simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Waziri Atupiwa Ndizi … Italia

with 2 comments

Bi Cecile Kyenge, Waziri wa Mshikamano nchini Italia. Waziri huyu ni wa kwanza mweusi nchini humo. Alizaliwa Congo.

Bi Cecile Kyenge, Waziri wa Mshikamano nchini Italia. Waziri huyu ni wa kwanza mweusi nchini humo. Alizaliwa Congo.

Ubaguzi … Waziri Mweusi Italia arushiwa ndizi

Wanasiasa nchini Italia wamepokea kwa hasira taarifa za kitendo cha kutupiwa ndizi kwa waziri wa kwanza mweusi nchini humo wakati wa mkutano wa hadhara wa kisiasa.

Waziri wa Mshikamano Cecile Kyenge, ambaye amewahi kupitia vitendo kama hivyo vya ubaguzi miaka ya nyuma, alikipuuza kitendo hicho akisema ni “upotevu wa chakula”.

Lakini Waziri wa Mazingira Andrea Orlando alisema kupitia ukurasa wake wa Twita kwamba alijisikia “kudhalilishwa mno” kufuatia kitendo hicho.

Mapema mwanzoni mwa mwezi huu seneta mmoja wa Italia aliomba radhi baada ya kutamka kwamba Bi Kyenge alimkumbusha kuhusu orungatan (jamii ya sokwe wasio na mikia).

Bi Kyenge aliyezaliwa nchini Congo alikuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Democratic Party (PD) huko Cervia Ijumaa iliyopita wakati mtu mmoja ambaye hajatambuliwa bado alipomtupia ndizi zilizomkosakosa waziri huyo wakati akiwa jukwaani.

Polisi nchini Italia wanasema wanamsaka mtuhumiwa kwa hatua zaidi za kisheria.

Kupitia Twita, Bi Kyenge, alieleza tukio hilo kama la “kusikitisha” na “upotevu wa chakula”.

“Ujasiri na shauku ya kubadili mambo lazima ipite kila kitu kuanzia chini hadi ngazi za juu za taasisi,” alisema.

Wanasiasa wa Italia walimwunga mkono siku ya Jumamosi kwa kumutumia ujumbe na maneno ya mshikamano huku wakilaani kitendo alichofanyiwa.

Waziri wa Elimu Maria Chiara Corrozza alimsifu Bi Kyenge kwa ujasiri wake na nia yake thabiti a kusonga mbele hata kama mazingira si ya kirafiki.

Chanzo: http://www.bbc.co.uk/news/world-europe-23480489

Maoni: Safari yetu wanadamu katika kuvuka makandokando (accidents) yanayotuzunguka kama vile rangi, dini, mali, asili, kusoma au kutosoma bado ni ndefu. Tunaweza kuwa binadamu bora zaidi kwa kushinda makandokando hayo. Pengine ile ‘kanuni ya dhahabu’ ingetusaidia sana kama tungeizingatia kila mahali na katika vitendo vyetu vya kila siku: Mtendee mwenzako vile ambavyo ungependa yeye akutendee.

Advertisements

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Waliomtupia ndizi Waziri huyo walikuwa na maana kuwa yeye ni nyani [monkey] kwani huko Ulaya nyani anasifika kwa kupenda ndizi mbivu. Sisi weusi tuliokaa Ulaya siku za nyuma na kushuhudia ubaguzi tunatambua ishara hiyo. Lakini kabla hujwa maarufu hujatukanwa kwa hiyo Wazir Kyenge sasa atajulikana Ulimwengu mzima na kusifika!Mimi nilikuwa sijui kama Italia kuna Waziri Mweusi wa Asili ya Kiafrika!!

  Like

  Canute W Temu

  July 28, 2013 at 10:49 pm

 2. Acheni ubaguzi ulio waziwazi, mfano kutuhumu na kukashifu kwa njia ya rangi mnafikiri huo ni uungwana hasa nyie mlorusha ndizi huko Italy. Si kitambo ni nyie mlokuwa na hekaheka za kumtuhumu Rais Robert mugabe wa zimbabwe kwa kuwatimua Zimbabwe watu weupe kwa sababu kama hizo za kundi fulani wanaweza jingine hawezi, hali imekwisha, ni vipi na nyie mkafungiwa msitoke nje ya Italia patakalika , kuweni wastaarabu.

  Like

  Deo Isaack Kapufi

  August 30, 2013 at 5:28 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: