simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Obama … Wakomunisti Wamshambulia Afrika ya Kusini

with one comment

Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mmoja wa binti zake.

Rais Barack Obama wa Marekani akiwa na mmoja wa binti zake.

Safari ya Obama Afrika ni ya Upande Mmoja: Wakomunisti

Pretoria – Wale waliotaraji kwamba kipindi cha utawala wa Rais wa Marekani Barack Obama kingekuwa tofauti, wanajihisi kuangushwa, katibu mkuu wa chama cha Young Communist League (YCL) Buti Manamela alisema siku ya Ijumaa.

Safari ya Obama katika mataifa matatu, iliyoanzia Senegali, Afrika ya Kusini na inayotarajiwa kumalizika Tanzania, ni ya upande mmoja, nao ni kwa maslahi ya Marekani, alisema Manamela.

“Kusema ukweli, Obama yupo hapa kwa ajali ya kujenga uhusiano wa kibishara, si kwa manufaa ya bara hili, lakini kwa manufaa ya ubepari mkongwe wa Marekani. Manufaa kwa makampuni ya Amerika kuendelea kuvuna ralimali zetu za madini.”

Manamela na maofisa wengine waliwaongoza wanaharakati elfu moja katika maandamano kuelekea katika Ubalozi wa Marekani huko Arcadia, Pretoria.

“Tupo hapa ili kuonyesha hasira yetu na kukasirishwa kwetu na uhusiano unaoendeleza mabavu ya Marekani, sio tu katika uchumi, bali hata katika nyanja za siasa vilevile,” alisema.

“Tulitaraji kwamba kwa kuchaguliwa kwake, mambo hayo yangepungua.”

Dunia litaraji kwamba angeondoa majeshi kutoka Afghanistan, angewaruhusu Waafrika kutafuta suluhu zao kwa matatizo yao wenyewe, angefungilia mbali mahabusu yenye ulinzi mkali ya Guantanamo Bay.

Manamela alisema matarajio hayo yabebaki kuwa ndoto tu.

Obama aliamua kutembelea Afrika kwa sababu Marekani ilihisi kutishwa na kuzidi kujipenyeza kwa China katika soko kubwa la Afrika, alisema Manamela.

“Wao [Wamarekani] wanaona kwamba China tayari iko hapa. Ni kwa sababu ya kitisho hicho cha Uchina kwamba Marekani nayo imekuja hapa. Jambo hili zima [safari] limepata msukumo kutokana na ukweli kwamba uchumi wa Afrika unakua,” alisema.

“Ni udanganyifu kwa Wamarekani kuifanya safari hii ionekane kana kwamba ni kwa manufaa ya bara hili wakati ambapo kwa kweli ni sehemu ya vita yao dhidi ya China.”

Baada ya waandamanaji hao kufika hadi kwenye ubalozi huo, kikundi cha wanaharakati Waislamu kilifanya ibada. Kikundi hicho (kilichokuwa na watu wachache) kilisogea hadi mbele ya ofisi za ubalozi, ambapo mablanketi na vipande vya kapeti vilitandikwa karibu na eneo lenye mfumo wa kutolea hotuba. Mtu mmoja alizungumza na waumini hao waliokuwa wakisujudu.

“Tukimzungumzia Obama, yeye si alama ya demokrasia. Tumeona kuongezeka kwa mauaji ya watu. Hebu tazama Afghanistan, Irak na nchi nyingine,” alisema.

Waandamanaji

Waandamanaji wengine, wakivalia mavazi ya YCL, walishuhudia kikundi hicho wa Waislamu wakisujudu na kushiriki ibada.

Kulikuwa na maofisa kadhaa waliosimama karibu na lango la kuingilia ofisi za ubalozi. Kulikuwa na zaidi ya magari ya polisi 20, likiwemo Nyala, nje ya ubalozi.

Waandamanaji walichoma moto bendera ya Marekani karibu na lango hilo.

Baadhi ya mabango waliyokuwa wamebeba waandamanaji yalisomeka: “Obama, acha kuunga mkono madikteta barani Afrika. Hakuna mafuta hapa, nenda zako”; “Miaka 100 ya mauaji ya kimbari huko Irak. Vita katika mataifa 100. Dola la Kihuni.”

Bango la mwandamanaji mmoja mvulana lilisomeka: “Hapan, huwezi kunipeleleza”. Bango lingine lilisomeka: “USA = Under Satanic Administration, yaani ‘Marekani = Chini ya Utawala wa Kishetani”.

Bango kubwa lilibeba picha ya uso wa Obama na maneno: “Huyu ndiye mwuwaji nambari moja duniani”.

Bango hilo lilimwonyesha Obama akiwa katika chumba cha gereza.

Waandishi wengi wa habari wa nchini Afrika ya Kusini na wa Kimataifa, ambao walikuwa wamepiga kambi nje ya Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic, ambamo Rais wa zamani Nelson Mandela anatibiwa, walikimbia kwenda kuchukua habari za maandamano.

Wakati watu walipopita karibu na hospitali hiyo, walipaaza sauti ili kufikisha salamu zao za upendo na kumtakia faraja mwanaharakati huyo aliye ishara madhubuti ya kupinga siasa za ubaguzi wa rangi.

Chanzo: http://www.news24.com/SouthAfrica/News/Obamas-African-trip-one-sided-YCL-20130628

Ndio.

Katika kipindi hiki ambapo Dar es Salaam na Watanzania kwa ujumla tumeshikwa na ‘homa ya Obama’, ni muhimu kugeuza shingo, kufungua masikio na kusikiliza nini wengine wanasema kuhusu kiongozi huyu wa dola kuu la Marekani. Na, kwa ujumla mawazo yao hatuwezi kuyachukua kiurahisi, ni lazima tuyabebe kwa uzito unaostahili. Tuyapime, tuyachekeche na tujitathmini sisi kama Taifa na wapi tulipo, tunakokwenda na namna gani tunataka kufika huko.

Pamoja sana.

Advertisements

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. WAKOMUNISTI wa Afrika kusini wana hoja kuhusu ujio wa Mhe Rais Barack Obama! Aliahidi kufunga Guantanamo, bado. Vita Afganistani havijamalizika na kweli wangependa kushiriki katika kufaidi mali za Afrika kama Wachina wanavyofanya. Mimi nafikiri kamai anataka mahusiano ya kidhati angeanzisha uwekezaji wa uwazi na ushirikishwaji. Lakini tuelewe pia kuwa siasa za Marekani zinatawaliwa kwa kiasi kikubwa na ushawishi wa wenye pesa![financial lobbying]
  Kuhusu ushoga mimi nampinga kwa nguvu zote. Hata hivyo najiuliza, je kukua kwa ushoga hakuandamani na mabadiliko ya maisha kutoka vijijini kuingia mijini? Au kunaathiria mabadiliko (evolution) ya binadamu kutoka uzaaji wa kingono [sexual reproduction] kuingia uzazi usio wa kingono[assexual-reproduction/, vegetative-reproduction/cloning]? Shuhudia kasi ya sayansi katika uwanja huu na sasa ‘ kukubalika’ kwa utunzwaji/uleaji wa watoto wachanga na “walezi” wa jinsia moja wanawake na wanaume ambao si “wazazi” !
  Hata hivyo nampongeza Mhe Obama kwa kujitahidi kwake kulimudu dola hilo hasa tukikukmbuka ni rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Kiafrika!!
  Canute Temu

  Like

  Canute Temu

  June 30, 2013 at 8:56 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: