simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Amani Tanzania … Penye Miti Hakuna Wajenzi

with 4 comments

Hali ya mambo imekuwa si shwari katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, hasa mitandao ya kijamii, kuna kikundi kiliamua kufanya maandamano yasiyo rasmi ili kushinikiza kuachiwa kwa Sheikh Ponda. Polisi wa kuzuia ghasia na askari jeshi walimwagwa mitaani ili kudhibiti hali ya mambo.

Ama kwa hakika, tunaona upepo ukigeuka hapa nchini. Katika siku za karibuni tumeshuhudia kuongezeka kwa vurugu za kila aina. Ukitafuta kiini hasa cha machafuko hayo mtu hukioni.

Mathalani, katika picha hiyo ya tatu hapo juu, kuna jambo lililonigusa sana. Kuna huyo mwanafunzi (msichana) anayejaribu kuvuka barabara. Hebu wewe uliyedhamiria kuanzisha vurugu, je,uliwafikiria watoto hawa? Uliwaza kuhusu wazee, wenye ulemavu, maendeleo ya nchi kwa ujumla? Pengine huwezi kumfikiria mtoto huyu kwa sababu wewe si mzazi (maana wahenga wanasema, uchungu wa mwana aujuaye mzazi), lakini bado unaweza kuwa kaka, mjomba, binamu au basi jirani yake. Je, kabla ya kuingia mitaani na kuanzisha vurugu hizo, uliwaza ni namna gani mtoto huyu atatoka shuleni kwake, atafute usafiri na kurejea nyumbani kwao salama? Je, nini hasa kilikusukuma kuona usalama wa mtoto huyu ni kitu kidogo sana kuliko hicho unachokipigania?

Maswali ni mengi. Ila hakuna sababu hata moja inayoingia akilini kuhalalisha taharuki, mateso, hofu, mashaka na wasiwasi mkubwa anaoupata mtoto huyu kwa mazingira hayo ya fujo na vurugu uliyomwekea. Sizungumzii hisia za mzazi, maana pengine wewe uliyeamua kuanzisha fujo una chuki na watu wazima wote — hasa wale ambao hawakubaliani na matakwa yako.

Tanzania imekuwa chemichemi ya amani kwa miaka mingi sana. Amani hii ni lulu. Amani hii ina thamani kubwa sana kuliko utashi wako wewe mtu mmoja unayelala usiku ukiwaza ni namna gani uanzishe fujo. Hebu nikuase, hii ni nchi yenye miti (amani), wajenzi tupo, wewe mmoja usifanye sote tukose maana kwa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Tudumishe amani Tanzania. Choyo na ubinafsi tuvipige vita. Tupige hatua ya kukua zaidi kidogo na kutafakari athari na masaibu tunayoweza kuwasababishia watu wenzetu kwa sababu tu ya kutaka kutimiza tamaa yetu … pengine kujipatia umaarufu kwa njia zilizo rahisi.

Mwenyenzi Mungu, Mwingi wa Rehema tupe uvumilivu, tujaalie hekima na uwezo wa kuzishinda tamaa zetu. Amina.

Picha zote ni kutoka Wavuti.

Advertisements

Written by simbadeo

October 19, 2012 at 4:41 pm

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Reblogged this on Jemedari Kalundi's Weblog.

  Like

  jemedarikalundi

  October 19, 2012 at 6:13 pm

 2. Hii sio Tanzania Aliyoiacha Baba wa Taifa Mwl. Julius K Nyerere. Hivi hao watu wachache wasio na ufahamu wanataka nn? wakisababisha machafuko na vurugu na wakapoteza maisha inawafaidia nn? maana Ss wote jamii nzima ya Tanzania tunakaa na Dini zetu tunaheshimiana na kupendana. Mimi siamini hawa ni waisilamu ila wanavaa vivuli vya uislamu na wala si Waislamu ninaojua waislamu kweli wapo nao wanawashangaa. Na naamini pia hawaijui Dini ya kiislamu wala uislamu na wala hawaswali. Wakati Mahujaji wako MAKA kwa niaba yetu kuombea nchi zetu wao wanafanya yasiopasa. Wasituharibie na kuchafua undugu na amani tuliyonayo. Penye Upendo uovu hubainika.Tutabaki kuwa Ndugu na Amani yetu itadumu, watashindwa na udhalimu wao kwa Jina la Mwenyezi Mungu. Wala mwenyezi Mungu kwenye vitabu vyote iwe kuruani au biblia hajaagiza fujo na machafuko, ameagiza watu kuishi kwa upendo na amani na ndilo tunaloomba kila siku na Mwenyezi mungu anasikia dua zetu. Na naamini wafanyao mambo hayo si Watanzania, kama ni watanzania wangejua tulikotoka na wakajivunia walivyo hata kama kuna mapungufu kwa binadamu au maisha ni kawaida. WAISLAMU na WAKRISTO tufahamu ss ni NDUGU na haiwezekani kumkana NDUGUYO, hiyo na LAANA. Tafuteni jinsi ya kurekebisha Kero au makwazo yenu, Wako viongozi wa Kiislamu wenye Busara na upeo mkubwa wa kusaidia Jamii nduo maana Mwenyezi Mungu aliwachagua kwa ajili yetu watasaidia kusuluisha kwa Amani na utulivu ili Nchi yetu iendelee kuwa mfano mwema kwa Mataifa. MUNGU IBARIKI TANZANIA! MUNGU IBARIKI AFRIKA! MUNGU IBARIKI DUNIA NZIMA KWA UJUMLA.

  Like

  Diana Samson

  October 19, 2012 at 7:01 pm

  • Tuna changamoto kubwa Da Diana. Endelea kutushauri Watanzania ili tubadilike … sote kabisa kwa pamoja.

   Like

   simbadeo

   October 21, 2012 at 11:00 pm

 3. Watu wengi wanaofanya fujo ni wale ambao hawana kazi za kufanya na pia hawataki kutoa jasho kupata ridhiki za kila siku. Hivyo kwa mtazamo wangu wale wote ambao walikuwa siku ile kwenye vurugu hizo si Waislaam pekee na rafiki zao wa dini tofauti walijiunga kuongeza fujo hizo ili kukwapua na kuvunja vitu vya watu wengine.

  Tuwe macho nao.

  Like

  Bibi Mwapombe

  October 24, 2012 at 11:33 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s