ili kuzuia vitendo vya wizi kwenye biashara zao.

“Si tena suala la nauli,” alisema mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18, Camila Sena wakati akishiriki kwenye maandamano hayo katika Jiji la Niteroi, karibu na Rio de Janeiro, siku ya Jumatano.

“Wati wamechoshwa kabisa na mfumo, wamechoshwa mno, na sasa tunachodai ni mabadiliko.”

Ghasia zinazoendelea sasa ni kubwa kuliko zote tangu mwaka 1992, wakati ambapo watu waliingia mitaani kudai kuondolewa kwenye madaraka kwa Rais wa wakati huo, Bw Fernando Collor de Mello.


Taarifa za nyongeza:

1. Brazili ni moja kati ya mataifa matano yanayoibukia kwa nguvu za kiuchumi (nchi hizi hujulikana kama BRICS, yaani, Brazil, Russia, India, China na South Africa).

2. Brazili imekuwa na uhusiano mzuri (kwa viwango vya wastani) na Tanzania. Katika miezi ya hivi karibuni, kampuni ya Brazili la uchimbaji mafuta na gesi, Petro Bras, imepata fursa za kuendesha biashara yake hiyo kwa viwango tofauti hapa nchini.

3. Brazili ina uchumi unaokuwa kwa kasi sana duniani, kiasi cha kuelekea kuipuku hata Uingereza.

4. Pamoja na taarifa hizo muhimu, machafuko haya yanatupa picha kwamba mambo si shwari sana nchini humo. Kasi ya ukuaji uchumi inawanufaisha wachache na walio wengi wanabaki wakiishi maisha ya kubangaiza.

5. Swali. Tujifunze nini kutoka nchini Brazili na hayo yanayoendelea? Unaweza kuwa na majibu kwa swali hili, lakini, baadhi ni haya: Tujenge taifa lenye uwiano kimapato, tutoe haki kwa kila mmoja, tukumbuke kujenga kundi kubwa zaidi la watu wa kipato cha kati kuliko kuwa na watu wachache tu ndiyo wanaoshikilia uchumi wote. Tafadhali lete majibu yako.

Chanzo cha habari kuu: BBC News

Advertisements

Written by simbadeo

June 21, 2013 at 3:19 pm

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: