simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ajali … Ndege Yaanguka, Wawili Wafariki Dunia

with one comment

Ndege iliyoanguka huko San Francisco. Watu wawili wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 150 kujeruhiwa. Ilikuwa na jumla ya abiria 291 na wafanyakazi 16.

Ndege iliyoanguka huko San Francisco. Watu wawili wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 150 kujeruhiwa. Ilikuwa na jumla ya abiria 291 na wafanyakazi 16.

Watu wawili wanasadikiwa kufariki na wengine 150 kujeruhiwa baanda ya ndege moja kuanguka huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa San Francisco, kwa mujibu wa taarifa kutoka Idara ya Zimamoto.

Ndege ya Asiana Airlines, Boeing 777 iliyokuwa ikitokea Seoul, Korea ya Kusini, inaaminika kuwa na abiria 291 na wafanyakazi 16.

Idara ya Zimamoto ya San Francisco ilisema kwamba watu 181 wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali, 49 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Ugaidi umechukuliwa kwamba si chanzo cha ajali hiyo, Shirika la Upelelezi la FBI lilithibitisha.

Mashahidi walitoa taarifa kwamba mkia wa ndege ulikatika wakati wa ajali hiyo. Wizara ya Usafirishaji ya Korea ya Kusini ilisema kwamba mkia wa ndege hiyo ndio ulianza kukita chini kabla ya ndege kuanguka kabisa.

Moto ulianza kuwaka baada ya ndege kuwa ardhini na abiria walilazimika kutumia milango ya dharura ili kujiokoa, mashahidi walisema.

Vipande vya mkia wa ndege vilitawanyika huku na kule katika barabara ya kutulia ndege. Picha ya televisheni ilionyesha upande wa juu ukiwa umeungua vibaya na injini moja kung’oka.

David Eun, anayesadikiwa kuwa mmoja wa abiria kwenye ndege hiyo, alituma ujumbe wa Twita: “Nimepata ajali ya ndege sasa hivi katika uwanja wa SFO. Mkia wote umekatika. Watu wengi wako salama. Mimi pia ni mzima. Hii ni kweli.”

Chanzo: Yahoo! News.

Blogu hii inatoa pole kwa wale waliopotelewa na jamaa zao katika ajali hiyo. Vilevile, inatoa pole nyingi za faraja kwa majeruhi. Tunawatakia kupona mapema.

Advertisements

Written by simbadeo

July 7, 2013 at 8:19 am

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Ajali nyingi hutokea, lakini si zote zinatokea kwasabsbu ya ule usemi wa ” Bahati mbaya anajua Mungu ” nyingine husababishwa na watu na hali za hewa , si lazima kusema aa amependa Mungu , natia shaka kumsingizia Mungu muda fulani ,sababu nyingine si Matakwa ya Mwenyezi Mungu. Tuchukue tahadhari.

    Like

    Deo Isaack Kapufi

    August 14, 2013 at 1:53 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: