Archive for January 16th, 2013
KIA … Kazi ya Sanaa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (JRO/KIA) … nao ni sanaa ya aina yake. Ingawa ni uwanja mdogo na kama unatoka ughaibuni utahisi kama vile unatua kwenye uwanja wa ndege wa Kijiji, kubwa ni kwamba aliyesanifu ramani ya jengo na mpangilio wa vitu kuwa nini kiwe wapi na wapi kiwekwe nini alifanya kazi nzuri. Upungufu uliopo unaweza kushughulikiwa na uongozi wa sasa, hasa kwa vile hivi sasa kiwanja hiki kimeanza kuwa na kazi nyingi na kwa hiyo kinaingiza mapato mazuri.
Kilicho chako, japo kidogo, yakupasa kujivunia.
Pamoja sana