simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for March 7th, 2012

World Women’s Day … Tuwaenzi

leave a comment »


Mama ambaye kwaye mimi nilizaliwa. Cecilia Paul Shabani Ntunguminso Mnyang’ombe (Kulia) akiwa na mdogo wake. Nafurahi kuwatambulisha kwenu wadau. Feb. 2010.

Mwanamama niliyewahi kumkuta wakati natoka tarafa ya Mwese kuelekea Mpanda. Mtoto anakula raha. Tunatoka mbali … Sijui kwa nini tunapokua huwa tunaishia kujawa na kiburi na majivuno wakati ambapo tunatoka katika hali ya kutoweza kujifanyia chochote. Ubinadamu kweli ni kazi, kazi kubwa. Feb. 2010.

Dada binamu. Esther Tanganyika. Wilayani Mpanda. Feb. 2010.

Hii ni maalumu kwa ajili ya kuwaenzi akina mama popote pale walipo. Naamini duniani pamekuwa bora zaidi kwa uwepo wao. Hebu fikiria kama tungekuwa ni dunia ya midume mitupu … LA HAULA. Kusingekuwepo hata chembe ya huruma. Pengine hata maendeleo yasingekuwapo, maana kuna msemo ule ‘nyuma ya mafanikio ya mwanamume yeyote, yupo mwanamke’. Pengine watu wasingekuwa hata na motisha wa kujishughulisha. Wanawake wana nafasi yao katika kututia hamasa ili kujibidiisha zaidi. Pengine ni vema tutazame zaidi upande ule mzuri wa uwepo wa wanawake. Barani Afrika, wamekuwa na mchango mkubwa. Mtawakumbuka akina Bibi Titi Mohamed, Winnie Mandela, Malkia Nzinga, Mama Maria Nyerere … na wengine wengi. Tuna haki ya kujivunia kuwepo kwa wanawake. Tushirikiane nao katika kuifanya dunia iwe mahali bora zaidi pa kuishi. Amen.

Written by simbadeo

March 7, 2012 at 11:41 pm

Posted in Siasa na jamii

Black and white … Kupewa … au … kujipa?

leave a comment »


Kesho tunaposherehekea Siku ya Wanawake Ulimwenguni. Tuwape nafasi … au … wajipe nafasi? Tuwashirikishe … au … wajishirikishe? Tuwahusishe … au … wajihusishe? Tuwakaribishe … au Wajikaribishe? Tuwawezeshe … au Wajiwezeshe? Mie ningechagua upande wa pili … Mara nyingi tunataka kusubiri tufanyiwe kitu/jambo fulani … hapana … tuanze sisi kuchukua hatua … tena hatua madhubuti. Nawaambia akina mama mchukue hatua … muwe proactive katika kujisimimia maslahi yenu … msisubiri kupewa. Jamani … hapa sijazungumzia Ubunge wa Viti Maalumu … tafadhali … msinitafsiri vibaya … Tupo pamoja.

Written by simbadeo

March 7, 2012 at 12:19 am

Posted in Siasa na jamii