simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for January 20th, 2013

Tembea Dar … Tazama Sanaa ya Majengo ya Kale

leave a comment »


Unapotokea Kivukoni Front ...

Unapotokea Kivukoni Front …

Mahakama ya biashara ...

Mahakama ya biashara …

Magereza na Ofisi za Takwimu ...

Magereza na Ofisi za Takwimu …

Mahakama ya Rufaa Tanzania ...

Mahakama ya Rufaa Tanzania …

Kanisa la Kilutheri ... Azania Front ...

Kanisa la Kilutheri … Azania Front …

Atman House (foreground) na Mnara wa St Joseph Cathedral ...

Atman House (foreground) na Mnara wa St Joseph Cathedral …

Railway Station ...

Railway Station …

There is art everywhere. You just have to open your eyes. You just have to open your mind. You just have to open your ears. Your five senses, plus the sixth one. Sanaa imetuzunguka kila mahali, fungua macho, masikio, akili, milango yako mitano ya ufahamu (pamoja na ule wa sita). Binafsi huwa ninaguswa sana na kazi za sanaa zilizojificha kwenye majengo. Majengo yaliyo kwenye picha hapo juu yana zaidi ya miaka 75 tangu yajengwe. Lakini unaweza kuona sanaa ya hali ya juu iliyo nyuma yake, kwamba waliobuni michoro na kufanya kazi ya kujenga, walitulia na kutulizana.

Ninapotazama majengo mengi yanayojengwa siku hizi … pamoja na teknolojia ya ujenzi kukua sana, bado ninahisi upungufu katika akili yangu. Kuna kitu kinakosekana katika kufanya majengo hayo yawe na mvuto kamili. Kuna tofauti sana kati ya bidhaa inayotengenezwa kwa mkono na zile zinazozalishwa kwa mpigo kufuata modeli moja iliyotengenezwa. Ndivyo nionavyo kati ya majengo ya zamani na majengo ya siku hizi.

Tofauti hizi, tunaweza kuziona sana katika namna tunavyojenga majengo yetu ya ibada siku hizi na yale yaliyojengwa zamani. Haijalishi kama ni makanisa au misikiti. Naona siku hizi tunalipua zaidi. Sidhani kama watu wanaweka mioyo na akili zao katika majengo hayo wanayojenga.

Pamoja sana!