simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Merry Christmas. Noeli Njema. 2015

with 7 comments

20151225_094711

This is to wish a Merry Christmas to all fans and readers of this blog and other social networks associated with it. May the day bring joy and plant the seeds of peace in our societies. Let there be peace always and the rest will follow.

Stay blessed.

Hii ni maalumu kuwatakia Furaha ya Noeli kwa wapenzi na wasomaji wote wa blogu hii pamoja na mitandao mingine ya kijamii inayohusiana nayo. Siku hii ilete furaha na kupanda mbegu za amani katika jamii zetu. Sote tujibidishe kuleta amani na mengine yote yatafuatia.

Ubarikiwe sana.

Advertisements

7 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Nawe pia noeli njema!

  Like

  Yasinta

  December 26, 2015 at 8:37 pm

 2. BWANA DEO SIMBA,
  UBARIKIWE SANA.
  SINA MENGI YA KUNENA LEO ZAIDI YA KUWATAKIA HERI NA FANAKA ZA MWAKA MPYA WA 2016, WEWE NA FAMILIA YAKO.
  BAADA YA KUFAHAMU KUWA U MJUKUU WA MZEE MNYANG’OMBE NAJISIKIA KWAMBA NAWASILIANA NA NDUGU YANGU.
  KWA WAKATI MUAFAKA TUTAONGEA ZAIDI TULIVYOISHI NA MZEE MWENYE UPEKEE KWA UPENDO, BUSARA NA HEKIMA ALIYEITWA MNYANG’OMBE.

  Like

  RWAKA RWA KAGARAMA

  December 30, 2015 at 1:31 am

  • Ndugu Kagarama

   Asante sana kwa kututakia heri. Nasi tunafurahi sana. Kwa hakika teknolojia imetuunganisha tena. Naam, descendants wa Mzee Mnyang’ombe ni wengi. Tumetawanyika sehemu mbalimbali katika uso huu wa dunia. Kwa hakika hata yeye anafurahi huko aliko. Mwenyezi Mungu amrehemu. Tuzidi kuwasiliana na kupashana habari. Asante sana.

   Like

   simbadeo

   December 30, 2015 at 4:03 pm

 3. MASAA YASIYOZIDI 19 YAMEBAKIA KABLA YA KUUFIKIA MWAKA MPYA WA 2016, MANDHARI YA MWESE YANAKUJA MAWAZONI. NDANI YAKE NAIONA TASWIRA YA MZEE MMOJA TU AITWAYE MNYANG0MBE. NAIONA TASWIRA HIYO PEKE YAKE SABABU MAWAZO YAMEFOCUS KWA MZEE HUYU TU NA KUMBUKUMBU YAKE KWANGU NI KAMA VILE TULIKUWA PAMOJA JANA JIONI. HATA MAMBOYE MEMA KWANGU HATA KWA WENGINE YATAKUWA MAPYA KIPINDI CHOTE CHA MAISHA YANGU.
  Nayakumbuka yafuatayo:
  # Kaya ya Mzee MNYANG’OMBE, Ilokuwa mithili ya Ikulu ya Mtemi, kwa uwingi wa nyumba (Majumba na vijinyumba, vikiwemo vijumba vidogo vya watoto wakubwa wa kiume na wa kike, bila kusahau nyumba xa wageni walioonekana siku zote hapo na vijumba vya mababu na mabibi waliokuwa wanaendelea kukumbukwa kama watakatifu waliotangulia Mbinguni (mizimu yetu). Vile vile kulikuwa na uwingi wa vihenge na mizinga ya asali iliyoanzia katika mashamba yaliyokuwa jirani ya kaya yake mpaka mapori ya mbali huko msimbazi. Alikuwa na maeneo ya mizinga yake hata sehemu nyingine za mbali kama Ngondo na kwingineko.
  Namkumbuka sana akiwa nyumbani kwa Mzee KAGARAMA (rafiki yake mpenzi) wakinywa pamoja kwa tabasamu na maongezi mema yenye utulivu, pombe ya BUKI kutokana na asali za MNYANG’OMBE ambapo baba alikuwa mteja wake na kutokana nazo alikuwa anatengeneza pombe ya kinyarwanda iliyokuwa inaitwa INZOGA Y’UBUKI. Baba alikuwa ndiye mwenye kilabu kikubwa cha pombe kienyeji kipindi hichoooo Mwese nzima, kabla ya mwaka 1973.
  #Bado ninaipata ladha ya ugali mweupeee sana, mtamu na nyama tamu za pori, nilizokuwa nakula kwa Mzee MNYANG’OMBE kila nikitumwa huko na baba. Kama kuna sehemu niliyokuwa nafurahia sana kutumwa na baba yangu Bwana SIMBA, ni numbani kwa babu yako, kwamba wakati mwingine nilikuwa namuuliza baba kwa nini zimepita siku nyingi bila kunituma huko. hebu nawe fikiria Babu au mmoja wa mabibi zako alikuwa ananifungashia hata asali ya kulamba tu wakati narudi kwetu Namba tatu, njiani nailamba weeeeere mpaka nilipofika jirani ya shule ya msingi ya Mwese. JE ALIYEKUWA ANAKUFANYIA MAMBO HAYO UTOTONI, UNAWEZA KUMSAHAU ?
  Baada ya kusoma ujumbe ulionijulisha kwamba wewe ni mjukuu wa Mzee MNYANG’OMBE, nilikuwa peke yangu ofisini kwangu, kwa ukweli machozi yalinidondoka kwa hisia nilizopata. Natamani sana kama ingewezekana ikapatikana jinsi ninavyoweza kumtumia bibi yako zawadi ya kitenge au baadhi ya mama zako wadogo waliokuwa wananisongea ugali kwa furaha na kunikaribisha kwa ukarimu na upendo mwingi walorithi kwa MTAKATIFU MNYANG’OMBE.

  #Naikumbuka siku Mzee MNYANG’OMBE alipobatizwa na familia yake parokiani Mwese kama vile ilikuwa jumapili iliyyopita. Ilikuwa sikukuu. Na kipindi hicho si wabende tu hata wazee wa kinyarwanda baadhi yao walikuwa hawajabatizwa akiwemo na ndugu ya babu yangu Mzee NYABIRANDA wa No.7 ambaye alikataa katakata kubatizwa ujanani, akaendeleza ibada zetu za jadi mpaka tulipokuwa Mwese.Alikubali kubatizwa baadaye sana alipokuwa karibu kufariki.

  #Namkumbuka Mzee MNYANG’OMBE mwenye kipara kizuri tu, kinachong’ara akiongoza mkutano wa usuluhishi katika maeneo ya kaa yake. Nakumbuka kwamba wakati mwingine nikifika kwake, nilikuwa namkuta akiwasuluhisha watu ambao wengine siwafahamu, ikionekana kwamba nafikiri walitoka mbali kuitafuta suluhu itokanayo na busara na hekima za mzee wetu.
  JAMBO AMBALO HUWA NAJIULIZA KWA SABABU HILO SIKUWAHI KULITAMBUA. JE MZEE MNYANG’OMBE ALIKUWA MTWARE? AU ALIKUWA NI RAIA WA KAWAIDA ALIYEKUWA NA VIPAJI BORA TU VYA UPENDO KWA WOTE, HEKIMA NA BUSARA NA JUHUDI NA BID KAZINI? (maana alikuwa anaifahamu fika thamani ya KAZI. na jambo hili lilijidhihirisha kwa yeyote aliyefika kwa Mzee MNYANG’OMBE.)
  ######
  EE BWANA EE TUTAENDELEA BAADAYE KWA SABABU NI MENGI SANA NINAYOKUMBUKA KWA MZEE WETU AMBAYE KATIKA UJUMBE HUU WAKATI MWINGINE NAMTAJA KWA USASA KAMA VILE YUKO HAI.
  SIKUJIDANGANYA, MZEE MNYANG’OMBE ATAENDELEA KUWA HAI MOYONI MWANGU SAMBAMBA NA WAZAZI WANGU KAGARAMA NA MUKAMURERA. NINAAMINI ATAKUWA HAI HATA KTK MIOYO YA WANAMWESE WANAOMFAHAMU NA WANAOENDELEA KUPUMUA. NA ZAIDI YA YOTE YUKO HAI NDANI YA VIZAZI VYAKE AMBAVYO VITAENDELEA KUPEPEA NA KUENEZA BENDERA YA MZEE WETU PANDE ZOTE ZA DUNIA KUTOKA KTK KAYA HIYOOO ILIYOTENGENEZWA NA MZEE MNYANG’OMBE KIJIJINI No.6 MIAKA KADHAA ILIOPITA.
  MZEE MNYANG’OMBE ANAAMBATANA NA HISTORIA YA MWESE .
  #########
  MUNGU ATUBARIKI WOTE NA AEENDELEE KUWALINDA WANA, WAJUKUU, VITUKUU, VILEMBWE NA VILEMBWEKEZO VYA MZEE MNYANG’OMBE POPOTE WALIPO DUNIANI.

  Like

  RWAKA RWA KAGARAMA

  December 31, 2015 at 2:14 pm

  • Ndugu Kagarama

   Asante sana kwa historia fasaha ya Mzee Mnyang’ombe. Kwa hakika, mimi binafsi nimeangaziwa mengi na tafakari uliyofanya kuhusu maisha yake. Kwa hakika yeye ni babu yangu, lakini nikiri kwamba kwa maelezo uliyotoa sasa nimemfahamu vizuri zaidi. Nakushukuru sana.

   Tuendelee kubadilishana mawazo. Salamu kwa wote huko nyumbani na katika shughuli zako za kila siku.

   Ubarikiwe sana.

   Wasalaam

   Deo Simba

   Like

   simbadeo

   January 7, 2016 at 2:29 pm

 4. ASANTE SANA BWANA SIMBADEO, MUNGU AENDELEE KUKUBARIKI WEWE, FAMILIA YAKO NA UKOO MZIMA WA MZEE WETU MNANG’OMBE.

  Like

  Rwaka rwa Kagarama.

  February 9, 2016 at 11:07 am

 5. HERI YA MWAKA MPYA WA 2017, FAMILIA YA MZEE MNYANG’OMBE POPOTE MLIPO.

  Like

  rwaka rwa kagarama

  January 17, 2017 at 1:08 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: