simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for November 26th, 2012

Mabibo Hosteli … Mandhari Kiduchu

with 2 comments


Ndiyo. Ni kiduchu tu. korido hiyo ndefu na cafeteria pale Mabibo Hosteli. Kwa hakika huu ulikuwa mmoja wa miradi madhubuti kwa fedha za NSSF (au za wanachama wa taasisi hiyo?). Ukiachilia mbali baadhi ya yale ambayo hujiri hapo … Lakini hapa pamekuwa kitovu muhimu sana katika elimu ya juu nchini. Kuna wengi tu wamepita hapa katika safari yao ya elimu. Kwa wale walio hapo … wakumbuke tu parable ya Nyerere: Kijiji hakikuwa na chakula. Wakaona ni bora wamchagua kijana mmoja, wamkabidhi chakula chao cha akiba, ili yeye akitumie kwenda kutafuta chakula zaidi kwa ajili ya wanakijiji wenzake. Kijana akatoka kwenda zake … SASA, sina hakika kama alisharudi na kupeleka chakula kule kijijini kwake, au baada ya kufika nchi ya neema alisahau kabisa kuhusu wanakijiji waliotoa sadaka chakula chao ili yeye awe na nguvu za kwenda kuwaletea na wao chakula? Maana hizi habari za mabilioni kufichwa Uswisi, na jinsi watu walivyogeuka kuwa mchwa wala fedha na mali ya umma katika karibu kila taasisi … si dalili nzuri. Huenda kijana aliAMUA kuendelea kutumikia tumbo lake binafsi.

Sasa wewe uliye hapo … jitafakari, chukua hatua. Wewe uliyepewa chakula ili uwasaidie wanakijiji wenzako, tafakari, chukua hatua.

Pamoja sana!

Written by simbadeo

November 26, 2012 at 10:46 pm

Cosmetics / Vipodozi … Wapi Vipa Umbele Vyetu?

leave a comment »


Ni biashara kubwa sana ulimwenguni. Kwa kila shilingi 100,000 inayotumiwa kununua vipodozi, ni shilingi 1,000 tu ndiyo inayotumiwa kununua vitabu. Hebu fikiria kama walau robo tu ya fedha inayotumiwa kununua vipodozi ingetumiwa kwa ajili ya vitabu … na kisha watu wavisome. Nina uhakika wa asilimia zote kwamba jamii yetu na nchi yetu vingekuwa vimepiga hatua kubwa sana ya kimaendeleo na kuwa utamaduni madhubuti — unaoenzi na kuendeleza ubunifu chanya. Vinginevyo … tutarajie kuendelea na jamii ya WAKOBOKAJI. Aaghrr! Wapi vipaumbele vyetu?

Kama huamini takwimu hizo hapo juu … tazama waliokuzunguka … iwe kwenye daladala, ofisi, sherehe, nyumba ya kupanga, chuoni, shuleni … popote.

Written by simbadeo

November 26, 2012 at 10:36 pm