simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Waasisi wa Taifa Letu: Julius Nyerere na Abeid Karume

with one comment

Nyerere and Karume rare photo

Tunapoelekea katika Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar, ni muhimu tutafakari mchango wa waasisi wetu, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume. Tunaingia katika sherehe za mwaka huu tukiwa bado hatujapata ufumbuzi wa mgogoro uliotokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi uliopita upande wa Zanzibar.

Tujitafakari kama kweli tumekomaa vya kutosha kama Taifa (lenye umri wa zaidi ya nusu karne) kiasi cha kushindwa kufikia maelewano. Tunaweka mfano gani kwa vizazi vijavyo? Tunaweka mfano gani kwa mataifa yanayotuzunguka? Pande zinazohusika zimekuwa zikikutana kwa takriban miezi miwili sasa, lakini hakuna taarifa za ndani ya vikao hivyo zinazoufikia umma. Ni wazi umma mzima wa Watanzania ni wadau katika hili, kwa nini wasifahamishwe kuhusu yanayoendelea?

Tuna hazina ya hekima ya waasisi wetu, hata kama hatunao leo kiroho, lakini walituachia maandiko mengi, huma tunaweza kupata ufumbuzi. Zaidi sana tukumbuke kuwa tunajenga nyumba moja, kwa nini tupigane vita? Kwa nini tutiane vidole vya macho?

Pamoja sana.

Heri ya Mwaka Mpya 2016 kwa kila mmoja wetu.

Advertisements

Written by simbadeo

January 7, 2016 at 2:25 pm

One Response

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kuasisi jambo si kazi ndogo, inahitaji uwezo na falsafa iliyo na mashiko. Unapobadili taswira ya uasisi katika kazi ya kitaaluma na utalamu wake uwe na jambo mbadala, si kuvuruga na kuvurunda kwa ajiri ya kutafuta sifa tu.

  Tumieni fursa mlizo nazo kuwaunganisha Watanzania wote, hiyo ni njia mahususi ya kukua na kuendelea kwa Taifa lililo na Umoja na si vinginevyo.

  Kumbukeni wakoloni walitugawa ili watutawale kiurahisi zaidi, na kinchotokea sasa ni kurudi katika mikono ya kujigawa yaani ” DIVIDE AND RULE”. Kwa ujumla falsafa hii haina nafasi kwa nchi zinazotanuka na kukua Kimataifa hususani katika nyanja za Uchumi,Kijamii na Kisiasa.

  Wapo wanaowagombanisha na kuwachonganisha ili wawatawale, wapo vibaraka wanaoandaliwa na waliopo kutumikia falsafa za wanyonyaji kwa mifumo ya unyonyaji wa kisasa, tuwe makini na watu wa aina hiyo , la sivyo Taifa litakosa mwelekeo na kuangamia kabisa.

  Like

  Deo Isaack Kapufi

  February 25, 2016 at 12:27 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: