simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for August 2012

Wikiendi … Pumzisha Akili na Mwili

with one comment


Ndiyo. Kama binadamu tunahitaji kupata mapumziko ili kupata nguvu za kusonga mbele kwa namna yenye tija zaidi. Moja ya maeneo ambayo yanasaidia sana kupunguza stress za wiki nzima ni kandokando ya bahari au kutembea katika mazingira yanayokuburudisha kwa namna moja au nyingine. Bahari huipa akilia uwezekano usio na kikomo. Mandhari ya misitu na milima milima nayo hufanya vivyo hivyo. Kila baada ya muda fulani … Acha shughuli zako za kila siku … Nenda kule ambako utapata uhai mpya. Mazingira yatakayochochea akili yako kufanya kazi kwa viwango vya juu zaidi. Wikiendi njema kwa kila mmoja!

Written by simbadeo

August 31, 2012 at 11:27 pm

UDSM … Kinachakaa, sad

leave a comment »


Nilitembelea makazi ya wakufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam karibu na Gate Maji. Kila unapotupa jicho … unakutana na uchakavu. Kisha huoni kama kuna juhudi zozote za makusudi ya kurekebisha hali ya mambo. Ukiwa na moyo mwepesi unaweza kupata mshtuko mkubwa. Unajiuliza … Inakuwaje hadi taasisi nyeti kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam inafikia hatua hii? Kwa nini barabara ziruhusiwe kuingia katika hali mbaya kiasi hiki? Vivyo hivyo kwa miundo mbinu, hasa mifumo ya maji taka. Kwa nini? Je, hakuna fedha zinazotengwa kwa ajili ya kukarabati miundo mbinu? Na hapo nimeona just 1% ya chuo. Suppose tukipita kila mahali, kila Kitivo, kila Idara, kila Unit … kuna madudu gani?

Hivi, chuo hiki mama wa vyuo vikuu vingine hapa nchini na hata katika nchi jirani … hakina members wa Alumni? Maana naamini kundi hilo wala si haba hata kidogo. Hata wao wanaweza kuchukua hatua na kujaribu kunusuru aibu hii!

Je, hii ndiyo taswira ya Taifa kwa ujumla? Kwamba kila kitu kinaparaganyika? Kila kitu kinarudi nyuma? Tafakari.

Written by simbadeo

August 30, 2012 at 10:07 am

Kitabu Kipya … Asili Halisi ya Mwanadamu

with 4 comments


Asili ya Bin-Adam kama kilivyoandikwa na Maalim Juma Kinyemi …

Mama Bahati Jonathan Mbwambo, mke wa mwandishi, akionyesha moja ya nakala za kitabu hicho

Mwandishi anasema hivi juu ya kazi yake hii:
“Madhumuni ya Historia hii siyo malumbano, tuhuma wala masahihisho, ila ni kuweka mwelekeo ulio wa kweli katika hali ya dunia na matendo ya binadamu. Kwa wale ambao watajaliwa kupitia maelezo ya kitabu hiki, watagundua kwamba nia yangu ni kutoa mwangaza kwa binadamu wote wanaokusudia kuupata mwangaza huu popote pale duniani bila kujali imani yao ya dini.” Maalim Juma Kinyemi.

Msomaji Athmani Iddi Millanzi alipata kusema haya alipopata bahati ya kusoma muswada katika hatua zake za mwanzo:

“Nilipomaliza kusoma rasimu hiyo, kabla ya kuonana na mwandishi wa kitabu, sina budi nikiri kuwa nilikuwa na mawazo ya kwamba mwandishi wa kitabu hiki lazima angekuwa msomi wa hali ya juu sana mwenye elimu isiyo chini ya shahada. Kutokana na mambo yaliyomo ndani ya kitabu hiki kuwa:
1. Ya ajabu kwani yalikuwa ambayo nadhani siyo kwangu tu bali bali kwa yeyote atakayesoma, hayapo kabisa kwenye kitabu au andiko lolote ambalo tayari limechapishwa.
2. Linamhusu kila binadamu wa kale na wa leo kwa vile yanazungumzia Historia ya ‘Adam na Hawa’ wanaokubalika duniani kuwa ndiyo chanzo cha binadamu yeyote ambaye alikuwapo au yupo bila kujali ni wa dini gani, kabila gani, itikadi gani au kutoka pande gani katika dunia hii ya Mungu.”

Ili kujipatia nakala yako kwa Sh15,000 tu andika barua pepe kwa anwani hii: fgdtanzania@gmail.com au P.O. Box 40331, Dar es Salaam, Tanzania.

Tukikaribishe kitabu hiki kwa mikono miwili. Kinaongeza idadi ya vitabu bora vinavyoendelea kuchapishwa nchini Tanzania, yote ni kwa manufaa ya binadamu wa sasa na wa kizazi kijacho. Pamoja sana.

Written by simbadeo

August 27, 2012 at 8:12 am

Sensa ya Watu na Makazi … Ni Leo

with one comment


Hapa ni Tandika, Uwanja wa Mabatini …

Moja ya maswali litakuwa kuhusu mifugo tunayofuga. Taswira hii ilichukuliwa kwenye daladala hivi karibuni.

Ile Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi inaanza leo. Wewe, mimi na yule sote tunawajibika kushiriki kwa maendeleo ya Taifa letu. Anayejenga Taifa ni mwananchi mwenyewe. Mwananchi wa Taifa la Tanzania si mwingine bali ni WEWE na MIMI. Sisi ndiyo tunaoijenga Tanzania. Sisi ndiyo tunaojenga hatma ya vizazi vya Watanzania. Tunaposhiriki kwenye zoezi hili la sensa tunashiriki katika kupanga maendeleo ya Taifa letu. Pamoja sana.

Written by simbadeo

August 26, 2012 at 12:30 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , , , , , ,

Product Launch … Uzinduzi wa Bidhaa … apple drink

leave a comment »


Jukwaa la uzinduzi …

Burudani …

Manjonjo …

Mdau …

Ni katika pitapita zangu leo pale Mlimani City jijini Dar es Salaam. Nilikutana na tukio hilo la uzinduzi wa bidhaa za vinywaji vya Apple na Pineapple. Ilikuwa burudani ya kutosha kabisa kusafisha akili mwishoni mwa juma. Na hizo ni baadhi ya taswira nilizochukua kwa muda mfupi niliokuwa pale. Ilikuwa bomba sana … na kinywaji chenyewe pia ni bomba sana … kwa jinsi nilivyokionja.

Kwa jicho la pembeni:

– Ubepari umetugubika hivi sasa. Suala ni kuona namna gani ubepari huu tunaumudu ili kwamba usitupelekeshe kombo. Hapa nazungumzia suala zima la kujali utu wa mtu na heshima ya binadamu (Staha, heshima yake, haki zake n.k.)

– Je, bidhaa hizi zitatoa fursa kwa wakulima wetu waliopo kule Lushoto, Matombo na kwingineko matunda yanapostawi kupata bei bora zaidi na hivyo kuinua kipato chao? Ni matumaini yangu tu kwamba malighafi za bidhaa hizi zitatoka humu humu nchini na si kuagizwa kutoka nje. Ni muhimu tule vile vinavyozalishwa hapa nchini ili kukuza uchumi wetu na nguvu yetu ya kununua na kuuza.

Pamoja sana.

Written by simbadeo

August 26, 2012 at 12:22 am

Giraffe Ocean View … Pumzisha Akili

with one comment


Mapokezi poa kabisa … Kazi ya sanaa.

Kutokea upande wa baharini … jioni. Inawezekana … Kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi katika Tanzania.

Written by simbadeo

August 24, 2012 at 11:19 pm

Reli … na Kujikimu

leave a comment »


Katumba …

Ugala …

Mpanda …

Hata kama wanajikimu kwa njia hizi, bado wanastahili kuwezeshwa ili wapate njia bora zaidi. Tanzania haiwezi kuendelea kwa kutegemea ajira za aina hii. Wananchi wawezeshwe ili kufanya biashara zenye tija zaidi kwao binafsi na kwa Taifa kwa ujumla. Mipango bora inawezekana. Shiriki Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi kikamilifu ili kufanikisha upatikanaji wa tawimu muhimu kwa mipango madhubuti ya maendeleo. Utashi na utayari wa mambo ni muhimu sana. Pamoja sana!

Written by simbadeo

August 23, 2012 at 10:39 pm

Posted in Siasa na jamii

Mazingira … Usipoyatunza

leave a comment »


Mazingira, tusipoyatunza tunafanana na yule aliyeketi kwenye tawi la mti kisha akaanza kulikata tawi hilo. Hata alipoonywa kwamba kitendo hicho kilikuwa hatari kwake, yeye aling’ang’ania. Matokeo yake ni kuwa alianguka na tawi hilo. Pamoja na hayo, hakuishia hapo kwenye ujinga wake. Alimsihi yule aliyemwonya kuwa amtabirie na siku yake ya kufa. Lo. Ni muhimu tutunze mazingira, kwani bila mazingira endelevu, maisha na ubinadamu vitafikia ukomo mara moja. Kwa nini watu wachome misitu ovyo? Kwa nini katika nchi ambapo gesi imevumbuliwa kwa kiasi kikubwa bado tuendelee kutumia kuni kama chanzo cha nishati? Tubadilike.

Written by simbadeo

August 22, 2012 at 11:42 pm

Posted in Siasa na jamii

Tunatoka … Kusoma

leave a comment »


Tunatoka shule. Hamu ya kusoma ingalipo bado. Kiu cha elimu hakikatiki. Wazazi nipeni vitabu. Nataka kusoma. Nataka kupata maarifa. Nataka kukuza akili yangu na uwezo wangu wa kuelewa. Niwekeeni vitabu nyumbani. Niwekeeni vitabu shuleni. Niwekeeni vitabu maktaba. Niwekeeni vitabu katika sehemu za michezo. Mtaona nitakavyofanya vizuri zaidi katika masomo yangu na katika maisha yangu ya kila siku. Elimu. Vitabu. Maarifa. Kukua.

Written by simbadeo

August 21, 2012 at 10:32 pm

Posted in Siasa na jamii

Kilimo Kwanza … Ratiba

leave a comment »


Haya shime wakulima. Baada ya kusherehekea Sikukuu ya Nane Nane, ni wakati wa kuanza kuandaa mashamba. Ratiba yetu iko wazi hapo juu. Sisi ndiyo wa kulijenga Taifa hili. Tukizingatia ratiba hii kikamilifu … mafanikio tutayaona. Kwa wale wa umri wangu bila shaka mnakumbuka shairi lile: Karudi baba mmoja na kutetemeka mwili … Kama mnataka mali, mtayapata shambani!

Written by simbadeo

August 21, 2012 at 10:28 pm

Posted in Siasa na jamii