simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for September 24th, 2012

Ya Livepool na Man U … Tunaelekea kwenye Dini ya Soka?

leave a comment »


Haya tena. Liverpool wamelala kwa Man U. Matokeo hadi mwisho wa mchezo uliopigwa kule Anfield ni Liverpool 1, Man U 2. Hiyo, ni licha ya Man U kucheza wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja. Kwa hiyo, mashabiki wa Man U waliendelea kupata raha.

Ila, kila nikiangalia mwenendo wa soka duniani … naona tunaanza kuingia kwenye ‘dini’ mpya. Soka hivi sasa inavuta watu wa kila aina, tabaka, rangi, kabila, hadhi ya kiuchumi, rika tofauti … watu wanajaa kwelikweli kwenye mabaa na maeneo mengine mechi zinakoonyeshwa. Je, tunaelekea kwenye ‘dini’ za soka … na hivi vilabu ndiyo ‘madhehebu’? Nadhani bado kidogo tu tuaanza kuona vikapu vya sadaka vikitembezwa na michango kudaiwa.

Itafika mahali kama huna timu (hasa ya Ulaya) unayoishabikia utakosa marafiki, maana hutakuwa na kitu cha kuzungumza na wenzako!

Aaah! Pengine ni wakati tujitafakari kuhusu nini ni muhimu katika maisha na kipi ni cha kupitisha muda tu!

Pamoja sana. Pongezi wana Manchester United!

Written by simbadeo

September 24, 2012 at 1:36 am

Riziki kwa Mungu … Au Mikononi Mwako?

leave a comment »


Kwa waliopata ni rahisi kusema kwa Riziki inatoka kwa Mungu. Ila kiukweli kabisa … chacharika, tumia akili yako, fanya kazi kwa bidii, uwe mbunifu na hakika riziki hiyo utaipata. Ukilala nyumbani au ukiamua kuzembea na kutotumia talanta ulizopewa, kwa hakika hutaiona hiyo riziki. Jitume, jibidishe, fanya kazi kwa juhudi na maarifa … utafanikiwa.

Ila … duh … Ni muhimu kuondokana na ajira za aina hii. Taifa haliweze kuendelea kama tunapoteza nguvu kazi muhimu kama hawa mabwana kwenye kazi hizi. Tufanye kazi kwa juhudi na maarifa … lakini kwa kazi ambazo zina tija kwa Taifa. Usafi sawa, lakini si kuna sehemu zake … sio humu barabarani.

Pamoja sana.

Written by simbadeo

September 24, 2012 at 1:27 am

Posted in Siasa na jamii