simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Nelson Mandela Day … Apata Nafuu, Upendo Wasisitizwa

leave a comment »

Former South African President Nelson Mandela during his meeting with Conservative Party leader David Cameron at The Dorchester in central London. PRESS ASSOCIATION Photo. Picture date: Sunday June 29, 2008. Watch for PA story POLITICS Mandela. Photo credit should read: Johnny Green/PA Wire

Former South African President Nelson Mandela during his meeting with Conservative Party leader David Cameron at The Dorchester in central London. PRESS ASSOCIATION Photo. Picture date: Sunday June 29, 2008. Watch for PA story POLITICS Mandela. Photo credit should read: Johnny Green/PA Wire

Na Associated Press, Updated: Wednesday, July 17, 9:34 PM

Johannesburg. Nelson Mandela amepata ‘nafuu kubwa’, na huenda atarejea nyumbani ‘wakati wowote kuanzia sasa’, alisema binti yake Zindzi siku moja kabla kiongozi na shujaa huyo mashuhuri hajatimiza umri wa miaka 95.

“Nilimtembelea jana na alikuwa akitazama televisheni huku akitumia mashine za kusikilizia (headphones),” alisema Zindzi Mandela wakati wa mahojiano na Kituo cha televisheni cha Sky cha nchini Uingereza. “Alituachia tabasamu pana na kunyanyua mkono wake … anawasiliana kwa macho na mikono.”

Mandela anazidi kupata “nguvu na umadhubuti”, alisema binti yake. “Ninafikiri atarejea nyumbani hivi karibuni”.

Maelezo haya ya Zindzi — ambaye ni mmoja wa mabinti zake kwa mke wake wa pili, Winnie Madikizela-Mandela — ni hatua kubwa kutoka katika mivutano ya kimahakama iliyoikumba familia hiyo mapema mwezi huu ambapo nyaraka za mahakama zilisema kwamba alikuwa katika hali mbaya na kwamba maisha yake yalikuwa yakisaidiwa na mashine maalumu na kwamba alikuwa akikijongelea kifo.

Mandela amelazwa kwenye hospitali moja jijini Pretoria tangu tarehe 8 Juni na maofisa wamekuwa wakisema kwamba hali yake ilikuwa mbaya lakini isiyoyumbayumba.

Habari hizi za kupata nafuu kwa Mandela zitawatia moyo wanaomwunga mkono nchini Afrika ya Kusini na kote duniani na ambao wamekuwa wakijiandaa kusherehekea anapotimiza mwaka wake wa 95 tangu kuzaliwa kwake — leo Alhamis tarehe 18, 2013, siku ambayo imetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Siku ya Mandela lengo likiwa ni kutambua mchango wa mshindi huyu wa Zawadi ya Nobeli katika amani na upatanisho.

Mvuto katika Siku ya Kimataifa ya Mandela iliamshwa na kulazwa hospitalini huko Pretoria kwa shujaa huyu, na tayari watu wanatafuta namna gani wapate kuenzi fikra zake adimu.

Taasisi moja ya jijini Johannesburg ambayo imepewa jina la Mandela pamoja na vikundi vingine vingi vimewaomba watu kujitolea dakika 67 kufanya vitendo vya upendo katika jamii ili kuoanisha na miaka 67 ambayo Mandela ameitumikia jamii yake. Mandela aliiongoza Afrika ya Kusini katika kipindi kigumu kutoka siasa za ubaguzi wa rangi kwenda kwenye demokrasia na alikuwa rais wa kwanza katika uchaguzi uliohusisha watu wa rangi zote wa nchi yake mwaka 1994.

Rais Jacob Zuma anatarajiwa kusherehekea siku hii ya Mandela kwa kusimamia utoaji misaada kwa familia za watu weupe maskini jijini Pretoria, sambamba na ujumbe wa Baraza lake la Mawaziri kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mandela kwa kulenga kukuza usalama wa chakula, upatikanaji wa malazi na kufuta ujinga.

Image source: http://www.google.co.tz/imgres?imgurl=http://www.wineandbowties.com/wordpress/wp-content/uploads/2011/07/madiba62.jpg&imgrefurl=http://wineandbowties.com/culture/style/nelson-mandelas-shirts/&usg=__iS-KPBZxOfOIoaaBK3KuCEmsKnw=&h=2969&w=2759&sz=2517&hl=en&start=17&zoom=1&tbnid=4PdEsoGkHGU4hM:&tbnh=150&tbnw=139&ei=kQDnUcH4DIbetAa9yIGoCQ&prev=/search%3Fq%3Dnelson%2Bmandela%2Bphotos%26sa%3DX%26biw%3D1052%26bih%3D553%26tbs%3Disz:l%26tbm%3Disch&itbs=1&sa=X&ved=0CE4QrQMwEA

Watanzania

Tuchukue mafundisho ya maridhiano, kustahimiliana, kuchukuliana, kuelewana, kupendana na kuthaminiana. Tuchukue kauli hii ya Mandela na kuifanyia kazi: “Poverty is not an accident like slavery and apartheid, it is man-made and can be removed by actions of human beings”, yaani, ‘Umaskini si ajali kama ilivyokuwa utumwa na ubaguzi wa rangi, bali ni kitu kilichoundwa na watu na kinaweza kuondolewa kwa binadamu kuchukua hatua stahiki.”

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: