Enero la Feri jijini Dar. Ni mahali unapoweza kutembea na kuburudika. Hata hivyo, kuna changamoto nyingi. Soko la samaki limechakaa ndani ya muda mfupi sana … kama muongo mmoja tu. Swali la kujiuliza … kutujengea watujengee … hata kutunza nako waje kututunzia? Sisi kazi yenu ni nini? Kukusanya ushuru tu??? Tubadilike!
Mvua inapoamua kunyesha … Hapana budi kusubiri … Ndivyo ilivyokuwa … Dakika 45!
Haya … ulimi unaniponyoka … Mara nyingi huwa tunalazimishwa kutenda vitu vingi pasipo kuhiyari. Mathalani, upo kituo cha basi, unasubiri usafiri ambao nao unakuwa umeota mbawa … huna hili wala lile … mara anakuja jamaa na spika yenye sauti kali … anakatisha fikra ulizo nazo kwa kuanza kukumiminia neno. Papo hapo hakukutaka radhi, hakuomba ruhusa yako kama unaridhia kusikiliza au la. Kuondoka hapo huwezi, maana ndipo mahali pa wewe kupata usafiri. Unajikuta unameza dozi bila kupenda … sorry … Vitendo kama hivi … haviwezi kuwekwa kundi moja na ‘ubakaji’? Vipo vingine vingi. Huu ni mfano mmoja tu! Kuuliza si ujinga … wahenga walisema!
Weekend njema wadau wa blogu hii. Mbarikiwe sana. Natumaini nimepata ridhaa yako hapo kabla ili kukuletea makala hii. Maoni ni ruksa, tusivunje tu sheria za nchi! Pamoja sana!
-6.822921
39.269661
Hahahaha kaka simba umenichekesha sana, yaani kitendo cha kupewa dozi ya neno la Mungu kwa kushtukizwa umekiita “ubakaji”? Hapo kunawengine wameshukuru kupata dozi hiyo kwani mioyo yao imepona na kunawengine wamedharau na kuponda, sasa lipi jema aliyedharau au aliyeponyeka?
LikeLike
dorin
January 29, 2013 at 9:57 am
Dorin. Mtu anayetaka kusikiliza ‘Neno’ aende kanisani. Makanisa yapo wazi. Kunapokuwa na maandalizi ya mikutano kama hiyo, yafanyike mawasiliano na mamlaka zinazohusika na watu wapewe taarifa muda wa kutosha ili kila mmoja ajue kwamba wiki ijayo maeneo fulani kutakuwa na tukio fulani. Asiyependa, atafute njia nyingine ili ‘asibughudhiwe’ na hicho kitakachoendelea hapo. Vinginevyo, unapolazimishwa ‘kushiriki’ jambo pasipo hiyari yako … ni sawa na kufanyiwa kitendo hicho kisicho cha kiungwana … ni maoni tu. Wengine pia wanakaribishwa kutupa maoni yao.
LikeLike
simbadeo
January 30, 2013 at 3:21 pm