simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Archive for October 2008

Kopitan – reprographic rights organisation

leave a comment »


It was on 10th October 2008 at Blue Pearl Hotel & Apartments, Ubungo Plaza, Dar es Salaam when a Reprographic Rights Organisation to be known as KOPITAN was born.

Top: Interim chairperson of Kopitan, Abdul Saiwaad.

Middle: Members of the floor who witnessed the event.

Down: Mr John Kitime, famous musician and member of COSOTA board, was also present.

Safari bado ni ndefu. Waandishi, watunzi, wabunifu, wachoraji, wachongaji, wafinyangaji, wanamuziki, waigizaji na wasanii wa fani mbalimbali bado hawafaidi vya kutosha matunda ya kazi zao. Ni jukumu letu sote kuenzi na kutuza ubunifu wa aina yoyote kwa kuzingatia taratibu za haki miliki na haki shiriki. Tuwasaidie wanasanaa wetu popote walipo.

Written by simbadeo

October 17, 2008 at 10:16 pm

Posted in Siasa na jamii

Jeshi…

leave a comment »


Nani mwenye uwezo wa kulimiliki jeshi hili? Je, tunao ubavu wa kudhibiti biashara za mkononi? Je, hali itakuwaje miaka mitano, kumi au zaidi ijayo?

Ama kwa hakika hapa tunapaswa kufikiri kwa bidii. Hapa sadaka kubwa inahitajika. Kiongozi shupavu tu ndiye atakayeweza kumaliza changamoto hii ya umachinga. Uchumi serious haupaswi kuwa na biashara aina hii kwa kiwango tulicho nacho.

Tukiwa na viongozi walio ‘visionary’, committed and courageous tutaweza. Mungu Ibariki Tanzania.

Ni Kibaha Maili Moja, Jumamosi 4 Oktoba 2008.

Written by simbadeo

October 8, 2008 at 9:44 pm

Posted in Siasa na jamii

A-town ndani ya nyumba

leave a comment »


Moja ya vikwangua anga huko A-town. Vinavutia.

Written by simbadeo

October 8, 2008 at 9:32 pm

Posted in Siasa na jamii

UDA katika jiji 2008

leave a comment »


Katika blogu ya Da Chemi Che Mponda aliweka picha ya basi la UDA kama yalivyoonekana mwaka 1974 hapa jijini Dar es Salaam. Juzi nimeona basi hili la UDA kama yanavyoonekana siku hizi. Pamoja na hayo, bado usafiri wa umma ni kimbembe kwa wakaazi wa jiji la Dar. Mpaka sasa bado ni mipango, mipango, mipango, mipango. Utekelezaji umebaki wa kusuasua kama si kubabaisha.

Tupo pamoja.

Written by simbadeo

October 3, 2008 at 1:22 pm

Posted in Siasa na jamii

Eid-el-Fitr in pictures …

leave a comment »


Ni hekaheka mitaani. Nyakati za sherehe kubwa, kama vile Idi na Krismas, watoto ndiyo wanaosherehekea kwa namna ya pekee. Pengine ni kutokana na kukosekana kwa maeneo mengi mazuri ya wazi ya burudani kwamba watoto humiminika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Hapo utakuta makundi ya watoto mamia kwa mamia kutoka pande mbalimbali za jiji la Dar es Salaam na viunga vyake.

Pichani ni watoto waliofika Uwanja wa Ndege kusherehekea sikukuu ya Idi ya mwaka 2008. Ni wakati jiji na manispaa wabuni maeneo zaidi ya wazi kwa ajili ya matukio kama haya.

Heri ya Idi al Fitri.

Written by simbadeo

October 1, 2008 at 8:09 pm

Posted in Siasa na jamii

Majengo ya Machinga …

leave a comment »


Majengo ya Machinga jijini Dar es Salaam yaliyo katika eneo la Karume. Majengo haya yaliyo katika pande mbili za barabara ya Kawawa yataunganishwa kwa daraja kama inavyoonekana pichani. Mafundi wako katika hekaheka za kujenga daraja hilo. Haya ni maendeleo muhimu. Nina imani tu kuwa kimo cha daraja, mita 4.5 hazitaleta mgogoro hapo baadaye.

Written by simbadeo

October 1, 2008 at 7:47 pm

Posted in Siasa na jamii

Teknolojia na maendeleo

leave a comment »


Usafirishaji wa mitambo Bongo Dar es Salaam. Inafurahisha kwamba tunaanza kutumia teknolojia hata kama ni kwa upande wa watumiaji na si waundaji. Hatua hii bila shaka itatupeleka katika hatua nyingine. Hatua muhimu ya kubuni, kuunda na kusambaza zana za teknolojia.

Written by simbadeo

October 1, 2008 at 7:34 pm

Posted in Siasa na jamii