simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for October 2012

Eid Mubarak … na Ushauri Murua wa Mzee Buffet

leave a comment »


Nimetumiwa ushauri huu. Nami katika kuwatakia Sikukuu Njema ya Idd, ninawawekeeni hapa. Huenda mtu ukaokota moja au mawili ya kukuongoza kuelekea kwenye mafanikio. Inawezekana umekuwa ukifuata kanuni hizi, kwa kuzisoma hapa, utakuwa ukiimarisha imani yako kwazo. Au siyo?

Eid Al Haj njema kwa kila mmoja anayesoma hapa na familia zenu.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

October 26, 2012 at 9:45 am

Smile … Tabasamu

with one comment


Begin your new day with a smile. It’s healthy. It helps your mind to stay focused and creative. Try it every morning. Do it every day.

Anza siku yako mpya kwa tabasamu. Ni jambo jema kwa afya. Kitendo hicho kinakuongezea umakini na kujawa na ubunifu. Jaribu kila asubuhi. Fanya hivyo kila siku.

Pamoja sana.

Above images are of my very dear friends. Picha hizi ni za marafiki zangu wa karibu sana.

Written by simbadeo

October 23, 2012 at 9:55 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with ,

Ufugaji Kuku … Sanaa ya Uuzaji

leave a comment »


Unapokamilisha kuwafuga kuku, na sawa wamefikia umri wa kuuzwa, unaingia katika kutafuta masoko. Je, wadau, mtu afanye nini ili utafutaje wake wa masoko uwe wa mafanikio? Bila shaka sote tunaelewa kwamba katika uzalishaji bidhaa, ni muhimu kuwa na mzunguko wa biashara unaotiririka vema ili kukuza biashara hiyo. Tupeane mbinu katika ulimwengu huu wa ufugaji kuku na usambazaji wake.

Karibuni.

Written by simbadeo

October 21, 2012 at 11:07 pm

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , ,

Amani Tanzania … Penye Miti Hakuna Wajenzi

with 4 comments


Hali ya mambo imekuwa si shwari katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, hasa mitandao ya kijamii, kuna kikundi kiliamua kufanya maandamano yasiyo rasmi ili kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Ponda. Polisi wa kuzuia ghasia na askari jeshi walimwagwa mitaani ili kudhibiti hali ya mambo.

Ama kwa hakika, tunaona upepo ukigeuka hapa nchini. Katika siku za karibuni tumeshuhudia kuongezeka kwa vurugu za kila aina. Ukitafuta kiini hasa cha machafuko hayo mtu hukioni.

Mathalani, katika picha hiyo ya tatu hapo juu, kuna jambo lililonigusa sana. Kuna huyo mwanafunzi (msichana) anayejaribu kuvuka barabara. Hebu wewe uliyedhamiria kuanzisha vurugu, je,uliwafikiria watoto hawa? Uliwaza kuhusu wazee, wenye ulemavu, maendeleo ya nchi kwa ujumla? Pengine huwezi kumfikiria mtoto huyu kwa sababu wewe si mzazi (maana wahenga wanasema, uchungu wa mwana aujuaye mzazi), lakini bado unaweza kuwa kaka, mjomba, binamu au basi jirani yake. Je, kabla ya kuingia mitaani na kuanzisha vurugu hizo, uliwaza ni namna gani mtoto huyu atatoka shuleni kwake, atafute usafiri na kurejea nyumbani kwao salama? Je, nini hasa kilikusukuma kuona usalama wa mtoto huyu ni kitu kidogo sana kuliko hicho unachokipigania?

Maswali ni mengi. Ila hakuna sababu hata moja inayoingia akilini kuhalalisha taharuki, mateso, hofu, mashaka na wasiwasi mkubwa anaoupata mtoto huyu kwa mazingira hayo ya fujo na vurugu uliyomwekea. Sizungumzii hisia za mzazi, maana pengine wewe uliyeamua kuanzisha fujo una chuki na watu wazima wote — hasa wale ambao hawakubaliani na matakwa yako.

Tanzania imekuwa chemichemi ya amani kwa miaka mingi sana. Amani hii ni lulu. Amani hii ina thamani kubwa sana kuliko utashi wako wewe mtu mmoja unayelala usiku ukiwaza ni namna gani uanzishe fujo. Hebu nikuase, hii ni nchi yenye miti (amani), wajenzi tupo, wewe mmoja usifanye sote tukose maana kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Tudumishe amani Tanzania. Choyo na ubinafsi tuvipige vita. Tupige hatua ya kukua zaidi kidogo na kutafakari athari na masaibu tunayoweza kuwasababishia watu wenzetu kwa sababu tu ya kutaka kutimiza tamaa yetu … pengine kujipatia umaarufu kwa njia zilizo rahisi.

Mwenyenzi Mungu, Mwingi wa Rehema tupe uvumilivu, tujaalie hekima na uwezo wa kuzishinda tamaa zetu. Amina.

Picha zote ni kutoka Wavuti.

Written by simbadeo

October 19, 2012 at 4:41 pm

Lyamba la Mfipa Village Hotel … Mpanda

with 4 comments


Unapoingia … unakutana na jengo hili

Cottages za hoteli hiyo …

Alama ya kuelekeza hotelini iliyo kando ya ukuta unaoizunguka …

Sikupata muda mrefu wa kuketi hapo na kufurahia huduma zao. Lakini ni matumaini yangu kwamba mwonekano na huduma vitakuwa vinashabihiana.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

October 19, 2012 at 1:42 am

Posted in Siasa na jamii

Natural Resources … Ugalla River Valley

leave a comment »


Ni sehemu ya bonde la Mto Ugalla mkoani Katavi. Tanzania ina mabonde kama haya mengi sana. Swali langu ni moja, kwa nini nchi hii isigeuke na kuwa ghala la chakula kwa ulimwengu mzima? Tunashindwa nini? Au ndiyo vijana wote wamekimbilia mijini kwenda kufanya biashara ya kusafirisha abiria kwa bodaboda na kuuza bidhaa cheap na nyingine feki za kutoka China mitaani? Wahenga walisema, penye miti hakuna wajenzi!

Written by simbadeo

October 19, 2012 at 1:23 am

Digital Divide … Filling the gap

with 3 comments


Kwa takwimu zilizopo, ni kaya chini ya asilimia 20 tu ndiyo zilizounganishwa kwenye mitandao ya umeme unaozalishwa hapa nchini. Katika zama hizi za teknolojia na matumizi ya vifaa vinavyohitaji umeme, asilimia hiyo zaidi ya 80 imeachwa nyuma. Hata hivyo, watu hujitahidi kivyao kutokuachwa nyuma sana … ingawa hawana budi kuingia gharama zaidi. Njia moja wanayotumia ni kwenda kwenye maeneo ya kuchajisha simu. Kwa hiyo, unaweza kuishi nyumba isiyounganishwa na umeme, lakini bado ukamiliki simu na ukaiwekea umeme kwa kwenda kwenye sehemu zinazotoa huduma hizo.

Picha hiyo ni katika moja ya sehemu zinazotoa huduma hiyo katika mji wa Mpanda. Ni karibu kabisa na soko kuu.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

October 18, 2012 at 9:51 am

Unapokua … Nao wanakua

leave a comment »


Anaitwa Martin.

Akiwa na wahitimu wenzake wa Darasa la Saba katika Shule ya Macedonia pamoja na baadhi ya walimu wao.

Akifuatilia yanayojiri …

Moja ya onyesho la jaribio la kisayansi lililofanywa na wanafunzi shuleni hapo.

Anaitwa Cecilia … akitiririka na ubeti wa ngonjera wakati wa shughuli hiyo ya kuwaaga Darasa la Saba shuleni hapo…

Digidigi wa shuleni hapo nao wakifuatilia yanayojiri … Huyo wa pili anaitwa Martina na anayemfuatia anaitwa Alice.

Martin (katikati), Cecilia (kulia) wakiwa na rafiki ya mama yao. (Mama yao alikuwa busy akipiga picha hizi na nyinginezo).

Pamoja sana … Wewe unapozeeka, wao nao wanakuwa. Maisha … sijui ni sawa na mchezo wa kukabidhiana vijiti?

Picha zote na Bibiana Msuya.

Written by simbadeo

October 14, 2012 at 5:21 pm

Posted in Siasa na jamii

Dar es Salaam … Katika Taswira

with one comment


Mitaa ya Amana …

Kutumia muda vizuri mtu unapokuwa kwenye usafiri wa umma … quality time

Kwenye viambaza katikati ya jiji …

Mnara wa Saa …

Mwalimu akielekea kazini … Kujenga Taifa la leo na kesho

Vijana kibao wakiuza bidhaa zinazofanana fanana … nani anauza, nani anatoka kapa? Je, mtu akitoka kapa wiki nzima mfululizo anafanya nini ili kufanya wategemezi wake waendelee na maisha? Tujitafakari kama Taifa na mustakabali wetu …

Karume … Kila mmoja na hamsini zake

Polisi wa usalama barabarani kazini … ni kamatakamata kwa kwenda mbele. Nilimwuliza kondakta mmoja aliyekuwa anawapigia simu wenzake kuwatahadharisha kuhusu kazi waliyokuwa wakifanya askari hawa pale Tazara kuwa badala ya kuendesha biashara kiujanjaujanja kwa nini wasisahihishe makosa? Alinijibu kuwa matajiri hawako tayari na pili polisi trafiki akikukamata lazima akubabatize hata kosa moja.

Ama kweli, usafiri wa umma Tanzania bado una safari ndefu kabla haujafikia viwango. Kwa sababu ya ubovu huo wa huduma, kila anayedunduliza tusenti twake … atakimbilia kwenye kujichukulia kamtumba kake … matokeo yake barabara zinajaa … foleni zinakuwa za kutesa sana … na kulisababishia Taifa hasara zaidi sana tena sana.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

October 13, 2012 at 12:56 am

African intellectuals … Kazi Kwenu!

with 6 comments


Soma ujumbe huu, utafakari. Nafasi yako ni ipi kama msomi? Mchango wako kitaaluma kwa maendeleo ya nchi ni upi? Unaacha legacy gani kwa Watanzania (ukiachilia mbali majumba na mali kwa wanafamilia wako)? Wewe mwenyewe unajivunia nini katika nafsi yako kuhusu maendeleo ya wanadamu wenzako kwa ujumla wake?

The African Paradox: Plenty “Intellectuals”, Yet No Physical Solutions

Africa, our beloved continent, is currently becoming dominated by a generation of noise makers: a people who can talk, talk and talk almost all the time, yet with no physical action. In fact, it is very annoying when you tune into your radio or television set in the morning and all you can hear are some “experts” giving speeches to the audience, while reserving the real action to some inexperienced folks out there.

There are many scholars with PhDs and master’s degrees in Agricultural Science. Yet many of them will never set foot on the farm. Many of our scientists are probably very good at teaching but never good at inventions and innovations. I have always wondered where our mechanical engineers have been hiding, as we continue to import motorbikes and even bicycles from abroad every year. The taxpayer is often told: “plans are far-advanced for the implementation of this project”; the other project is “in the pipeline”, the implementation phase comes “in 4 years”, and so on. Many of such proposals have always remained a pipedream. Yet every year such slogans are shamefully echoed to the masses.

From the scientific researchers, through the religious leaders, the academicians, our scholars and most annoyingly, the politicians- when in opposition, almost everyone could perfectly demonstrate exactly what ought to be done in any given circumstance; yet once in power, such ideas will always remain either on paper or at best be held “in the pipeline”. Instead of taking action and making things happen in a swift and decisive manner for the benefit of our people, it is rather very sad that even those tasked with such responsibilities are rather good at making speeches, while pushing the actual action onto the future generations.

So far, it appears a few of those in the built environment are physically making impact, whiles the majority of the other professions especially those in the manufacturing fields remain to be seen. Meanwhile the media which ought to bring such topics for discussion has always been focusing on politicians and their frustrations whiles ignoring the lack of action from the professionals groups out there.

From Total Illiteracy to Incompetent Intellectualism Many years ago, there were only a few “scholars” in Africa. At that time, the mass majority of the people had not received “formal education” as we often call it. Many had not been to engineering schools, polytechnics nor the university. There were only a few tens of people who had the benefit of receiving “formal education”.

In spite of this, Africans were producing soaps, shoes, body cream, they were producing different kinds of cooking oil and their local African medicines were very effective and powerful. They cured almost every major disease by relying on their local medication and eating organic food which was very rich in vitamins and nutrients. In fact, they ate good quality food. As a result, many of them lived long, averagely beyond the age of 90 years.

“It was very common to see many of our parents living beyond the age of 120 years with good eyesight.Most importantly, many of our grandparents never wore glasses”.

Ironically, today we call ourselves “intellectuals”, we live in “hygienic environments”, we eat “balanced diet” and use “modern medication”.

“Yet, many of us are dying below age of 40! Today, millions of children at age 10 are wearing glasses”!

As if that is not enough, there are several hundreds of incurable diseases that currently threaten our very survival. What an irony!

How many of our forefathers died of malaria fever? How many of our grandmothers were infertile? In fact, there are many reproductive health-related diseases in our modern Africa than it was in the pre-colonial era despite the so-called advancement in medical research. Isn’t it time we took a critical look at the quality of our food today? But of course, many will consider this to be some “conspiracy theory”. After all, once you successfully discredit legitimate concerns such as the above, it becomes easy to ignore the need to take action.

Currently even though Africa can boast of several millions of scholars, professionals, professors and several others with PhDs, one can always wonder the whereabouts of these experts as almost everything we used in Africa is imported from elsewhere, despite having all the raw materials here at home.

For instance, 40 years ago, Africa was importing a sizeable amount of matches, sugar, cooking oil, roofing sheets, steal, cars, bicycles, shoes, wristwatches, typewriters and others. This was due to the fact that during that time, Africa did not have the needed expertise to mass-produce some of these items here at home. Unfortunately, after 40 years, nothing has changed despite the fact that mother Africa has millions of intellectuals who currently hold the relevant qualifications in the production of these items.

After many years of importing mobile phones, computers, electric generators, sound systems, radio and television sets, fluorescent lamps, electric cables and many other electronic gadgets, there is no indication that this trend will change anytime soon, though there are millions of African experts who have studied the production of these things. Isn’t it a shame that our scholars take pride in their numerous academic qualifications and titles, yet such credentials often do not make any practical contributions to the development of our continent?

Elsewhere in the Middle East and Asia, ordinary students are sending satellites into space. University researcher are actively engaging with their students in the production of mobile phones, digital tablets, computers, cars, and all sorts of physical results can be seen everywhere.

Unfortunately, here in Africa, our studies are characterized by reading theories, looking at diagrams and observing images with little or no practical demonstrations. The educational system, instead of teaching our people “how to think” and solve problems, the system is rather teaching young ones “what to think”. Today, one can write over a thousand pages of research, yet this research may not have a single practical input. Of course one can perfectly describe how to move a car. But it takes continues practise to be able to practically drive the car. Is it a wonder that many of our mechanical engineers therefore cannot even fix a faulty car engine? Our universities are over populated with more than 60% of political and the social sciences. The last time I checked, the technical schools and the polytechnics were still reserved for students with poor academic backgrounds, whiles the brilliant and most intelligent ones were those allowed entry to the universities.

In fact, it is a common phenomenon that many of our real electrical engineers, the mechanics and all the real technicians out there did not learn their profession from schools. Rather many of them were school drop-outs who learnt their profession as a “trade” and by the “road-side technicians”. Therefore when the scholar’s car suffers a mechanical breakdown, the individual will rather look for a road-side mechanic to fix the problem despite him having a degree in the field. To me, the most interesting thing about these local technicians is that, many of them do not have any academic qualifications at all. Yet they’re better at solving real-life problems than many of our so-called professionals who have acquired a number of degrees. Isn’t this a shame? Today our universities are increasingly producing intellectuals who can talk too much but lack the skills to personally contribute to problem-solving.

It is increasingly becoming annoying that many of our intellectuals, who continue to hold themselves as such, can only make noise and give plenty of lectures while pushing their real responsibilities to the man on the street. Such acts of negligence must stop if Africa is determined to make any progress in the near future. African intellectuals must live up to their responsibilities. It is time for our these experts to demonstrate their profession by physically being part of the solution to our many challenges rather than merely dominating the airwaves with empty speeches that often lead to no physical results. It is time to be proactive. We must demonstrate our desire to contribute to problem solving by leading the charge on the battlefield. This is the way forward.

Real leadership is to be demonstrated; not lectured. We’re getting tired of those talks, seminars and the workshops which have become the hallmark of our current batch of intellectuals who ought to bear the responsibility of taking the action. If those tasked with the responsibility to make things happen are rather doing the talks, whose duty will it be to take action? As long as our intellectuals continue to look up to the layman to take up his responsibilities, Africa will never make any meaningful progress. I challenge all African experts, the intellectuals and all those with meaningful qualifications in their various portfolios to make their presence felt as the continent begs for solutions. Our destinies must be in our own hands.

Long live the African intellectual. Long live mama Africa!

Honourable Saka The writer is a Pan-African analyst and a well-known social commentator in Africa. He’s the founder of the Project Pan-Africa (PPA), an organisation that seeks to create a mental revolution across Africa. PPA’s website is available at: http://www.projectpanafrica.org. He is highly grateful to Itech Plus, and all the media which supports his vision for the African people.

Source: http://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/artikel.php?ID=252112

Written by simbadeo

October 8, 2012 at 12:16 am