simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Afya … Maswali Sita ya Kuokoa Maisha Yako

with one comment

Orodha ya Ukaguzi kwa Upasuaji Salama

Orodha ya Ukaguzi kwa Upasuaji Salama

Maswali Sita Yanayoweza Kuokoa Maisha Yako

Na Cathy Edwards BBC

Kukagua upya vitu vidogovidogo kunaweza kuhakikisha kwamba mgonjwa mnayejiandaa kumfanyia upasuaji ni yule aliye sahihi, utaratibu kama huo unaweza kuokoa hadi nusu milioni ya watu duniani kote.

Kuna wagonjwa ambao wamewahi kuripotiwa kufa kwa sababu wapasuaji waliondoa kiungo kisichostahili, waliacha zana za upasuaji kwenye miili yao, au hata kumfanyia upasuaji fulani mgonjwa asiye sahihi (kesi kama hiyo imewahi kutoka katika Hospitali ya Mifupa ya Moi iliyoko Muhimbili).

Mwaka 2008, Shirika la Afya Duniani, lilizindua Orodha ya Ukaguzi kwa ajili ya Upasuaji Salama ili kukabiliana na makosa ya kibinadamu kama hayo. Hata hivyo, mpango huo umekuwa vigumu kutekelezeka katika mataifa yanayoendelea.

Je, maswali haya yanayoweza kuokoa maisha yako ni yapi?

1. Je, mnamfanyia upasuaji mgonjwa aliyekusudiwa?

Pengine inaweza kuwa vigumu kuaminika, hutokea mara nyingi tu kwamba mgonjwa anayefanyiwa upasuaji anakuwa siye yule aliyekusudiwa. Huko Marekani, kosa hili huhusisha visa kati ya 200 hadi 300 kila mwaka.

Kukugua ili kuhakikisha kwamba mtu aliyelala kwenye meza ya upasuaji ni suala muhimu mno. Ni muhimu kufanya hivyo mara mbili: mara moja kabla ya kumwekea mgonjwa dawa ya usingizi na mara ya pili kabla ya kuanza kufanya upasuaji wenyewe.

2. Je, mnafanya upasuaji sahihi?

Hili ni jambo lingine linalopaswa kukaguliwa mara mbili.

‘Kupasua pasipo sahihi’ ni operesheni ambazo pia si za kushangaza, hasa pale inapohushisha kupasua kushoto au kulia.

Katika kisa kimoja ambapo mtu alipoteza maisha baada ya figo nzima kuondolewa, mpasuaji alisema kwamba aliitazama picha ya X-ray visivyo kabla ya upasuaji wenyewe.

Nchini Rwanda, ambako ni hospitali chache tu zinazotumia utaratibu huu wa orodha ya ukaguzi, mtu mmoja mzima alipelekwa kwa upasuaji baada ya kuvunjika paja la kulia. Aliamka saa chache baadae na kuambiwa kwamba alikuwa amewekewa msumari katika upande usio sahihi na kwa hiyo ilibidi upasuaji uanze upya.

3. Je, unajua jina na kazi ya kila mmoja aliye kwenye timu ya upasuaji?

Je, mnafahamiana na wenzako?

Je, mnafahamiana na wenzako?

Pengine hili ni jambo ambalo kwa sababu ya muda kupita sana, timu za upasuaji zinaweza kugomba: kwa nini wanataka tujitambulishe?

Lakini, kutambulishana sio tu kunasaidia watu kufahamiana na pia kujua wajibu wa kila mmoja kwenye operation, bali pia zinasaidia wataalamu hawa kuzungumza hili na lile wakati wa upasuaaji, anasema mtaaalamu mmoja, Dkt Isabeau Walker.

“Daima kuna mtu ambaye ataona kitu au jambo lisilo la kawaida. Endapo watu hao wameshatambulishana, kuna uwezekano mkubwa zaidi wa mtu huyu kuzungumza.”

4. Je, mashine ya kuwekea dawa ya usingizi imekaguliwa?

Ingawa orodha yenyewe inachukua tu dakika chache kuitekeleza, inahushisha hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kabla katika ukaguzi jumla wa mashine zote.

Hii ni hatua muhimu sana hasa katika mataifa yanayoendelea ambako karibu asilimia 40 ya vifaa vya afya huwa havifanyi kazi, ikilinganishwa na asilimia 1 tu katika mataifa yaliyoendelea.

Mbinu za kisasa na ufuatiliaji umepunguza vifo kutokana na tatizo hili hadi kubaki 1 katika 200,000 katika nchi zilizoendelea.

Lakini nchini Togo, uwezekano wa mtu kufariki kwa sababu ya dawa za usingizi na maumivu ni juu sana kwa uwiano wa mtu 1 katika 133. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2005.

5. Je, viwango vya oksijeni kwa mgonjwa vinatazamwa?

Viwango vya oksijeni katika damu ya mgonjwa hukaguliwa kwa kifaa cha kuangalia mapigo ya moyo — pulse oximeter — kifaa hiki huunganishwa kwenye kidole au sikio la mgonjwa na hutoa mlio pale viwango vinapopungua.

Karibu asilimia 70 ya vyumba vya upasuaji katika nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara huendeshwa bila vifaa hivyo.

6. Je, mmeondoa vifaa vyote vya upasuaji kutoka kwenye mwili wa mgojwa baada ya kukamilisha kazi?

Vifaa vya upasuaji ... ni baadhi tu.

Vifaa vya upasuaji … ni baadhi tu.

Mwanamke mmoja nchini Uganda alifariki baada ya kitambaa cha usafi chenye ukuwa wa nchi 12 kuachwa mwilini baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji. Wakati kitambaa hicho kilipogunduliwa, kilikuwa tayari kimeshaungana na utumbo wa mwanamke huyo.

Kuna hatua tatu za ukaguzi: “wakati wa kuanza”, yaani kabla ya kuwekewa dawa ya usingizi; “muda kuisha”, yaani kabla ya upasuaji wa kwanza kufanyika; na “wakati wa kumaliza kazi”, yaani kabla mgonjwa hajatolewa kwenye chumba cha upasuaji.

Moja ya ukaguzi wa mwisho inahusisha kuhesabu vifaa vyote vilivyotumika, ikiwa ni pamoja na sponji, sindano — ili kwamba makosa yale yanayoweza kusababisha kifo yasitokee.

Chanzo: http://www.bbc.co.uk/news/health-23252784

Advertisements

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Tunashukuru sana madaktari wetu kwa kazi mnazofanya za kutoa tiba mahususi. Hakika tabibu mzuri hupenda kazi yake lakini hitilafu hutokea kwa dharula zisizopingika, mfano kukatika kwa umeme na kiza kutanda vyumba vya upasuaji hii inaweza kuleta madhara makubwa na hata kusahau baadhi ya vifaa mwilini. Natoa wito kwa wale wote wanaoshughulika na nishati ya nguvu za umeme wawe makini, wasikate kate umeme hovyo kwa mambo yao ya ajabu ajabu, au masiasa, tumezoea kuona masiasa yanaingia hata katika nishati za uendeshaji na uokoaji wa maisha, swali nani ni abunuwasi hapa ? ni watalamu wetu au mafundi mitambo ? Muwe wa kisasa mtajenga jamii inayodumu.

    Like

    Deo Isaack Kapufi

    August 30, 2013 at 5:24 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s