simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Digital Divide … Filling the gap

with 3 comments

Kwa takwimu zilizopo, ni kaya chini ya asilimia 20 tu ndiyo zilizounganishwa kwenye mitandao ya umeme unaozalishwa hapa nchini. Katika zama hizi za teknolojia na matumizi ya vifaa vinavyohitaji umeme, asilimia hiyo zaidi ya 80 imeachwa nyuma. Hata hivyo, watu hujitahidi kivyao kutokuachwa nyuma sana … ingawa hawana budi kuingia gharama zaidi. Njia moja wanayotumia ni kwenda kwenye maeneo ya kuchajisha simu. Kwa hiyo, unaweza kuishi nyumba isiyounganishwa na umeme, lakini bado ukamiliki simu na ukaiwekea umeme kwa kwenda kwenye sehemu zinazotoa huduma hizo.

Picha hiyo ni katika moja ya sehemu zinazotoa huduma hiyo katika mji wa Mpanda. Ni karibu kabisa na soko kuu.

Pamoja sana!

Advertisements

Written by simbadeo

October 18, 2012 at 9:51 am

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Bwana Deo,
  Hiyo ni kweli lakini kitu ambacho mimi nimekijua ni hawa wenye kuchajisha simu baadhi yao huwa si waaminifu. Wanabadilisha sana betri na wakati mwingine pia hutumia simu hizo kupiga simu zao. Tafadhali tuwe macho sana. Lakini yote kwa yote ni kitu kinachosaidia saaaana.

  Like

  Bibi Mwapombe

  October 18, 2012 at 10:10 am

 2. Nakubaliana na aliyetangulia kuwa wanabadilisha betri na kutumia kwa kupiga..ila unachotakiwa kufanya usipeleke kuchanji wakti simu ina hela/salio kubwa…

  Like

  yasinta

  October 18, 2012 at 11:27 am

  • Ni kweli. Mtu asiye na umeme nyumbani kwake anaingia gharama nyingi sana. Nyingine ndiyo kama mlizoziainisha: kupoteza muda kupeleka simu kuchajiwa, kuibiwa betri/salio/housing na charging kutumia charger zisizo na viwango na kwa hiyo kusababisha simu kufa haraka. Kwa hiyo, ninakubaliana na wachangiaji wenzangu hapo juu kwamba ‘digital divide’ ni adui anayepaswa kutokomezwa. Njia moja ni kuongeza idadi ya kaya zinazounganishwa na mitandao ya usambazaji umeme nchini. Kubuni vyanzo vingi zaidi vya umeme. Kuleta ubunifu wa matumizi ya nishati mbadala, mathalani, nishati ya jua n.k. Pamoja sana Bibi Mwapombe na Yasinta.

   Like

   simbadeo

   October 19, 2012 at 4:50 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: