simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ajali … Kinyerezi

with 2 comments

Ni ya uso kwa uso … Hiace na Lorry

Viti vya kwenye Hiace … viliparaganyika na vingine kung’oka

Mparaganyiko wa viti kwenye daladala …

Barabara ilifungwa kwa muda … kisha magari yalianza kupita upande mmoja wa barabara kwa kusubiriana

Ni majira ya saa 2 usiku. Wakati ninawasili eneo la tukio, kiasi cha kama dakika kumi zilikwishapita. Ni basi dogo, Hiace, na lorry la kama tani tatu yaliyohusika na ajali hii. Magari haya kwa yanavyoonekana, yaligongana uso kwa uso. Baada ya kutazama, inaelekea kwamba dereva wa lorry ndiye aliyehama kutoka upande wake wa barabara na hatimaye kugongana na daladala hilo. Baadhi ya abiria waliokuwa kwenye daladala hilo bado wapo. Wengine bado wana mshtuko wa kuhusika kwenye ajali. Wananieleza kwamba walioumia hasa ni madereva wote wawili wa magari hayo. Madereva hao hawapo hapo lakini wamekwishatoka, hakuna aliyejua hasa wako wapi. Lorry lilikuwa likiteremka kwenye kilima kutoka upande wa Kinyerezi na Haice ilikuwa ikipanda kilima hicho kutoka Njia Panda Segerea.

Ajali. Barabara ni nyembamba na ina miteremko mikali kidogo na madaraja daraja. Ingawa hakuna aliyepoteza maisha katika tukio hili, lakini mtu unapata maswali mengi. Linaloumiza kichwa zaidi ni kuhusu umahiri wa madereva wetu hapa nchini. Ajali zilizo nyingi zinasababishwa na uzembe wa madereva. Mtu unajiuliza, hivi hizi leseni zilizo mikononi mwa madereva … wanazistahili kweli? Je, vigezo vyote na masharti yalizingatiwa kabla ya kuwapa leseni hizo? Je, polisi wa usalama barabarani wanafanya kazi yao kikamilifu … au ndiyo baadhi wanawalinda wahalifu wa makosa ya barabarani baada ya kulambishwa shilingi mbili tatu?

Tupige vita ajali. Tunaweza kuwa na barabara zilizo salama katika nchi yetu. Kila mmoja atimize wajibu wake vizuri. Pamoja sana!

Written by simbadeo

September 18, 2012 at 10:48 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. tuwe waangalifu tunapokuwa barabarani…kikubwa zaidi ni high speed lakini kama tunaendesha kutokana na speed inavyopangwa na vyombo vya sheria ,basi ajali inaweza kuhepukika,,,

    Like

    RAPHAEL CHAMBO

    September 18, 2012 at 10:59 pm

    • Ndugu Raphael, asante kwa maoni yako. Kwa ujumla, hatuna budi kuketi chini na kujifunza ustaarabu wa kuendesha vyombo vya moto. Ajali zilizo nyingi zinasababishwa na uzembe … na kisha watu husingizia ‘bahati mbaya’. Yatupasa tufike mahali tuseme basi. Utaona mtu anakwenda speed kali, ukimwuliza anachokimbilia … hana! Safari ni ndefu. Asante sana.

      Like

      simbadeo

      September 18, 2012 at 11:08 pm


Leave a comment