simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Muungano Day … Ni safari ndefu

with 2 comments

Bado dakika chache tuanze kusherehekea Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Muungano huu unatimiza miaka 48. Ni umri wa mtu mzima. Ni umri wa mtu ambaye katika hali ya kawaida anakuwa na majukumu mazito katika familia na jamii yake. Ni umri wenye kuheshimika ikiwa mtu unajiheshimu.

Tangu kuwepo kwa Muungano huu jamii ya Watanzania imenufaika na mengi. Katika muungano huo, nchi ilihimili vishindo na mikiki ya Vita Baridi kati ya Magharibi na Mashariki. Katika zama hizo, Tanzania ilijipambanua kama Taifa lenye falsafa makini na uwezo wa kuchagua nani awe rafiki na nani asiwe rafiki. Taifa lilikuwa na kauli na kauli hiyo ilisikilizwa na hata wale wanaojiona wao ndiyo wakubwa katika ulimwengu huu.

Chini ya Muungano huu pia Taifa lilishinda Vita vya Uganda na kufanikiwa kumng’oa Nduli Idd Amin Dadaa. Ikumbukwe kwamba chini ya ‘Uwezo Tunao, Sababu Tunayo, Nia Tunayo’ wapiganaji kutoka pande zote mbili za Muungano walishiriki. Hii ilituingiza katika undugu ule wa damu. Kuna watu — bila shaka umewahi kusikia — huingia udugu kwa kuchanjiana damu. Tanganyika na Zanzibar ziliingia kwenye udugu wa aina hii wakati wa vita vile.

Kuna upungufu pia. Bado Muungano wetu haujafaulu sana katika kukomboa wananchi dhidi ya maadui wale wakubwa: Umaskini, Maradhi na Ujinga (Siku hizi kuna adui mpya aliyeingia – Ufisadi). Sina hakika kama nje ya Muungano kila upande ungekuwa umepiga hatua kubwa zaidi. Sina njia ya kupima jambo hilo. Lakini kwa ujumla maisha ya watu wa kawaida bado ni ya shida sana.

Upungufu mwingine ulio karibu na huo uliotangulia ni kule kukua kupita kiasi kwa tofauti ya kimapato na hali ya kimaisha kati ya wachache walio nacho na wengi wasio nacho. Hili ni tatizo kubwa. Hili ni jambo litakaloendelea kuutikisa Muungano watu tupende au tusipende.

Upungufu mwingine, nao unakaribiana na huo wa kwanza hapo juu, suala la UTEGEMEZI kwa mataifa ya nje ni ugonjwa mkubwa sana unaotudhoofisha kibinadamu. Miaka 48 ya Muungano bado tunatembeza bakuri kwa wafadhili? Hapa Muungano bado haujafaulu. Hatuna budi kurejea kwenye itikadi yetu ya kutafuta kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Tukifaulu kupunguza na hatimaye kuondosha utegemezi wetu kwa mataifa ya nje, hapo tutarejea kuwa na kauli inayosikilizwa, kauli inayoheshimiwa. Hivi sasa, hawa mabwana wakubwa watatuendesha tu kama wanavyotaka. Wakitaka uranium yetu — watajichotea kwa bei karibu na bure; wakitaka mafuta na gesi vivyo hivyo. Aah. Uhuru wetu utabaki kuwa wa bendera.

Vinginevyo, ninawapongeza sana Watanzania wa pande zote mbili kwa kutimiza miaka 48 ya Muungano. Kwa pamoja tumeonyesha njia kwamba Afrika inaweza kuwa moja. Sharti tuanze hatua kwa hatua. Nchi moja moja, kanda moja moja hatimaye bara zima.

Masuala ya kumeguka kwa nchi kama ilivyokuwa kwa Sudan ni sehemu muhimu ya kuelekea kwenye Bara moja, kwani ni lazima kwanza kuvunjilia mbali ile mipaka iliyolazimishwa na wakoloni ili kupata mipaka ya asili. Baada ya hapo safari ya kuungana itaanza kwa kasi na nguvu mpya.

Tumeweza. Tusonge mbele. Tuweke haki, heshima na umoja mbele. Kila mmoja atimize wajibu wake vile inavyompasa … kwa kuanzia.

Advertisements

Written by simbadeo

April 25, 2012 at 11:33 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Muungano ni suala muhimu sana katika maendeleo ya binadamu. wahenga walisema kidole kimoja hakivunji chawa. lakini ikiwa muungano ni wa mashaka ni heri kuondoa mashaka haya mapema. na pia ilisemwa lisemwalo lipo kama halipo laja, ni heri kumaliza tofauti zinazosikika polepole mapema maana heri nusu shari kuliko shari kamili. kama watu wana mashaka na muungano tatizo ni nini? nani anasema anaonewa na kwa nini kuwe na wale wamesema na hawa hawakusema, wakati sisi ni wamoja? je tukiuvunja tutapata suluhisho lenye kuleta maendeleo? na tukiuimarisha tutafika wapi?

  binafsi najipongeza kuwa katika nchi yenye mundo tofauti na wengine, kwani najua wanatutamani, nao wangeungana, cha msingi ni kuangalia tatizo liko wapi hadi watu watake kufanya mageuzi ya chinichini. kisha tufanyie kazi tusonge mbele. kama kauli ya miaka 50 inavyosema, tumethibutu kuungana, tukaweza sasa basi tusonge mbele kwania njema.

  suala la utegemezi ni kuwa sisi watanzania tumekuwa wavivu na wa kwanza kulalamika kuwa tunaonewa, katuonea nani? kazi ndogo hatuwezi tutaweza kubwa? unaendesha bajaji umechafukaa ukipewa lori, watu hawakuoni si ndio hata nguo hutavaa? angalia watu wanafika kazini saa ngapi na wanafanya nini wakifika ofisini? mazungumzo gani wanayo? wakitoka kazini wanaenda wapi? kujiendeleza au kujipendekeza? tubadilishe msimamo, mtu akifanya kazi kwa bidii akifanikiwa tunasema kawa free manson ( hili sijui ni kundi, chama, dini au kazi , mie sijui), hizo ni fikra duni katika ulimwengu unaokwenda kasi kwa maendeleo na uvumbuzi.

  Hongera watanzania wotee

  Like

  jennifer

  April 26, 2012 at 8:51 am

  • True. Muungano ni muhimu sana kwa maendeleo. Hekima, ustahimilivu, kujitambua. Kuelewa nini ni mambo ya muhimu kwetu sote ndiyo nguzo za kudumisha muungano. Tuna safari. Tunaweza.

   Like

   simbadeo

   April 27, 2012 at 12:18 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: