simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kampeni: Damu Salama kwa Wagonjwa

with 6 comments


Ni katika Viwanja vya Sitakishari Social Club, Ukonga Banana, Dar es Salaam.

Ni katika Viwanja vya Sitakishari Social Club, Ukonga Banana, Dar es Salaam.

Wamejitokeza watu wa karibu rika zote kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Wengi wao wakiwa ni wanachama wa vilabu vya mchakamchaka (jogging clubs).

Wamejitokeza watu wa karibu rika zote kutoka kona mbalimbali za jiji la Dar es Salaam. Wengi wao wakiwa ni wanachama wa vilabu vya mchakamchaka (jogging clubs).

Naam, kulikuwa na upimaji na uchangiaji damu.

Naam, kulikuwa na upimaji na uchangiaji damu.

Walijitokeza wadau mbalimbali ...

Walijitokeza wadau mbalimbali …

Mstahiki Meya wa Ilala, Bw Jerry Silaa, hakuwa nyuma.

Mstahiki Meya wa Ilala, Bw Jerry Silaa, hakuwa nyuma.

Wadau wakisubiri zamu zao kuingia uwanjani kukipiga ...

Wadau wakisubiri zamu zao kuingia uwanjani kukipiga …

Naam. Mshika kibendera yuko makini tayari kuchukua hatua inayostahili wakati mechi mojawapo ikiendelea.

Naam. Mshika kibendera yuko makini tayari kuchukua hatua inayostahili wakati mechi mojawapo ikiendelea.

Wanamasumbwi kutoka Kongowe wakifanya mazoezi hapohapo uwanjani...

Wanamasumbwi kutoka Kongowe wakifanya mazoezi hapohapo uwanjani…

Ni sekeseke karibu na lango ...

Ni sekeseke karibu na lango …

Kwa hakika ni bonanza la aina yake. Kuna burudani kedekede — soka, ndondi, muziki. Kuna vyakula na vinywaji vya kutosha kila mmoja. Ni muhimu kuchangia damu salama ili kunusuru maisha ya wale wanaohitaji kuongezewa damu, hasa akina mama wajawazito na watoto. Jitolee kuchangia damu ili kuokoa maisha. Pima afya yako. Ni leo tarehe 22 Juni, 2014 katika Viwanja vya Sitakishari – Ukonga Banana, jijini Dar es Salaam. Pamoja sana.

Homa ya Kutisha … Dengue … Wakinge Uwapendao

with 2 comments


Sote tujitahidi kuzingatia maelekezo haya. Ni kwa kushirikiana tu ndio tutaishinda homa hii hatari. Jikinge na wakinge wengine dhidi ya Homa ya Dengue. Ni homa hatari ya virusi vinavyoenezwa na mbu. Pamoja Tutashinda.

Sote tujitahidi kuzingatia maelekezo haya. Ni kwa kushirikiana tu ndio tutaishinda homa hii hatari. Jikinge na wakinge wengine dhidi ya Homa ya Dengue. Ni homa hatari ya virusi vinavyoenezwa na mbu. Pamoja Tutashinda.

Written by simbadeo

May 6, 2014 at 11:27 pm

Papa John Paul II na Papa John XXIII … Watangazwa watakatifu

leave a comment »


Papa Francis akielekea madhabahuni kuongoza ibada maalumu ya Misa ya kuwatangaza watakatifu Papa John Paul II na Papa John XXIII huko Jijini Roma, Italia.

Papa Francis akielekea madhabahuni kuongoza ibada maalumu ya Misa ya kuwatangaza watakatifu Papa John Paul II na Papa John XXIII huko Jijini Roma, Italia.

Papa John Paul II na John XXIII watangazwa watakatifu

Vatikano imewatangaza leo hii mapapa wawili maarufu wa Karne ya 20 — John Paul II na John XXIII — kuwa Watakatifu katika sherehe zilizofana katika Jiji la Roma.

Chanzo: BBC World

Written by simbadeo

April 27, 2014 at 11:58 am

Waziri Mkuu ajiuzulu … Ni baada ya kivuko kuzama

leave a comment »


Ndugu wa watu wanaohofiwa kufa maji baada ya kuzama kwa kivuko kule Korea Kusini wakifuatilia taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw Chung, akitangaza kujiuzulu.

Ndugu wa watu wanaohofiwa kufa maji baada ya kuzama kwa kivuko kule Korea Kusini wakifuatilia taarifa ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Bw Chung, akitangaza kujiuzulu.

Huyu si mwingine bali ni Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Bw Chung Hong-won. Amejiuzulu kufuatia serikali yake kukosolewa vikali kwa namna ilivyoshughulikia tukio la kuzama kwa kivuko.

Katika taarifa yake, Bw Chung, aliyeonekana mnyonge, alisema: “vilio vya familia za watu ambao bado miili yao haijapatikana vinanifanya kukesha usiku kucha”.

Kivuko cha Sewol kikiwa na abiria 476 — wengi wao wakiwa wanafunzi na walimu — kilizama katika bahari huko Korea Kusini mnamo tarehe 16 Aprili.

Maofisa wamethibitisha kuwa watu 187 walifariki dunia, lakini kuna makumi wengine ambao hawajapatikana na wanahofiwa kuwa wamekufa maji.

“Kwa niaba ya serikali, ninaomba msamaha kwa matatizo mengi kuanzia kushindwa kuzuia kutokea kwa ajali hadi namna ilivyoshughulikiwa.”

Ndugu wenye hasira wamekuwa wakitoa shutuma kali dhidi ya kile kilichoonekana kama uzembe katika kuendesha operesheni ya uokoaji.

“Jambo sahihi kwangu kufanya ni kuwajibika na kujiuzulu kama mtu niliyekuwa kiongozi wa baraza la mawaziri,” alisema Bw Chung katika taarifa fupi iliyorushwa moja kwa moja kupitia televisheni.

Aliongeza: “Kumekuwa na matatizo mengi yaliyoendelea kutokea katika jamii yetu pamoja na utendaji ambao umekwenda kombo. Nina imani kuwa safari hii maovu haya yaliyojikita katika jamii yatasahihishwa na kuwa aina hii ya ajali hazitatokea tena.”

Hakukuwa na taarifa iliyopatikana mara moja kutoka kwa Rais Bi Park Geun-hye kama alikubali kujiuzulu kwa Bw Chung.

 

Chanzo: BBC World

Swali: Utamaduni huu wa kuwajibika kutokana na upungufu unaojitokeza katika uongozi utaota lini mizizi barani Afrika?

Written by simbadeo

April 27, 2014 at 11:37 am

Kilimo Kwanza … Tutavuna?

with one comment


Tina Bahati na mama yake wakitathmini ubora wa maendeleo ya mahindi. Wanaulizana, je, tutavuna? Tutapata mahindi ya kuchoma? Naam. Bustani ndogondogo hata Dar zinawezekana. Pamoja sana.

Tina Bahati na mama yake wakitathmini ubora wa maendeleo ya mahindi. Wanaulizana, je, tutavuna? Tutapata mahindi ya kuchoma? Naam. Bustani ndogondogo hata Dar zinawezekana. Pamoja sana.

Written by simbadeo

April 26, 2014 at 12:40 pm

Dar yanyanyasika … Dar humbled

with one comment


Wakati wa Tabata TIOT wakiwa kandokando ya Barabara ya Mandela wamejikunyata wakiwa hawajui wafanye nini kutokana na mafuriko kukumba makazi yao, huku baadhi ya mali zao zikisombwa na maji. Hali hii imejirudia katika vitongoji vingi sana vya jiji. Kwa hakika ... ni dhahama jijini.

Wakazi wa Tabata TIOT na maeneo ya jirani wakiwa kandokando ya Barabara ya Mandela wamejikunyata. Hawajui wafanye nini kutokana na mafuriko kukumba makazi yao, huku baadhi ya mali zao zikisombwa na maji. Hali hii imejirudia katika vitongoji vingi vya jiji. Kwa hakika … ni dhahama jijini.

Kuna msemo usemao, kufa kufaana. Wakazi hawa wa eneo la Kinyerezi Darajani wakijaribu kuunganisha barabara iliyokatika ili watu wapate mahali pa kuvukia. Hata hivyo, hawakufanya kazi hiyo bure. Kila kichwa kinatozwa Sh500 ili kuvuka kwa 'daraja' waliloweka vijana hawa. Barabara hiyo inatumiwa na mamia ya wakazi wa Mongolandege na Zimbili. Inaunganisha maeneo hayo na Barabara ya Kinyerezi.

Kuna msemo usemao, kufa kufaana. Wakazi hawa wa eneo la Kinyerezi Darajani wakijaribu kuunganisha barabara iliyokatika ili watu wapate mahali pa kuvukia. Hata hivyo, hawakufanya kazi hiyo bure. Kila kichwa kinatozwa Sh500 ili kuvuka kwa ‘daraja’ hilo. Barabara hiyo inatumiwa na mamia ya wakazi wa Mongolandege na Zimbili. Inaunganisha maeneo hayo na Barabara ya Kinyerezi.

Daraja jipya la Kinyerezi likikabiliana na misukosuko ya maji ya Mto Msimbazi. Litamudu? Kwa muda gani?

Mwananchi akishangaa kasi na nguvu ya maji. Daraja jipya (la muda?) la Kinyerezi likikabiliana na misukosuko ya maji ya Mto Msimbazi. Litamudu? Kwa muda gani?

Wakazi wa Mongolandege na Zimbili wakivuka katika kivuka kilichotengenezwa na vijana wanaotoza Sh500 kwa kila kichwa. Kwa hakika, kufa kufaana. Kivuko hicho, licha ya kutumika kuweka tozo iliyo ya juu ... bado si salama kwa watumiaji. Ni kivuko hatari hasa kwa watoto, wazee na akina mama. Pengine serikali ichukue hatua za haraka kushughulikia sehemu kama hizo katika Jiji la Dar.

Wakazi wa Mongolandege na Zimbili wakivuka kwa ‘kivuko’ kilichotengenezwa na vijana wanaotoza Sh500 kwa kila kichwa. Kwa hakika, kufa kufaana. Kivuko hicho, licha ya kutumika kuweka tozo iliyo ya juu … bado si salama kwa watumiaji. Ni kivuko hatari hasa kwa watoto, wazee na akina mama. Pengine serikali ichukue hatua za haraka kushughulikia sehemu kama hizo katika Jiji la Dar.

Taswira za matukio ya kutisha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha zinatawala vyombo vya habari vya aina zote, hasa vile vya kijamii. Je, unaweza kueleza vipi hali inayowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na jiji lenyewe.  … Mimi naona kuwa wananyanyasika na jiji limenyanyasika kutokana na mvua zinazoendelea kumwagika katika vitongoji mbalimbali na wilaya za jirani. Pengine hii ndio bei ambayo wakazi tunalipa kwa kukosa mipango miji? Pengine hii ni gharama tunayoingia kwa sababu za uzembe wa watu fulani? Kila mmoja atafakari nafasi yake katika haya yanayoendelea sasa jijini … je, unaweza kufanya nini kupunguza makali ya madhira haya?

Written by simbadeo

April 13, 2014 at 12:09 am

Kwa heri Dodoma … Adios Dodoma

with 2 comments


Mzunguko katika Makutano ya Barabara za Jamatini na Nyerere. Wenyeji huita Whimppy.

Mzunguko katika Makutano ya Barabara za Jamatini na Nyerere. Wenyeji huita Whimppy.

Pamoja na kwamba si msimu wa zabibu ... lakini zinapatikana kiasi chake. Hili ni zao moja muhimu sana kwa mji na mkoa wa Dodoma.

Pamoja na kwamba si msimu wa zabibu … lakini zinapatikana kiasi chake. Hili ni zao moja muhimu sana kwa mji na mkoa wa Dodoma.

Wadada wa Dodoma wakiyarudi magoma moto katika live show ya Sukki Stars katika kiwanja cha burudani cha Master Pub.

Wadada wa Dodoma wakiyarudi magoma moto katika live show ya Sukki Stars katika kiwanja cha burudani cha Master Pub.

Pamoja na kwamba kuna mengi ya kukumbuka kuhusu mji wa Dodoma, kikubwa sana nitakachokikumbuka ni barabara zisizo na foleni. Ukiwa na miadi mahali, unafika katika muda uliokubaliana na hao unaotaka kuonana nao. Kwa hakika, suala hilo lifanyiwe kazi ili liwezekane Dar es Salaam na miji mingine pia. Kwa heri ya kuonana Dodoma … Idodomya.

 

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 1,319 other followers