simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for September 5th, 2012

Postal Services … Changing with the Tide

leave a comment »


Huduma za posta zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na mabadiliko yanayotokea katika teknolojia ya mawasiliano. Jiulize, hivi ni lini mara ya mwisho ulikwenda posta ili kutazama kama umetumiwa barua au la? Bila shaka wengine wana miezi mingi. Je, kiasi cha barua zinazoingia kwenye masanduku hayo bado ni kama ilivyokuwa miaka kumi iliyopita au kuna mabadiliko — kimepanda au kushuka? Ni wazi, jibu hilo la pili ndiyo sahihi.

Watu wengi hivi sasa wanawasiliana kwa barua-pepe na simu za mkononi. Biashara ya posta imebaki kwa idadi ndogo ya barua, pengine na vifurushi. Ingawa hata kwenye biashara ya vifurushi kuna ushindani mkubwa. Kuna makampuni ya mabasi na makampuni ya usafirishaji mizigo yanayoshindania vifurushi hivyohivyo. Huduma za kibenki … okay … huku nako ushindani unakua.

Changamoto ni nyingi. Hata hivyo, kwa aina ya miundombinu na mtandao ilio nao Shirika la Posta, wana fursa nyingi za kuendelea kujiendesha kibiashara iwapo wataongeza ubunifu, wataongeza aina mpya za huduma za kisasa (kama pichani hapo juu), na kwa hiyo kufanya mambo makubwa zaidi. Ubunifu ndiyo neno la msingi katika yote haya. Kwa nini mathalani ofisi za posta zisijishughulishe na kuuza vitabu na magazeti. Kwa kutumia mtandao huohuo wana uwezo wa kuuza si chini ya nakala 50,000 kwa siku za vitabu. Hata kama wao watapata faida ya sh100 kwenye kila nakala, je, ni kiasi gani hicho cha fedha jumla kwa siku?

Ni muhimu wajipange na kujituma zaidi. Wale watumishi wasio waaminifu wanaofungua vifurushi na mizigo ya wateja, wasakwe na kushughulikiwa ipasavyo kwa mujibu wa sheria. Hatua hiyo itarudisha imani ya wananchi kwa shirika hilo na kwa hiyo nalo litafanya biashara zaidi.

Nawasilisha.

Written by simbadeo

September 5, 2012 at 9:22 am

R.I.P. Daud Mwangosi … Mpiganaji

leave a comment »


Daud, enzi za uhai wake.

Dr W. Slaa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Mbeya, Daud Mwangosi. Inaelezwa kwamba Daudi aliuwawa akiwa mikononi mwa polisi na kitu kinachoaminika kuwa bomu la machozi.

Picha kutoka swahilitimes.blogspot.com na mjengwa.blogspot.com

Pole nyingi kwa familia, hasa mke na watoto, na vilevile kwa wanahabari wote nchini, Channel Ten TV Station na Watanzania kwa ujumla. Tukio hili limeiacha jamii nzima imepigwa na bumbuwazi.

Wito: Haki itendeke. Umma unafahamu nini kilitokea na kwa hiyo haki itendeke.
Waliobaki waendeleze jahazi kwa juhudi, umakini na uadilifu zaidi sana.

Written by simbadeo

September 5, 2012 at 9:08 am