simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Waziri Mkuu wa Zamani … Miaka Saba Jela

leave a comment »

Bi Karima na Bw Silvio Berlusconi

Bi Karima na Bw Silvio Berlusconi

Hukumu ya Bunga Bunga: Silvio Berlusconi Akutwa na Hatia

Na Nick Pisa, Jijini Milano

Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Bw Silvio Berlusconi, amejitetea kwamba yeye “hana hatia hata chembe” baada ya kukutwa na hatia ya kulipa kwa ajili ya ngono kwa kahaba mwenye rika la mtoto.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 76 alihukumiwa miaka saba jela na kupigwa marufuku kushika wadhifa wowote wa uongozi na majaji watatu wa Jijini Milano.

Mwanzoni alikanusha kujihusisha na vitendo vya ngono na Karima El Mahroug, anayejulikana pia kama Ruby the Heart Stealer, baada ya waendesha mashtaka kudai kwamba kulikuwa na tafrija za ngono zilizoitwa “bunga bunga” katika kasri la thamani kubwa la Bw Berlusconi mwaka 2010.

“Nilikuwa na imani kubwa sana kwamba ningeachiliwa huru kwani hakukuwa na uwezekano wa kukutwa na hatia, hasa kwa kuzingatia ushahidi,” alisema.

“Ninakusudia kupinga mashtaka kwa sababu mimi sina hatia kabisa na sitaki kupoteza mapambano yangu ya kuifanya Italia iwe huru na ya haki
kweli.”

Wakati wa kesi, mahakama iliwasikia dazeni kwa dazeni ya wasichana, akiwemo Bi El Mahroug, ambaye wakati wa tukio alikuwa na umri wa miaka 17 tu, ambapo walilipwa kwa fedha taslimu, malipo mengine na hata magari ili kushiriki kwenye tafrija za ngono za Berlusconi na hata kucheza mbele yake wakiwa nusu uchi.

Vilevile, Berlusconi pia alikutwa na hatia ya kutumia madaraka yake vibaya kwa kumsaidia Bi El Mahrough, ambaye sasa ana umri wa miaka 17, kuachiwa kutoka mahabusu alipokamatwa kwa kushukiwa kwa wizi.

Upande wake wa utetezi ulidai kwamba yeye aliamini kwamba mcheza muziki huyo alikuwa mpwa wa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak na kwamba alikuwa akijaribu kuepuka tatizo la kidiplomasia.

Wakili wake, Niccolo Ghedini, alithibitisha kwamba watakata rufaa, huku akiielezea hukumu hiyo kama “ilisiyoendana na hali halisi” na “isiyo na mantiki hata chembe”.

“Tazama, majaji wamekwenda mbali zaidi ya kile walichoomba waendesha mashtaka, hukumu ya miaka sita,” alisema.

Kila mara Berlusconi amesisitiza kwamba alikuwa akikandamizwa na majaji kwa sababu za kisiasa.

Hata hivyo, mchakato wa rufaa unaweza kuchukua miaka mingi kabla haujakamilika, kwa sheria za Italia.

Mwezi Oktoba uliopita, Berlusconi alihukumiwa miaka minne jela kwa kosa la kuepa kodi kuhusiana na vituo vyake vya televisheni.

Kesi hiyo kwa sasa inasikilizwa katika mahakama ya juu kabisa na ya mwisho kwa rufani, baada ya upande wake wa utetezi kushindwa kukwamisha
hukumu hiyo katika mahakama ya kikatiba.

Chanzo: http://uk.news.yahoo.com/silvio-berlusconi-found-guilty-sex-trial-152906400.html#4BnSKXg

Naam. Kama hukumu za namna hii zingetiliwa mkazo nchini Tanzania, sijui ni nani angepona, maana mmm! matumizi mabaya ya ofisi, ndoa zinazohusisha mabinti chini ya umri wa miaka 18, ma-shuga dadi na ma-shuga mami. Kazi kwelikweli.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: