simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kitabu Kipya … Asili Halisi ya Mwanadamu

with 4 comments

Asili ya Bin-Adam kama kilivyoandikwa na Maalim Juma Kinyemi …

Mama Bahati Jonathan Mbwambo, mke wa mwandishi, akionyesha moja ya nakala za kitabu hicho

Mwandishi anasema hivi juu ya kazi yake hii:
“Madhumuni ya Historia hii siyo malumbano, tuhuma wala masahihisho, ila ni kuweka mwelekeo ulio wa kweli katika hali ya dunia na matendo ya binadamu. Kwa wale ambao watajaliwa kupitia maelezo ya kitabu hiki, watagundua kwamba nia yangu ni kutoa mwangaza kwa binadamu wote wanaokusudia kuupata mwangaza huu popote pale duniani bila kujali imani yao ya dini.” Maalim Juma Kinyemi.

Msomaji Athmani Iddi Millanzi alipata kusema haya alipopata bahati ya kusoma muswada katika hatua zake za mwanzo:

“Nilipomaliza kusoma rasimu hiyo, kabla ya kuonana na mwandishi wa kitabu, sina budi nikiri kuwa nilikuwa na mawazo ya kwamba mwandishi wa kitabu hiki lazima angekuwa msomi wa hali ya juu sana mwenye elimu isiyo chini ya shahada. Kutokana na mambo yaliyomo ndani ya kitabu hiki kuwa:
1. Ya ajabu kwani yalikuwa ambayo nadhani siyo kwangu tu bali bali kwa yeyote atakayesoma, hayapo kabisa kwenye kitabu au andiko lolote ambalo tayari limechapishwa.
2. Linamhusu kila binadamu wa kale na wa leo kwa vile yanazungumzia Historia ya ‘Adam na Hawa’ wanaokubalika duniani kuwa ndiyo chanzo cha binadamu yeyote ambaye alikuwapo au yupo bila kujali ni wa dini gani, kabila gani, itikadi gani au kutoka pande gani katika dunia hii ya Mungu.”

Ili kujipatia nakala yako kwa Sh15,000 tu andika barua pepe kwa anwani hii: fgdtanzania@gmail.com au P.O. Box 40331, Dar es Salaam, Tanzania.

Tukikaribishe kitabu hiki kwa mikono miwili. Kinaongeza idadi ya vitabu bora vinavyoendelea kuchapishwa nchini Tanzania, yote ni kwa manufaa ya binadamu wa sasa na wa kizazi kijacho. Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

August 27, 2012 at 8:12 am

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. ntakitafuta kwa kila hali na mali ahsante kwa taarifa!!

  Like

  yasinta

  August 27, 2012 at 5:20 pm

 2. naombeni idadi ya watu tanzania 2012

  Like

  ERNEST OSOKY

  October 8, 2014 at 11:19 am

 3. Amesoma Thiology?

  Like

  Edward Dunia

  April 6, 2015 at 8:47 pm

  • Ndugu Edward, asante kwa swali. Kuna Theology rasmi (kama wanayojifunza Wakristo au Waislamu) na kuna ile ya asili (Elimu Mungu) itokanayo na mapokeo na maono ya mtu. Nafikiri ni hii ya pili aliyotumia yeye. Pengine utafute kitabu hicho na kujisomea na kisha kuamua. Asante sana.

   Like

   simbadeo

   April 8, 2015 at 4:38 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: