simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Baiskeli … Suluhu kwa foleni jijini Dar?

with 3 comments

Nimeipenda hii. Imagine asilimia 75 ya watu wanaotumia magari yao binafsi kwenda na kurudi kazini (kwenye biashara) hapa jijini Dar wangekuwa wakitumia baiskeli. Naamini foleni zingepungua sana kwenye barabara za jiji hilo, au siyo? Vilevile, watu wangekuwa na afya bora zaidi … vitambi vingepungua, maana kuendesha baiskeli ni mazoezi mazuri sana ya mwili.

Labda maofisi ingebidi yawe na maji zaidi na mabafu ili watu wakiingia waoge na kubadili nguo … Si unajua tena hali ya Dar ilivyo? Lakini pamoja na changamoto hiyo, bado nafikiri kwamba Dar ingekuwa mahali bora zaidi na hata hali ya hewa ingekuwa safi zaidi. Hebu fikiri kuhusu moshi wa magari unavyochafua hewa … na sauti za honi na mingurumo zinavyoondoa utulivu … Aaaah Bongo!

Advertisements

Written by simbadeo

April 16, 2012 at 12:33 am

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Safi sana nimependa hii inapunguza usumbufu wa kubanana kwenye daladala na pia unapata na mazoezi.

  Like

  Yasinta/kapulya

  April 16, 2012 at 3:15 pm

 2. Good idea Simba but watu wanapenda kuugua magonjwa ya matajiri kama BP, kisukari nk kwani wanajua hayo tangu zamani lakini hawataki hata pikipiki; sasa wanataka magari kama ya Kanumba, ya milioni miambili na kuendelea! Ila bado kuna changamoto kwani Tanga kuna baiskeli kama utitiri na kila siku ajali zinatokea. Tanga kama huna gari, hakuna dala dala, hivyo wengi wanapenda baiskeli, huna baiskeli utakodi taxi na bei ni juu. Je hapa tukichukua baiskeli ili kuendana na ugumu wa maisha, haitakuwa na maana kuwa ajali zitaongezeka? Pia tukibuni kuendana na umaskini ambao kikwelikweli hatuna, ila wakubwa wanagawana pato letu, si ndiyo tutawapa nafasi ya kuendelea kutunyonya? Ki ukweli, ukiwa na mfanyakazi mwenye gari itabidi mshahara wake utoshe na kuendesha gari lake na kwa logic hii mtu akiwa na baiskeli hahitaji gharama kubwa kuiendesha.

  Like

  Reginald

  April 18, 2012 at 10:24 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: