simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Posts Tagged ‘ilala

Opportunities through Emerging Technologies

leave a comment »


20160407_104922

Phone charging. The less your cell phone battery lasts, the more lucrative somebody’s business becomes. As technology advances rapidly so are new opportunities created. Imagine charging each phone for Sh300 (US dollar cents 15) per two hours … the guy collects a relatively handsome amount a day. The ideal places include markets where traders would do anything to ensure that their phones are functioning fully.

This is the beauty of technology. Keep creating. Keep imagining. Keep producing.

Photo: At a stall within the Mchikichini Market, Ilala, Dar es Salaam.

Advertisements

Dar na Mvua … Hali Halisi ya Barabara Zetu

leave a comment »


Kamata, Kariakoo, Dar es Salaam

Kamata, Kariakoo, Dar es Salaam

Labda swali la kujiuliza hapa … miaka nenda, miaka rudi, kila inaponyesha mvua eneo hili hujaa maji kama hivi. Ni hatari kwa vyombo vya moto. Ni hatari kwa waenda kwa miguu. Ni hatari kwa watumia mikokoteni na hata baiskeli, hivi kwa nini mamlaka inayohusika na barabara hii haichukui hatua ya kukomesha tatizo hili? Kama ni halmashauri ya jiji, au Manispaa ya Ilala au TAROADS … kwa nini suluhu ya kudumu isitafutwe? Mbona kutoka hapa mpaka baharini hakuna umbali unaozidi kilometa moja na nusu? Kwa nini pasichimbwe mfereji wa kuelekeza maji ya mvua huko? Au hili nalo inabidi nchi iende kutembeleza kombe la ombaomba Ulaya?

Inaudhi … sana!

Written by simbadeo

April 11, 2013 at 9:53 pm

Dar Mitaani … Siamini Macho Yangu

leave a comment »


Kama siamini macho yangu vile! Tunaanza kuona kazi za sanaa kwenye mitaa ya Darisalama. Hizi ni katika Mtaa wa Makunganya, katikati ya jiji. Kwangu ilikuwa mshtuko kidogo … maana mambo haya hatukuzoea kuyaona hapa. Nipongeze mamlaka inayohusika na mpango huu. Ni mwanzo mzuri na hauna budi kuendelezwa. ILA tafadhali sana tuwashirikishe wanasanaa wa hapa nchini katika kufanya kazi hizi. Wao ndiyo wanaofahamu vema kabisa vionjo vya Watanzania. Kwa kuwahusisha wao, ni njia ya kukuza kazi za sanaa hapa nchini ili zipate kuthaminiwa kama zinavyostahili.

Kupitia sekta ya sanaa, nchi itapata fursa ya kukuza na kudumisha utamaduni wake; itazalisha nafasi nyingi za ajira; itachangia kuongezeka kwa kasi ya kukua kwa uchumi; itaimarisha thamani ya mwanadamu na ubinadamu na hata kukuza viwango vya kufikiri, namna ya kupanga vipaumbele katika maisha na mipango yetu ya mtu mmoja mmoja na ile ya Taifa — yaani katika kutazama hasa substance na si accident. Pamoja sana!

Written by simbadeo

September 2, 2012 at 11:00 pm

Posted in Siasa na jamii

Tagged with , , , ,

Airtel … mng’aro

leave a comment »


Ni katika makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Kawawa, eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam. Ni uwekezaji wa maana. Uwekezaji unaotoa ajira kwa maelfu ya watu … moja kwa moja na kwa njia zisizo za moja kwa moja.

Hakuna ubishi kwamba huduma ya mawasiliano imepiga hatua kubwa sana. Moja ya hatua zilizopigwa ni pamoja na kupunguza gharama za kupata habari. Wale wa kizazi changu watakumbuka kwamba zamani zile kama unataka kuwasiliana na mtu, say, yeye anaishi Ubungo, na wewe unaishi Ilala, basi ilikulazimu kusafiri hadi Ubungo. Hapo, fikiria: unatumia nauli (kwa gharamza za sasa hivi mathalani si chini ya mia 600 ili ufike Ubungo kutoka Ilala), na zaidi sana unatumia sio chini ya saa 4 ili kutimiza azma yako hiyo. Siku hizi, mawasiliano yapo kwenye ncha za vidole. Papo hapo unampigia, unazungumza naye ulichotaka kuzungumza na mambo yanakwisha. Unaokoa gharama. Unaokoa muda.

Lakini, mabadiliko haya pia yanatugharimu kijamii. Mawasiliano ya kwenye simu na yale ya kuonana ana kwa ana ni tofauti. Ana kwa ana mnazungumza mengi zaidi. Kuna hata yale mawasiliano yasiyotumia maneno lakini yanayoeleza na kufafanua kile mwingine anachokizungumza — hayo huwezi kuyapata kupitia simu.

Kwa hiyo, hata sasa tunahitaji ‘balancing’ ili kwamba tusipoteze kabisa physical contacts kwa sababu kuna simu.

Tafakari ya leo. Pengine wewe pia una maoni kuhusu mawasiliano ya siku hizi kwa kulinganisha na mawasiliano ya kizamani. Yamimine hapa maoni hayo.

Written by simbadeo

May 6, 2012 at 9:54 am