simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for November 14th, 2012

Matumaini kwa Wakazi wa Kinyerezi … Daraja Kujengwa

with 3 comments


Wahenga wanasema dalili ya mvua ni mawingu. Hapa kwenye daraja linalounganisha Kinyerezi na Segerea kuna dalili hizi. Naamini ni njema na zinazoleta matumaini mapya kwa wakazi wa pande zote mbili. Kipande hicho cha darajani kwenye barabara hiyo kimekuwa kero kubwa sana kwa watumiaji. Harakati hizi zinazoendelea sasa zinaleta matumaini makubwa.

Ingawa mimi si mtalaamu wa ujenzi, lakini si vibaya nikatoa ushauri kwamba daraja linyanyuliwe juu sana kupunguza ukali wa mteremko na vilevile kulipa nafasi kubwa kabisa chini ili maji ya mvua yapite pasipo kikwazo. Vilevile, tunataraji kuona daraja pana kiasi cha kutosha hata magari manne kupishana ili kuzuia/kupunguza uwezekano wa kutokea ajali.

Na kwa kukumbushia tu. Kazi ikikamilika hapo, serikali ielekeze macho yake kwenye daraja la Kinyerezi linalounganisha Kinyerezi na Majumbasita. Ni daraja finyu sana. Mara nyingi unapotokea mkwamo wa dakika mbili tu, tayari foleni pande zote mbili zinaenda umbali wa kilometa mbili. Ni vema daraja linanuliwe ili magari yapishane na iwekwe sehemu ya wapita kwa miguu — ni muhimu sana kuwalinda watoto na wazee wanaopita pale. Si vema tusubiri hadi ajali itokee kisha ndiyo tuchukue hatua. Kinga ni bora kuliko kutibu.

Pamoja sana. Wimbo: ‘Ni bora kujenga daraja … kuliko kujenga ukuta’ endelea…

Written by simbadeo

November 14, 2012 at 9:20 am