simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Matumaini kwa Wakazi wa Kinyerezi … Daraja Kujengwa

with 3 comments

Wahenga wanasema dalili ya mvua ni mawingu. Hapa kwenye daraja linalounganisha Kinyerezi na Segerea kuna dalili hizi. Naamini ni njema na zinazoleta matumaini mapya kwa wakazi wa pande zote mbili. Kipande hicho cha darajani kwenye barabara hiyo kimekuwa kero kubwa sana kwa watumiaji. Harakati hizi zinazoendelea sasa zinaleta matumaini makubwa.

Ingawa mimi si mtalaamu wa ujenzi, lakini si vibaya nikatoa ushauri kwamba daraja linyanyuliwe juu sana kupunguza ukali wa mteremko na vilevile kulipa nafasi kubwa kabisa chini ili maji ya mvua yapite pasipo kikwazo. Vilevile, tunataraji kuona daraja pana kiasi cha kutosha hata magari manne kupishana ili kuzuia/kupunguza uwezekano wa kutokea ajali.

Na kwa kukumbushia tu. Kazi ikikamilika hapo, serikali ielekeze macho yake kwenye daraja la Kinyerezi linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita. Ni daraja finyu sana. Mara nyingi unapotokea mkwamo wa dakika mbili tu, tayari foleni pande zote mbili zinaenda umbali wa kilometa mbili. Ni vema daraja linanuliwe ili magari yapishane na iwekwe sehemu ya wapita kwa miguu — ni muhimu sana kuwalinda watoto na wazee wanaopita pale. Si vema tusubiri hadi ajali itokee kisha ndiyo tuchukue hatua. Kinga ni bora kuliko kutibu.

Pamoja sana. Wimbo: ‘Ni bora kujenga daraja … kuliko kujenga ukuta’ endelea…

Written by simbadeo

November 14, 2012 at 9:20 am

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. Barabara hii ni kiunganishi muhimu sana kwa wakazi manispaa zote za Jiji la Dar es Salaam kwa kuunganishwa na ile inayotoka Mbagala-Chamazi,Magole-Kitunda -Banana -Kinyerezi-Mbezi hadi Tegeta au Tandika-Mwanagati-Kitunda -Banana-Kinyerezi-Mbezi hadi Tegeta.Kukamilika kwa mtandao huu wa barabara hata kwa kiwango cha changarawe kwa baadhi ya maeneo itakuwa ni faraja na ukombozi kwa wananchi katika kupunguza muda wa kukesha barabarani kutokana na foleni.

    Like

    ray

    November 14, 2012 at 1:01 pm

    • Ndugu Ray. Umenena. Ama kwa hakika tunaweza kabisa kupunguza foleni za Dar kwa kuimarisha barabara hizi za ndani kwa ndani. Pia tutaokoa muda mwingi sana unapotea kwenye foleni hizo, achilia mbali mafuta yanayochomwa na vipuri vinavyohitajika kwa ukarabati wa vyombo vya moto. Pamoja sana.

      Like

      simbadeo

      November 16, 2012 at 11:25 pm

    • Ray. Asante kwa kupanua mada na kuipa uzito zaidi. Thanks bro.

      Like

      simbadeo

      November 18, 2012 at 2:22 pm


Leave a comment