simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for April 2012

Vingunguti … Taswira Kiduchu tu

leave a comment »


a href=”https://simbadeo.wordpress.com/?attachment_id=4769″ rel=”attachment wp-att-4769″>

Haya … washabiki wa soka wakifuatilia mechi kati ya Simba SC ya Dar es Salaam, Tanzania dhidi ya Al Ahly Sindy ya Sudan. Hadi mwisho wa mchezo Simba 3, Al Ahly Sindy 0. Inasubiriwa mechi ya marudiano na Inshaallah, Simba itashinda ili kusonga hatua nyingine ya mashindano hayo ya kimataifa na yaliyo muhimu Barani Afrika.

Haya … tangazo la burudani ya soka la ulimwengu mzima …

Mitaani. Wale wenye majumba yenye thamani ya milioni 600 na ushee tena walizilipa cash … Wajichunguze nafsi zao. Ni hela safi? Je, katika fedha hiyo, hakuna ambayo pengine ilikusudiwa iwafikie watoto hawa na wakazi wa maeneo haya? Maisha … Mhubiri anasema kila kitu ni BATILI … BATILI … BATILI

Kona nyingine … vijana wanakonga nyoyo. Kila watu na zama zao. Vijana wa zamani. Vijana wa sasa. Wazee wa sasa. Wazee wa miaka ijayo. FROZEN in time.

Aaah! DJ akifanya vitu vyake. Na amevalia rangi ya USHINDI. …

Jamii isipowapa vijana mahali pa kujiburudisha kwa michezo … basi nature itawapa. Hapo vijana wakisakata kabumbu kwenye eneo ambalo mto umekusanya mchanga. Bila shaka wakati wa mvua nyingi kipande hicho hufunikwa na maji. Lakini kwa sasa vijana wamepata uwanja … na soka linaendelea.

Hiyo ndiyo ziara fupi ya baadhi ya mitaa ya Vingunguti jijini Dar.

Written by simbadeo

April 29, 2012 at 11:45 pm

Identity … Masai people

leave a comment »


Keeping one’s identity, let alone a whole community’s is not easy, especially with all sorts of pressure from all over. However, the Masai people, found mostly in Northern Tanzania and parts of Kenya have managed to keep their identity in spite of the pressure of modernity. You’ll still find them in their traditional attires along with the asortments that go with them. Their life styles have almost endured intrusions from the outside world and other communities. As such, they have become unique and can easily be recognisable.

There are many lessons we can draw from the Masai people. There may be so much pressure around us to lose our identity, yet we can contain it and pick only the things we want. The Masai have done it. You will find them in politics (with some ascending to very high offices – like the former Prime Minister of Tanzania, Edward Moringe Sokoike), they are in business – large and small; and they are not far behind in social affairs that also involve people from other communities. Technologically – they are in and make use of it just like everybody else.

What does this say. Our identities are important. It is through them that we can stand out and speak of what we are. East Africa is becoming one, however, each member state may as well keep its identity – the things that make it unique.

Shukrani kwa watu wa jamii ya Wamasai kwa kutuonyesha njia. Tunaweza kuendana na mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kiteknolojia pasipo kupoteza utambulisho wetu.

identified in a cr

Written by simbadeo

April 29, 2012 at 2:54 pm

Darkness … light ahead

leave a comment »


Kiza hufuatwa na mapambazuko. Kama kuna giza hapa, mbele kuna mwanga. Maisha nayo ni hivyo. Sasa giza, baadae mwanga. Upitiapo magumu, jua yana mwisho. Kikubwa ni nia ya kuendelea. Kukata tamaa kusipewe nafasi hata chembe. Kiza pia ni wakati wa kutafakari. Kuingia ndani – ya nafsi yako – ili kujichunguza na kujitayarishia kipindi cha mapambazuko. Yote haya yawezekana katika nafsi zetu, jamii na hata taifa. Daima mbele.

Written by simbadeo

April 27, 2012 at 12:11 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , , ,

Muungano Day … Ni safari ndefu

with 2 comments


Bado dakika chache tuanze kusherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu unatimiza miaka 48. Ni umri wa mtu mzima. Ni umri wa mtu ambaye katika hali ya kawaida anakuwa na majukumu mazito katika familia na jamii yake. Ni umri wenye kuheshimika ikiwa mtu unajiheshimu.

Tangu kuwepo kwa Muungano huu jamii ya Watanzania imenufaika na mengi. Katika muungano huo, nchi ilihimili vishindo na mikiki ya Vita Baridi kati ya Magharibi na Mashariki. Katika zama hizo, Tanzania ilijipambanua kama Taifa lenye falsafa makini na uwezo wa kuchagua nani awe rafiki na nani asiwe rafiki. Taifa lilikuwa na kauli na kauli hiyo ilisikilizwa na hata wale wanaojiona wao ndiyo wakubwa katika ulimwengu huu.

Chini ya Muungano huu pia Taifa lilishinda Vita vya Uganda na kufanikiwa kumng’oa Nduli Idd Amin Dadaa. Ikumbukwe kwamba chini ya ‘Uwezo Tunao, Sababu Tunayo, Nia Tunayo’ wapiganaji kutoka pande zote mbili za Muungano walishiriki. Hii ilituingiza katika undugu ule wa damu. Kuna watu — bila shaka umewahi kusikia — huingia udugu kwa kuchanjiana damu. Tanganyika na Zanzibar ziliingia kwenye udugu wa aina hii wakati wa vita vile.

Kuna upungufu pia. Bado Muungano wetu haujafaulu sana katika kukomboa wananchi dhidi ya maadui wale wakubwa: Umaskini, Maradhi na Ujinga (Siku hizi kuna adui mpya aliyeingia – Ufisadi). Sina hakika kama nje ya Muungano kila upande ungekuwa umepiga hatua kubwa zaidi. Sina njia ya kupima jambo hilo. Lakini kwa ujumla maisha ya watu wa kawaida bado ni ya shida sana.

Upungufu mwingine ulio karibu na huo uliotangulia ni kule kukua kupita kiasi kwa tofauti ya kimapato na hali ya kimaisha kati ya wachache walio nacho na wengi wasio nacho. Hili ni tatizo kubwa. Hili ni jambo litakaloendelea kuutikisa Muungano watu tupende au tusipende.

Upungufu mwingine, nao unakaribiana na huo wa kwanza hapo juu, suala la UTEGEMEZI kwa mataifa ya nje ni ugonjwa mkubwa sana unaotudhoofisha kibinadamu. Miaka 48 ya Muungano bado tunatembeza bakuri kwa wafadhili? Hapa Muungano bado haujafaulu. Hatuna budi kurejea kwenye itikadi yetu ya kutafuta kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Tukifaulu kupunguza na hatimaye kuondosha utegemezi wetu kwa mataifa ya nje, hapo tutarejea kuwa na kauli inayosikilizwa, kauli inayoheshimiwa. Hivi sasa, hawa mabwana wakubwa watatuendesha tu kama wanavyotaka. Wakitaka uranium yetu — watajichotea kwa bei karibu na bure; wakitaka mafuta na gesi vivyo hivyo. Aah. Uhuru wetu utabaki kuwa wa bendera.

Vinginevyo, ninawapongeza sana Watanzania wa pande zote mbili kwa kutimiza miaka 48 ya Muungano. Kwa pamoja tumeonyesha njia kwamba Afrika inaweza kuwa moja. Sharti tuanze hatua kwa hatua. Nchi moja moja, kanda moja moja hatimaye bara zima.

Masuala ya kumeguka kwa nchi kama ilivyokuwa kwa Sudan ni sehemu muhimu ya kuelekea kwenye Bara moja, kwani ni lazima kwanza kuvunjilia mbali ile mipaka iliyolazimishwa na wakoloni ili kupata mipaka ya asili. Baada ya hapo safari ya kuungana itaanza kwa kasi na nguvu mpya.

Tumeweza. Tusonge mbele. Tuweke haki, heshima na umoja mbele. Kila mmoja atimize wajibu wake vile inavyompasa … kwa kuanzia.

Written by simbadeo

April 25, 2012 at 11:33 pm

Waziri Mkuu Ajiuzulu … ni wa Uholanzi

leave a comment »


Dutch prime minister Mark Rutte resigns over austerity measures
Mark Rutte, the Dutch Prime Minister, handed his resignation to the country’s Queen after European Union demands for austerity measures to bring Holland into line with euro spending rules caused the collapse of his government.

Early elections, as early as June 27, will become a popular vote on EU imposed austerity measures after the fall of a Dutch government that over the last year strongly backed the eurozone’s fiscal union treaty and urged that Greece be stripped of sovereignty for falling behind with spending cuts.

Mark Rutte, the Prime Minister, resigned after his fragile liberal-conservative coalition government, which has a no parliamentary majority, fell apart at the weekend after the far-right Freedom Party walked out of talks to implement £12 billion (15bn euros) in cuts.

“The government now knows that it is no longer sufficiently assured of the necessary parliamentary support to do what is necessary for our national economy,” he admitted in his resignation letter to Queen Beatrix.

Diederik Samsom, the leader of the pro-European opposition Labour Party accused Mr Rutte of “dropping the ball at the worst possible moment” and demanded snap elections

“We have to deliver clarity to the country as soon as possible,” he said.

Source: http://www.telegraph.co.uk/news/worldnews/europe/netherlands/9221378/Dutch-prime-minister-Mark-Rutte-resigns-over-austerity-measures.html

HAYA. KATIKA SUALA LA KUWAJIBIKA NA UWAZI. WAZIRI MKUU WA UHOLANZI AMEAMUA KUJIUZULU KATIKA HEKAHEKA ZA KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI KUTOKANA NA MGOGORO WA KIFEDHA ULIOZIKUMBA NCHI ZA ULAYA. MARA NYINGINE ILI MTU ULINDE HESHIMA YAKO NA YA TAIFA LAKO, HUNA BUDI KUCHUKUA UAMUZI MGUMU. NAMPONGEZA WAZIRI MKUU MSTAAFU MARK RUTTE WA UHOLANZI KWA KUONYESHA NJIA. TUPO PAMOJA …

Written by simbadeo

April 23, 2012 at 11:53 pm

Posted in Siasa na jamii

Bahari … jimwage

with 2 comments


Jiachie … usijishikilie.

Hivi ule mpango wa kutumia bahari ili kutoa huduma za usafiri wa kutoka maeneo ya Tegeta/Boko kwenda mjini umefika wapi? Wenye mapesa … fursa hiyo ya kuwekeza. Mtasaidia sana kupunguza foleni kwenye barabara ya kwenda Bagamoyo. Vituo ni vingi. Wenye kuhitaji huduma hiyo ni wengi. Kwa hiyo fursa ya biashara ipo. Kikubwa ni kuhakikisha tu kwamba vyombo hivyo vya usafiri vinakidhi viwango vyote vinavyohitajika kufanya safari iwe salama.

Hii ni salamu … baada ya ukimya wa siku kadhaa.

Written by simbadeo

April 22, 2012 at 11:03 am

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , ,

Baiskeli … Suluhu kwa foleni jijini Dar?

with 3 comments


Nimeipenda hii. Imagine asilimia 75 ya watu wanaotumia magari yao binafsi kwenda na kurudi kazini (kwenye biashara) hapa jijini Dar wangekuwa wakitumia baiskeli. Naamini foleni zingepungua sana kwenye barabara za jiji hilo, au siyo? Vilevile, watu wangekuwa na afya bora zaidi … vitambi vingepungua, maana kuendesha baiskeli ni mazoezi mazuri sana ya mwili.

Labda maofisi ingebidi yawe na maji zaidi na mabafu ili watu wakiingia waoge na kubadili nguo … Si unajua tena hali ya Dar ilivyo? Lakini pamoja na changamoto hiyo, bado nafikiri kwamba Dar ingekuwa mahali bora zaidi na hata hali ya hewa ingekuwa safi zaidi. Hebu fikiri kuhusu moshi wa magari unavyochafua hewa … na sauti za honi na mingurumo zinavyoondoa utulivu … Aaaah Bongo!

Written by simbadeo

April 16, 2012 at 12:33 am

Posted in Siasa na jamii

Msiba … Mwanasoka afariki katikati ya mchezo

with one comment


Serie A – Serie B star dies after cardiac arrest on pitch

Piermario Morosini has died after suffering a cardiac arrest during an Serie B game at Pescara on Saturday, prompting the Italian football federation to postpone this weekend’s professional games.

“We have done everything possible to save him but he never regained consciousness,” doctor Leonardo Paloscia said.

Another doctor at the Pescara hospital said the 25-year-old, a former Italy under-21 international who was at Udinese until January, was dead on arrival at hospital.

The news comes just weeks after Bolton Wanderers midfielder Fabrice Muamba suffered a similar problem in an FA Cup match before making a remarkable recovery.

Serie A said in a statement that the federation had postponed all the weekend’s professional matches.

Morosini, born in Bergamo and a former player with the city’s Atalanta team, fell to the ground with no one around him in the 31st minute.

He got up looking confused and then collapsed again as medics and then an ambulance rushed on to the field.

The Serie B game was abandoned with Livorno leading 2-0 and Morosini, who was orphaned as a teenager and also lost a brother, was taken to a Pescara hospital where he was pronounced dead.

Defending Serie A champions Milan were due to host Genoa in Serie A that afternoon.

At first Milan said there would be a minute’s silence but then the public announcer told fans already in the stadium that the game would be postponed along with all other remaining Serie A matches this weekend.

There was applause but also some whistles.

The Italian Olympic Committee (CONI), which confirmed Morosini had suffered a cardiac arrest, announced in a statement that all other sporting events taking place this weekend would hold a minute’s silence.

The issue of players’ health has long been in focus across the game with extra medical and heart checks being brought in throughout many leagues.

Marc-Vivien Foe collapsed during Cameroon’s 1-0 victory against Colombia in a Confederations Cup match in June 2003 in Lyon, France and died shortly afterwards aged 26.

The shock over that high-profile death, one of at least 20 in the last 20 years in professional leagues, led to changes but some believe more needs to be done.

In the wake of Bolton’s Muamba suffering a cardiac arrest while playing at Tottenham Hotspur in an FA Cup quarter-final on March 17, Manchester City manager Roberto Mancini – an Italian – said English medicals were not as good as in his homeland.

Muamba too fell to the ground with no one near him and doctors later said he had been “in effect dead” for 78 minutes while his heart did not beat on its own. He was revived and has gone on to make extraordinary progress in hospital.

He is now walking and recently tweeted a photograph of himself sitting up in bed and smiling.

The Italian medical system hailed by Mancini did not help Morosini, however. Tearful Livorno players travelled to the hospital to pray alongside his body.

Italy is used to sporting tragedy in recent years.

Last October, popular MotoGP rider Marco Simoncelli died after a crash at the Malaysian Grand Prix.

Franco Ballerini, the coach of Italy’s cycling team, also died in a rallying accident in 2010.

Source: Reuters

Kuna umuhimu mkubwa wa kuwafanyia wanamichezo uchunguzi wa kiafya kila baada ya wiki kadhaa. Matukio kama haya ya mchezaji kuanguka uwanjani na kufariki yanatia simanzi sana. Lakini hatua madhubuti za uchunguzi wa afya zikifanyika kila baada ya muda fulani, basi naamini matukio yatapungua. Soka ni mchezo wenye wapenzi wengi sana ulimwenguni na kwa hiyo bila shaka wengi wameguswa kama mimi nilivyoguswa. R.I.P. Piermario Morosini na pole nyingi kwa familia yake na wapenzi wa klabu aliyokuwa akichezea. Bila shaka kufariki kwake ni pigo kubwa sana – tena katika umri mdogo wa miaka 25 tu!

Written by simbadeo

April 15, 2012 at 4:23 pm

Udereva … na Madereva

with 2 comments


Kazi kwelikweli. Tukisema kwamba pengine zaidi ya asilimia 70 ya madereva Dar es Salaam ni wale wa ‘leseni za kuletewa’ kuna watu watapiga kelele. Haya sasa … nani abanwe hapo? Nafikiri ni muhimu viboko vitembezwe kutoka kule zinakotolewa leseni, idara inayokagua leseni hizo, vyuo ‘vinavyotoa mafunzo ya udereva’ hadi ‘madereva’ wenyewe. Tukiwa na madereva wa namna hii … nguzo za barabarani, kingo za barabara, waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, waendesha pikipiki na hata vyombo vingine vya moto vitaponea wapi dhidi ya ajali? Ama kweli kila kitu kinawezekana Bongo … na ni Bongo pekee!

Written by simbadeo

April 13, 2012 at 10:55 pm

Mnazi … Manufaa mengi

leave a comment »


Wengi tumezoea kula madafu. Hii ni hasa kwa watu wa ukanda wa pwani. Dafu moja hivi sasa jijini Dar linauzwa kwa kati ya sh500 na sh700.

Hata hivyo, kuna bidhaa nyingine inayotokana na mnazi. Hii inaitwa ‘moyo wa mnazi’. Nayo pia inaliwa. Wapo ambao huitumia kuandaa saladi. Inasemekana kwamba moja ya kazi zake mwilini ni pamoja na kusafisha figo. Changamoto tu ni kwamba, ili ‘moyo wa mnazi’ upatikane, ina maana kwamba ndiyo mwisho wa mnazi huo. Maana ni lazima uangushwe na kisha ile sehemu ya juu (kichwa cha mnazi) ndiyo kichukuliwe ili kupata moyo wake. Ni bidhaa adimu. Siku ukikutana nayo … hasa katikati ya jiji … Mtaa wa Jamhuri … onja. Bei inaanzia Sh500 na kuendelea kutegemeana na ukubwa wa kipande.

Enjoy maisha ya pwani …

Written by simbadeo

April 13, 2012 at 10:47 pm

Posted in Siasa na jamii